Mwanamke mwanaharakati

Mwanamke mwanaharakati

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
MWANAMKE MWANAHARAKATI

Na, Robert Heriel

Siku hizi dunia imebadilika na kuchukua sura ya kisogo. Kumeibuka makundi ya watu wajiitao wanaharakati katika mambo mbalimbali katika jamii. Wanaharakati walikuwepo tangu kale, zamani za mababu na enzi ya enzi. Zamani wanaharakati walijipambanua kama watumishi wa Mungu, manabii, na mitume. Hawa walitetea haki ya Mungu, walitetea sheria za Mungu pale walipoona zinasiginwa. Hata hivyo huwezi utenganisha uanaharakati na sheria za Mungu. Mwanaharakati sharti apiganie sheria za Mungu, huyo atatambulika kama mwanaharakati.

Ajabu siku hizi wapo waasi, wahalifu, waovu ambao hujivika uanaharakati wa kutetea mambo ya hovyo, hutetea mambo ya kishetani ambapo kimsingi ni mawakala wa kuiangamiza dunia.

Wapo wanaharakati wanaotetea Mashoga, wapo wanaharakati wanaotetea wasagaji, wapo wanaharakati wanaotetea ndoa za jinsia moja, wapo wanaharakati wanaotetea haki za kutukana watu, kutukana viongozi wa nchi au wadini, wapo wanaharakati wanoua watu wa dini zingine ili dini yao itawale eneo husika, n.k

Leo nitaangazia upande wa WANAWAKE WANAHARAKATI.

Mwanamke mwanaharakati ni mwanamke mcha Mungu, mwema aliyeamua kutumia wema wake kama mfano wa kuigwa ndani ya jamii kwa kuwafundisha, kuwakomboa wanawake wenzake kutoka katika uovu mpaka kuwa wema kama yeye kusudi kuijenga jamii.
Hii ni tofauti na wanawake waliowengi siku hizi ambao hujivika koti la uanaharakati kumbe ni wahuni, makahaba, wachawi na watafutao mambo ya kishetani.

Mwanamke mwanaharakati hukemea na kuonya tabia mbaya za wanawake wasiowaheshimu waume zao, huwafunza wanawake jinsi ya kuwa wake wema, hukemea tabia mbaya za wanawake wenye umalaya, wabishi, wenye mdomo, wasiowasikivu na adabu ndani ya ndoa.

Mwanamke mwanaharakati ambaye siku zote ni mcha Mungu lazima awe ndani ya ndoa, na kama hayupo ndani ya ndoa basi ijulikane kuwa alishafiwa na mumewe hivyo ni Mjane. Na ifahamike alikuwa mke mwema kwa mumewe. Lakini mwanamke yeyote atakayejiita mwanaharakati hasa wa kukomboa wanawake wenzake asipokuwa ndani ya ndoa na inajulikana alikuwa hana sifa njema kwa mumewe basi huyo atambulike kama muhuni, mpotoshaji, muasi na asipewe nafasi ya kuongea.

Wapo wanawake wahuni ambao ndoa ziliwashinda zamani kwa upumbavu wao, leo wanageuka washauri. Hawa siwezi kuwaita wanaharakati bali watatambulika kama waasi ni kama shetani aliyefukuzwa mbinguni sasa anatafuta wafuasi wake huku duniani. Wanawake wa dizaini hiyo huharibu ndoa nyingi badala ya kuziponya.

Nampenda mwanaharakati mmoja ambaye nimetumia picha yake hapo chini, huyu si mwingine ni Irene Mbowe Kungwi Lao Dada Irene ni moja kati ya wanawake wanaharakati hapa nchini ambao ni tunu kwa taifa hili. Irene Mbowe ni mama aliyejipambanua kama Kungwi, mwandishi, mjasiriamali, mpiganaji, na mwalimu wa wanawake ambaye anatumia nafasi yake kuelimisha jamii.

Huyu ni Mfano wa mwanamke Mwanaharakati kwa kuwa kila jambo analichukulia katika namna ya kusuluhisha na sio kufarakanisha na kutenganisha. Hutoa mafunzo, hutoa uzoefu wake wa kimaisha hasa katika ndoa, changamoto za ndoa na namna ya kuzikabili, hushauri watu hasa wanandoa kinamama na kinadada wajikite zaidi kwenye maombi kuombea ndoa zao. Hii ni kusema Irene Mbowe anaamini Mungu huweza kuzifanya ndoa ziwe na amani.

Dada Irene ni Mama anayejipenda, mwenye kuvutia pengine kwa wanaume wengi, huenda hilo pekee yake lingemfanya ajisikie, ajivunie na awe kiburi na jeuri ndani ya ndoa yake. Kama wanawake wengi wapumbavu wanavyohadaiwa na uzuri wao. Lakini Irene hayupo hivyo, uzuri wake sio kitu, anajua hata angekuwa mzuri kama malaika wa kule Tibeli nilipoandika habari zake, bado atabaki kuwa mwanamke, ambapo atapaswa kusimama kama mama na mke wa familia.

Hii ni tofauti na wanawake wapumbavu ambao wamejivika uanaharakati kupotosha jamii ya wadada wadogo wanaochipukia kwenye ndoa. Wanawake wapumbavu labda anamvuto fulani au pengine asiwe nao labda anadanganywa anao. Basi hujigeuza kiburi na jeuri ndani ya ndoa, heshima hana wala adabu, kutwa kumfuruga mume wake, ambapo kwa wanaume wasiotaka mchezo huishia kuwazaba makofi ili akili ziwakae sawa.

Wanawake hawa wapumbavu mara zote hushawishi utengano, umalaya, uasi, uchawi na ushirikina, haki sawa, n.k

Irene Mbowe licha ya mwonekano wake, yeye kama Mwanaharaki na mwalimu kwa wanawake wenzake hilo halijali, ni mjasiriamali wa uji, anauza uji bila kujali ataonekana vipi. Pengine kama angekuwa mpumbavu angejiona uzuri wake, nafasi yake ndani ya jamii haiendani na biashara yake ya Uji lakini sivyo. Anauza uji na anafurahia kazi yake. Kupitia kazi hii anaonyesha mambo kadhaa mathalani; yeye sio mtu wa majivuno kwani angekuwa na majivuno asingeuza uji.
Pili, anawafunza wanawake wenzake kuwa, wasiangalie wapoje bali wafanye kazi yoyote iingizayo kipato bila kujali wataonekana vipi.

Nafahamu Irene alifiwa na Mume wake(pole sana Irene) Hili lilikuwa jaribu kubwa kihisia, kimwili, na kiuchumi. Lakini katika hatua za kukabiliana na jambo hilo, aliamua kuuza uji kukabiliana na changamoto za kiuchumi. Hii ingekuwa kwa mwingine hasa yule mwanamke mpumbavu, ingekuwa tiketi ya kufanya ufuska, kudanga ati akisingizia kuwa mumewe amefariki. Lakini sio kwa mwanamke mwanaharakati ambaye lazima awe mke mwema.

Mwanamke mpumbavu atakwambia mume wake hamuachii pesa ya matumizi, wakati yeye kutwa kucha hana alifanyalo. Ukimuambia uza genge hataki, uza chapati hataki, uza vitumbua hataki, anachotaka ni kupewa pesa. Ukimuuliza kwa nini hutaki kufanya kazi usishangae akakuambia yeye ni mzuri, yeye ni mwanamke, yeye ni yeye...... mpaka ushangae.

Mwanamke mpumbavu huzaa watoto wapumbavu, mwanamke mvivu huzaa watoto wavivu, mwanamke anayechagua kazi huzaa watoto wanaochagua kazi, si ajabu kizazi cha sasa kwa nini vijana wengi huchagua kazi, jibu lake litakuwa wazi.

Nakupongeza Dada Irene Mbowe Kungwi Lao kwa huduma zako kwenye jamii ya kitanzania, taifa linabarikiwa mno hasa kwa kinadada na kinamama ambao watakufuatilia katika mtizamo chanya.

Nasisitiza zaidi, mwanamke mpumbavu sharti apigwe akili imkae sawa, bila kujali nani atasema nini.

Hata hawa wanaharakati wa kijamii na kisiasa wanaotetea mambo ya hovyo, sijui ushoga, sijui ndoa za jinsia moja, sijui wanaotukana watu mwatusi ya nguo iwe viongozi au raia, wote wapigike, wachapike, wasagike mpaka wamalizike. Huwezi jifanya mwanaharakati kwa upuuzi au kuvunja sheria za Mungu, utapigwa kama utakufa tutakuzika, kesi zitafuatia.

Mwisho nimalize kwa kuwapongeza wanawake wanaharakati wote Tanzania mnaowakilisha Wake wema, wenye hekima mliotoka kwa Mungu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Naona umeamka na hasira kweli na wanawake wanaharakati
 
Umenena vema kabisa.
Hao wanaharakati wanaotetea mambo ya ovyo hawahitajiki Tz.
Waendelee kutetea haya mambo wakiwa hukohuko yanapofanyika.Sio huku.
 
Kwahiyo kwenye macho ya watu ni wanaharakati, lakini gizani yanayofanyika mi mengine! [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]

Wewe mtu atetee mashoga asiwe shoga kweli? atetee wachawi asiwe mchawi, atetee watukanaji asiwe mtukanaji, atetete malaya asiwe malaya. kwa kawaida mtu hujitetea, iwe kwa tabia za nje au tabia za ndani zilizojificha. psychoanalysis theory inaeleza hivyo
 
Wewe mtu atetee mashoga asiwe shoga kweli? atetee wachawi asiwe mchawi, atetee watukanaji asiwe mtukanaji, atetete malaya asiwe malaya. kwa kawaida mtu hujitetea, iwe kwa tabia za nje au tabia za ndani zilizojificha. psychoanalysis theory inaeleza hivyo
Mara nyingi mtu hutetea kile afanyacho
 
Umesema ukweli mtupu mkuu na hili bandiko nitalisambaza lisomwe na watu wengi zaidi.
 
Back
Top Bottom