BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
MWANAMKE AWEZA KUWA CHIFU?
Taarifa kuwa Rais Samia Suluhu amepewa hadhi ya Chifu kule Mwanza zimepelekea baadhi ya watu kuhoji kama kunaweza kuwa na Chifu mwanamke. Mchango wa Askofu hapa chini unalenga kupanua wigo wa mjadala kwa lengo la kuelimisha.
Neno Chifu, limetolewa kutoka katika neno la Kiingereza la Chief. Neno chief lina maana ya kiongozi ye yote hata wa nyumba kumi. Mbeya kuna makabila mengi, watawala wa jadi wanaitwa kwa majina tofauti tofauti. Wanyakyusa tunaita 'Malafyale'. Malafyale daima ni mwanaume na hata watoto wake wa kiume hujulikana kama banyafyale. Lakini mtoto wa kike wa malafyale ni undenga na mke wa malafyale ni umwehe.
Hivyo, ikitokea (ingawa haijawahi kutokea) mtoto wa kike akatawala, kama hajaolewa ataitwa undenga na kama ameolewa ataitwa umwehe. Hata mke wa malafyale anaitwa umwehe, hata akitawala (haijawahi kutokea) huitwa umwehe. Kuna jamii hapa Tanzania zilozowahi kutawaliwa na wanawake. Historia ambayo kwa sehemu kubwa iliandikwa na wanaume, haikuweza kuandika kumbukumbu za kutosha kuhusu watawala wa jadi waliokuwa wanawake.
Mtoto wa kwanza wa Malafyale Korosso Mwamakula aliitwa Sekela Itenda. Huyu alifikisha miaka 94 au 96. Alipendwa na aliheshimiwa sana. Aliishi katika Kijiji cha Itunge ambako alikuwa ameolewa na mtoto wa Mchungaji Munndekesye Mwamwaja aliyeitwa Gwilisoni (Wilson) Mwasogwe.
Mama Samia Suluhu alipewa jina la Sekela na baadhi ya banyafyale alipokwenda Kyela alipokuwa Makamu wa Rais, na hivyo kujulikana kama Sekela Itenda II. Kikwete pia alipewa hadhi ya Malafyale Mwangupili II.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula