Mwanamke na Uchifu

Mwanamke na Uchifu

Paskali nenda kawaambie leo hivi hao wazee wako wakisukuma waliomwita Samia chief uone kama hawajakukimbiza na mikuki.
Nikawaambie nini na nani, wakati waliomtawaza Samia kuwa Chief Hangaya, mkuu wa Machifu ni Chifu mkuu wa Wasukuma.
P
 
Nikawaambie nini na nani, wakati waliomtawaza Samia kuwa Chief Hangaya, mkuu wa Machifu ni Chifu mkuu wa Wasukuma.
P
Ni kwasababu ya uchawa tu na kujipendekeza mkuu. Labda na pressure fulani kutoka juu ila kiuhalisia ni ngumu. Mfumo dume upo sana tu tena usukumani huko nilienda bibi mtu mzima ananisalimia mimi under 20 anapiga magoti.
 
Hiyo ni heshima, nadhani wanawake wa Kisukuma ndio wanaongoza kwa heshima. Hata uchelewe kurudi home saa ngapi, huulizwi. Simu hagusi!. Hata upigiwe saa ngapi huulizwi. Kiukweli ningekuwa ushauri wa wanawake wa kuoa, ningeshauri watu wakaoe Usukumani.

Asee ngoja nijitahidi kuoa huko. Lakini mkuu Pasko hawa watoto wa siku hizi zi wameshachakachuliwa na utandawazi kweli watakuwa na maadili kama ya vizazi vya nyuma?
 
Malkia Chifu Nzinga Mbande.....

Hivi hayati Mfalme Phillip "Duke of Edinburgh" alikuwa ni "mtawala" kwa kuwa tu ni mfalme na si MALKIA Elizabeth?!!!

SIEMPRE CHIFU WA MACHIFU HANGAYA🙏
 
Hiyo ni heshima, nadhani wanawake wa Kisukuma ndio wanaongoza kwa heshima. Hata uchelewe kurudi home saa ngapi, huulizwi. Simu hagusi!. Hata upigiwe saa ngapi huulizwi. Kiukweli ningekuwa ushauri wa wanawake wa kuoa, ningeshauri watu wakaoe Usukumani.
P
🤣🤣👋👋👋👋
 
MWANAMKE AWEZA KUWA CHIFU?

Taarifa kuwa Rais Samia Suluhu amepewa hadhi ya Chifu kule Mwanza zimepelekea baadhi ya watu kuhoji kama kunaweza kuwa na Chifu mwanamke. Mchango wa Askofu hapa chini unalenga kupanua wigo wa mjadala kwa lengo la kuelimisha.

Neno Chifu, limetolewa kutoka katika neno la Kiingereza la Chief. Neno chief lina maana ya kiongozi ye yote hata wa nyumba kumi. Mbeya kuna makabila mengi, watawala wa jadi wanaitwa kwa majina tofauti tofauti. Wanyakyusa tunaita 'Malafyale'. Malafyale daima ni mwanaume na hata watoto wake wa kiume hujulikana kama banyafyale. Lakini mtoto wa kike wa malafyale ni undenga na mke wa malafyale ni umwehe.

Hivyo, ikitokea (ingawa haijawahi kutokea) mtoto wa kike akatawala, kama hajaolewa ataitwa undenga na kama ameolewa ataitwa umwehe. Hata mke wa malafyale anaitwa umwehe, hata akitawala (haijawahi kutokea) huitwa umwehe. Kuna jamii hapa Tanzania zilozowahi kutawaliwa na wanawake. Historia ambayo kwa sehemu kubwa iliandikwa na wanaume, haikuweza kuandika kumbukumbu za kutosha kuhusu watawala wa jadi waliokuwa wanawake.

Mtoto wa kwanza wa Malafyale Korosso Mwamakula aliitwa Sekela Itenda. Huyu alifikisha miaka 94 au 96. Alipendwa na aliheshimiwa sana. Aliishi katika Kijiji cha Itunge ambako alikuwa ameolewa na mtoto wa Mchungaji Munndekesye Mwamwaja aliyeitwa Gwilisoni (Wilson) Mwasogwe.

Mama Samia Suluhu alipewa jina la Sekela na baadhi ya banyafyale alipokwenda Kyela alipokuwa Makamu wa Rais, na hivyo kujulikana kama Sekela Itenda II. Kikwete pia alipewa hadhi ya Malafyale Mwangupili II.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula​

View attachment 1929969
Siongezi neno .
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom