Mwanamke ni vizuri pia kujifunza ku-fix baadhi ya vitu hapo nyumbani

Sasa mkuu unaposema kubadili bulb hujui watu wana bulb tofauti? Ya kawaida iko chini? Inahitajika ngazi nzuri na ndio vitendea kazi vyenyewe. Hizo kazi nyingi ni rahisi tu kama una vitendea kazi. Kama huna hata kubadili bulb sio kazi rahisi tena.
Chief kwamba kwenye hiyo nyumba hata ngazi inakosekana! Sawa umeeleweka. Lakini nijuavyo kwenye nyumba iliyokamilika vipo vitu ni lazima visikosekane kama vile ngazi, spade, nyundo, msumeno.
 
Umenikumbusha kituo changu Cha kwanza Cha kazi kijijini hukoo kwenye nyani....kota nimepewa jiko hakuna...nikaona ee isiwe shida....darasa la sita wa kiume mkuje...enhee,zile tofali za shule njoo tuchanganye tope hapa tuinue kajiko kakimtindo.....kakafika juu.....tukaingia porini kata miti ndo kenchi hizo.....laza pale....ikasalia bati ....hizo zikasubiri nipate mshahara nikajinunulia bati sita,misumali(nyundo ninayo sikuzote),nikaazima ngazi kijijini panda juu nikaanza kazi ya kuezeka....nikizipanga bati jike na dume pale....wanakijiji walisimama barabarani kunishangaa mie nipo juu Sina habari.Usitegemee nguo kuchanika nipeleke kwa fundi,au sijui kubadilisha bulb....au kunabanda la mbao kufugia kuku lahitajika ati nitamwita fundi...utasubiri
 
Mafundi tukale wapi, hao ndio wateja wetu wazuri na wanalipa pesa kubwa kwa kazi ndogo, tunatumia hadaa kidoo tu na sio watata kama vidume.
 
Hivi kitanda kinatakiwa kifanyiwe Service mara ngapi kwa mwezi, Ngoja nimpe hii kazi mamsap.
 
Ndo ujishangae sasa
 
utamkuta mwanamke hata kushona kifungo ya shati mpaka apeleke kwa fundi
 
Ndo ujifunze sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…