Mwanamke niliyemsaidia na kumpenda ametoroka na mtoto wangu

Mwanamke niliyemsaidia na kumpenda ametoroka na mtoto wangu

ibra87

R I P
Joined
Jul 22, 2015
Posts
5,614
Reaction score
5,351
Habari za jioni wakuu,

Kuna vitu ambavyo unaweza kukutana navyo katika maisha yako ya kila siku na ukavihifadhi katika moyo wako na kufanya siri kubwa ambayo kamwe hutataka kumwambia mtu yoyote yule.

Katika maisha ambayo nimeishi hapo kabla ikiwa bado sijakutana na huyu mpenzi niliyenae sasa nilibahatika kuzaa na msichana mmoja aitwaye Sheila.

Alikuwa ni msichana ambaye nilikutana nae kibahati mbaya sana, nasema kibahati mbaya sana kwa kuwa mazingira tuliokutana yalikuwa ni mazingira ya msaada zaidi, baada ya kumkuta maeneo ya Posta Mpya saa tano za usiku akiwa amejiinamia.

Sikujua nikitu gani ambacho kilinisogeza pale lakini nilijikuta tayari nikiwa mbele yake huku nikionyesha roho ya ubinadamu ikiwa ni pamoja na kuuliza ni lipi tatizo ambalo linamsibu.

Binti yule hakutaka kunijibu wala kunisikiliza alichokuwa anakifanya ilikuwa ni kunitazama tu na kunibinulia mdomo kwa dharau kubwa. Kusema kweli binti alikuwa ni mrembo sana na alikuwa anavutia sana.

Kijana nikaona nitangaze msaada huku moyoni nikiwa na mipango yangu mingine. Kweli baada ya vuta nikuvute binti akakubali kuondoka na mimi kuelekea Kigamboni ninakoishi huku akiweka angalizo la kutokumsumbua tukifika huko.

Mdomoni nikakubali lakini moyoni nilikuwa mbali sana, kifupi siku hiyo hiyo ndio siku ambayo tulifungua ukurasa wa penzi letu na tukawa kama kumbikumbi kila wakati tuko wote huku nikiwa sijui chochote kuhusu alikotoka na kwa wazazi wa huyu mwenzangu.

Ndani ya kipindi cha uhusiano wote mwenzangu akapata ujauzito ambao kila mmoja aliufurahia sana huku mapenzi yetu yakiongezeka maradufu.

Sasa kilichonifanya kuja hapa kwenu wanajamvi wenzangu ni kwamba licha ya kumhudumia kwa kila kitu kama mwenza wangu lakini baada ya kujifungua binti akanambia alichokuwa anakitaka ameshakipata hivyo nisimjue na nisimfuatilie tena.

Mwanzo niliona ni kama utani lakini baada ya siku chache akatoroka na mtoto mimi nikiwa kazini na hata niliporudi na kuwauliza majirani hawakuwa na jibu la maana.

Na hata namba zake za simu kila nikipiga hazipatikani tena lakini kuna siku nilitumiwa sms kwa namba ngeni akinipa hongera ya kumpatia mtoto.Lakini nilipoipiga haikupatikana na mpaka leo haipatikani.

Ombi langu kwenu wanajamvi wenzangu nifanyeje niweze kuipata damu yangu? Imefikia kipindi nahitaji kumuona mwanangu lakini sijui wapi nitampata huyu mwanamke.

Msaada wanajamvi wenzangu
 
Japo inauma,jitahidi kuvumilia.
Achana naye utapata mwingine,kama siyo jini basi ipo siku mwanao atakutafuta
 
uliwahi kufahamu kwao?,uliwahi mfahamu ndugu yake?,aliwahi kukuonesh hata rafiki yake?,kama sio basi:
1.Unatudanganya
2.umezaa na jini

Alinitambulisha Kwa Mama Mmoja Anafanya Kazi Pale Ardhi Lakini Nilipomfuata Baada Ya Kutokea Hili Tatizo Nikaambiwa Kaenda Nje Ya Nchi Kimasomo Kwahiyo Nilikwama
 
mkuu Mbona Unanitisha!?

Sio nakutisha kaka, hebu cheki kwanza tu madhingira uliyoishi nae. hivi uliwezaje kuishi nae kipindi hicho chote bila kujua hata chimbuko lake?. hivyo wakati unajiuliza swali hilo hapo ndipo utakopo kubali ukweli kwamba. huyo ni JINI Ambae alitumia uwezo wake kukufanya usahau kuhoji jambo la msingi kama hilo.
 
Alinitambulisha Kwa Mama Mmoja Anafanya Kazi Pale Ardhi Lakini Nilipomfuata Baada Ya Kutokea Hili Tatizo Nikaambiwa Kaenda Nje Ya Nchi Kimasomo Kwahiyo Nilikwama
pata mawasiliano ya huyo mama,umuulize,baada ya hapo utajua pa kuanzia,pia karipoti Polisi,watatress alipokupigia simu alikuwa wapi,namba gani aliazipigia,...lakini toa taarifa ,pia ujiandae maana Polisi watajua una shida lazima wakuombe pesa ya ``chai``
 
Sio nakutisha kaka, hebu cheki kwanza tu madhingira uliyoishi nae. hivi uliwezaje kuishi nae kipindi hicho chote bila kujua hata chimbuko lake?. hivyo wakati unajiuliza swali hilo hapo ndipo utakopo kubali ukweli kwamba. huyo ni JINI Ambae alitumia uwezo wake kukufanya usahau kuhoji jambo la msingi kama hilo.

Naanza Kukubaliana Na Ww Lakini Alishawahi Kunikutanisha na Mama Mmoja Pale Wizara Ya Ardhi Lakini Nilipomfuata BaadaE Nikaambiwa Yupo Masomoni
 
pata mawasiliano ya huyo mama,umuulize,baada ya hapo utajua pa kuanzia,pia karipoti Polisi,watatress alipokupigia simu alikuwa wapi,namba gani aliazipigia,...lakini toa taarifa ,pia ujiandae maana Polisi watajua una shida lazima wakuombe pesa ya ``chai``

Naona Umenifumbua Mkuu Hii Kazi Nitaianza Kesho na Jibu Ntakalopewa nitakupm Mkuu
 
Mkuu Kinachoniuma Nimejaribu Sana Kutafuta Mtoto lakini Bado Sijafanikiwa

Umejuaje kama binti alikuzalia wewe? Kama alikuwa anatafuta mtoto inawezekana haukuwa peke yako...

Stuka!!!
 
Back
Top Bottom