Mwanamke niliyetegemea kumuoa nimekuta picha zake group la Telegram

Wakuu habari za Jumatano! Naamini mapambano yanaendelea kama ilivyo ada.

Moja kwa moja pasipo kuwachosha, niliwaahidi nitaleta mrejesho nitakapokutana na kuzungumza na Binti baada ya kuwa amerejea kutoka Dar kufata mzigoπŸ˜’πŸ˜’

Sikuwa nimewasiliana nae tena tangu mara ya mwisho nilipoblock namba zake. Sasa jana asubuhi nilipokea simu toka namba ngeni alikuwa ni yeye kaamua kusajili namba mpya Ili anipate akanitaarifu kuwa ndio kaanza safari ya kurudi kutoka daslam, nikasema sawa.

Majira ya saa sita alikuwa ameshafika, akaniuliza wapi nilipo aje, nikamwambia nipo home. Japo nilitamani tukutane sehemu nyingine tofauti na kwangu lakini nilipofikiria juu ya Hali ya maongezi itakavyokuwa ikabidi nimruhusu tu aje. Haikuchukua muda mrefu akawa amefika. Baada ya salamu akaanza kuomba radhi kwa tukio lile, nikamuuliza lengo lake kufanya vile ni nini hasa, eti anasema ni shetani tu. Nikamwambia unadhani hata nikikusamehe nitaweza kusahau maumivu ya ulichokifanya? Akasema ananipenda na hatamani tulichopanga kiishie pale, atajirekebisha na kuwa mwanamke mwema, ameteleza pia kama mwanadamu.. akainuka na kunisogelea kabisa akijaribu kunipapasa huku akiniomba nimsamehe nikajua hapa nikikaa vibaya ntaanza kumuomba msamaha MimiπŸ˜‚πŸ˜‚. Nikakaza kiume nikamwambia, kubadili uamuzi sio makosa kwa hiyo nimekusamehe ila kuhusu tulichokipanga sahau! Nenda ukaendelee na maisha mengine.

Vilio vikaanza nikamwambia hata ukilia haitosaidia, heri tumeachana kwa amani tofauti na kupigana au kurushiana matusi.. muda huo roho inaniuma sana maana Binti nampenda kupita maelezo ila tukio alilofanya limezuia moyo wangu kurudi nyuma, ntaumia muda ila nitazoea.. Binti kalia huku akinikumbusha mema na mazuri tuliyofanya na ahadi nyingi tulizopanga pamoja nikaona huyu ananichoma sasa, nikamwambia kwa kufoka, TOKA BANA!! Akainuka huku anasema "sawa naondoka ila najua aliyekwambia, tambua nakupenda sana". Nikampuuza akatoka, aisee nililia kwa uchungu sana baada ya kubaki mwenyewe, niliumia sana nikiwaza tulipotoka hadi hapo ilivyokuwa, Binti ni mzuri ila ndio mwisho tena..

Mida ya saa moja jioni nikiwa naandaa msosi kiaina akawa amekuja yule rafiki yake ambae mwanzo niliwaambia alipiga simu sikupokea siku Ile msala huu umenikuta. Nikamkaribisha fresh tu na kujuliana Hali. Baada ya hapo kaanza kuniambia yule mwanamke wangu alienda anapokaa yeye na kamtukana sana hadi kuapa kuvunja urafiki nae kisa amevunja mahusiano yake na Mimi na sababu kuu ikiwa ni kuniambia kuhusu tabia zake za kujiuza kisiri Siri. Nikamuuliza kivipi? Akasema kwa ambavyo yule mwanadada wangu alivyoenda kishari ni kama alijua yeye ndio alinitonya kuhusu Ile ishu..

Akili ikanicheza haraka kuwa Ina maana huyu siku zote anajua kuhusu tabia za Binti na hakuwahi kuniambia? Nikamuuliza nikiwa serious kama anajua kuhusu hizo tabia za Binti? Akaanza kujikanyaga kanyaga mara ooh najua ila sikukwambia kama ipo hivyo maana Binti yupo serious na amedhamiria kwa dhati kuwa na Mimi hivyo hakutaka kuniambia Ili nisije nikamuacha sababu ananipenda na mara kadhaa amekuwa akimwambia kuhusu kunipenda. Nikaona huyu nae ni walewale,, kuniita shemeji ni upumbavu tu, kwa hiyo unaona naingia shimoni hata kunisanua hakuna ,unaendelea kunikoleza tu niongeze speed? Nikajua huyu ni malaya mwenzake tu, nikamwambia sawa, unaweza kwenda. Kaanza kujivuta eti niazime sijui flash, nikamwambia sina, USO ukiwa serious akawa kajiongeza akaondoka..

Yule Binti kumbe tena alienda akapiga simu kwa mama yangu mdogo ambae mara kadhaa tuliwahi kwenda kumtembelea na kujuzana kuhusu yeye, kamwambia nimemsusia hivyo ajaribu kuongea na Mimi mambo yawe sawa japo hakumwambia sababu ni nini. Mamdogo amenipigia simu kaniuliza ila nikamwambia basi tu, nahisi simhitaji tena, muda tulioandikiwa kudumu utakuwa umetamatika..

Kukitokea Cha zaidi nitawajuza..πŸ™
 
Muite huyo shemeji wako geto uumle kupunguza hasira.
 
Huyo rafiki yake ungemgonga
 

Sasa hapo si ungemla shemeji??😳

#YNWA
 
Maamuzi ya kiume umefanya, usiendekeze hsia
 
Maamuzi ya kiume umefanya, usiendekeze hsia
Natambua mkuu, ila haikuwa rahisi. For every action there is an equal and opposite reaction.. jinsi nilivyokuwa nampenda ndivyo maumivu ya kumkisa yalirudi kwa nguvu hiyo hiyo
 
Natambua mkuu, ila haikuwa rahisi. For every action there is an equal and opposite reaction.. jinsi nilivyokuwa nampenda ndivyo maumivu ya kumkisa yalirudi kwa nguvu hiyo hiyo
Piga moyo konde utakua sawa ni maumivu ya mda tu
 
UShawahi kumkagua na ile sabufa a.k.a spika?
Maana yaeza kua we unapewa fronti door af masela wa telegram wanapita uani tena wengi kama wazamiaji wa chakula ya harusi uswazi
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hii kitu unafanana na series moja ya kinaijeria inaitwa "hey you".

Kaitazame utapata jbu nn ufanye

Mwamba ile movie ni kali
Yule manzi anajua kucheza na nyakati halafu pesa haikufanyie upendwe si mwishoni yule mwamba wa pesa alikimbia manzi akarudi kwa mshkaji wa IT yule domo zege aliekua anampigisha nyeto usiku
 
Mzee ungemkula Cha mwisho mwisho shemeji na hasira ingine ungemalizia kwa rafikie
 
Walimwengu wana mazigizaga sana! πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ™ŒπŸΎ
 
Mwamba ile movie ni kali
Yule manzi anajua kucheza na nyakati halafu pesa haikufanyie upendwe si mwishoni yule mwamba wa pesa alikimbia manzi akarudi kwa mshkaji wa IT yule domo zege aliekua anampigisha nyeto usiku
Sema wanaijeria wanajtahd asee Kuna nyngne inaitwa far from home nayo ni Kali Ina episodes Tano tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…