sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
PAKA JIKE HAWEZI KUKUZA SIMBA DUME
Mwanamke pekee hawezi kumkuza mtoto wake wa kiume kwenye kizazi hiki kipya, hii haijalishi mwanamke kaelimik kiasi gani, cheo, pesa, n.k. itakuwa ni ngumu sana, ponea ya mtoto labda awe na wajomba, ndugu wa kiume, n.k wenye muda nae, pia watoto wengine wanabahatika kuwa na watu wa mitaani sahihi ambao hugeuka kuwa kama baba kimtindo, lakini bado nafasi ya baba ni nzito.
Baba ni muhimu sana katika malezi ya mtoto wa kiume, uwepo wake pekee ndani ya nyumba hauna uzito, baba inabidi awe na jukumu la kukuza watoto wa kiume waje wanaume na sio watu wa kiume.
DISCIPLINE:
Mtoto wa kiume humuona mama yake kama rafiki yake tu ambae hata wakikosana anajua kuna madhara kidogo sana, atafinywa finya labda au atakaripiwa tu, binafsi mama yangu hata anichape nilikuwa namatania "hakijaingia", rafiki yangu flani akianza kuchapwa alikuwa anavunja vunja kiboko.
kwa baba ni tofauti kabisa, mtoto akikosea halafu aambiwe amsubiri baba yake wamalizane anajua tayari mziki wake, sio lazima kipigo kama wengi wanavyodhani lakini hata baba akikaa na mtoto wake kumpa darasa huwa kuna kitu kizito sana kinachomfanya mtoto ajihisi kweli kakosea na atajisikia vibaya, kiukweli huwa yanakuwa ni maumivu.
binafsi baba alikuwa ananipa dozi ya viboko mara chache sana na hapo ni kwamba nimekuwa mtukutu sana, lakini yale maneno aliyokuwa akinihusia kwenye makosa niliyofanya yalikuwa mazito sana, kuna muda niliwahi kulala saa tisa usiku nawaza tu darasa chungu alilonipa bila hata kuinua kiboko.... hii hali inamwingizia sana displini mtoto kujua kutii sheria hata za mama yake.
KUKABILIANA NA MAISHA YA WANAUME
Hapa utake usitake maisha ya wanaume utakutana na wanaume wenzako wakorofi ama waonezi, baba atamfundisha mtoto jinsi ya ku deal na hizi hali aidha kujua kupigana, kuwa na marafiki wa kum back up, n.k. mama yake atakuwa anaenda kulalamika mtoto kapigwa ila mzee wake anamuonesha mbinu.
ELIMU YA KUJITEGEMEA
Baba anaweza kuwa mfugaji, mkulima, seremala, fundi ujenzi, fundi mabommba, n.k hapa anaweza kumfundisha mtoto wake haya mambo ili hata akiondoka kuwe na mtu wa kuweka ugali mezani kihalali, mtoto akikosa hizi mbinu kuna uwezekano mkubwa akaanza kukaba watu.
MASULINITY (TABIA ZA KIUME)
Uwepo wa baba pia unamfanya mtoto wa kiume aweze kukopi tabia kibao za kiume, mzee anaweza kuwa mpenzi wa kutazama kwenye tv mieleka na muvi za ngumi, hapa mtoto nae anajijenga taia za ujasiri, kupenda mazoezi , n.k. hata pale mtoto anapoona mzee ana upinde ama rungu chumbani kwake hii inamfanya ajue mapema kwamba baba ndie mlinzi wa familia,
mtoto akikaa sana na mama yake si ajabu anaweza kuanza kupenda taarab, kujipiga make up, n.k,
INAENDELEA.............