Mwanamke sio mtu wa kumuamini kabisa kwa asilimia mia. Naombeni ushauri

Anaweza. Kuna watu wanaishi kwa mshahara wa 300k. Sembuse yeye 800k.
Vitu hivi ukiweza kuviepuka utaweza:
1. Wanawake(umalaya)
2. Pombe
3. Marafiki wa hovyo
4. Kuendekeza kusaidia ndugu marafiki
Wewe unaleta mzaha hapa kumbe? Mtu mwenye mshahara wa 1.2 anawezaje kutunza 400k katika nchi hii? Ajabu sana
 
Nenda Ustawi wa Jamii ili wakusaidie. Pia omba wewe na mtoto mpimwe DNA, kuthibitisha mtomto ni wako. Nasema hivyo, kwa sababu mwanamke anaweza kudai mtoto si wako.
 
Unazaaje na mwanamke kama hauna power mkuuu 😒 duuuh hapo sijui aseee
 
Mm na yeye tushaachana, shida mm nataka kuwa karibu na mwanangu, Sina shida na yeye nataka mwanangu niwe karibu nae, Ili niishi nae maana mtoto now ana miaka 6 inaenda
Mtoto sio wako huyo
 
Mimi sijalia naomba ushauli nijue jinsi gani ya kuweza kuwa karibu na mwanangu wa kike. Labda niende maakamani au nifanye hivi ilimradi nisivunje sheria
Una sound kama bado unampenda huyu mwanamke!!, ila mwanaume kulilia hivi sio poa!!
 
UPDATE: MUENDELEZO WA KISA HICHI

31/7/2023:

Habari jf: Mda mrefu umepita, miezi kadhaa imepita. Leo Ex Wife kanipigia simu ananiambia nikafate mtoto, maana alianza na gia kuwa anaumwa yupo hospital karazwa. Anashida na pesa nimtumie 500k, nmemtumia baadae ananiambia kuwa niende nikamfate mwanangu ili nimlee maana katoka kujifungua.

Maana ilikuwa asubuhi, now nipo na mtoto wangu wa kwanza wa kike nme enjoy sana. Nmefurahi sana maana niliamua kuwa nimuache ata kama akibadilisha jina bado atabaki kuwa mwanangu. Nimejifunza kitu katika maisha usinganganie kitu katika maisha kama kitu chako tu utakipata tu ata kama kitachukuwa mda kama ulipangiwa kukipata utapata tu.

Ila ananiomba sana msamaha nmsamehe na ananisisitiza nmpende sana mwanangu, yani kama vile ana hope na maisha yake hivi au ana tumaini la kesho, mm nmemwambia nmekusamehe ila mimi nipo na maisha yangu na yeye awe na maisha yake.

Nmemuonea huruma maana nilimpenda sana ila ndo hivyo aikuwa riziki au bahati ya kuwa nae pamoja. Kila kitu kinapangwa na lazima kitimie, kitu muhimu wacha niangalie maisha yangu na ya familia yangu.

Leo 31/7/2023 imekuwa siku yangu ya furaha na amani, ya kuwa karibu na mwanangu. Uvumilivu ni muhimu sna katika maisha.

SHUKRANI:
Kwa watu wote walio toa ushauri kipindi nipo katika matatizo, nashukuru sana na mungu awajali na kukutimizieni maitaji yenu katika maisha na familia zenu.

JAMII FORUM: PONGEZI ZOTE ZIENDE KWA WAUSIKA NA TEAM YOTE KWA KUWA NA PLATFORM NZURI HII YA JF,
 
Una sound kama bado unampenda huyu mwanamke!!, ila mwanaume kulilia hivi sio poa!!
Yah kwa sababu alikuwa mzazi mwenzangu. Siwezi kumchukia kisa kanikosea, mm nmemsamehe na sina kinyongo nae
 
""Anashida na pesa nimtumie 500k, nmemtumia... ""

Sorry kusema hili ila we jamaa una utoto mwingi.

Mnahela za kuchezea sanaaaa.

#YNWA
 
Dah!! Pole sana mkuu ila ilo mbona swala dogo sana wewe ndiyo unafanya liwekubwa sababu bado unampenda na yeye anajua unampenda ndiyo maana unaumia

Fanya hivi jichanganye na washikaji, kula msosi safi na vimazoezi kimtindo alafu tafuta pisi ambayo haina mambo mengi maana wachumba wapo wa kutosha achana nae uyo mshamba abebeki dah!! sema wewe unamoyo mm huwa sirembi mapeme sana angesepa

Kuhusu dogo usiwaze Je kama sio wakwako? piga chini angalia maisha yako
hawa viumbe sio
 

Kama haya ni kweli, wewe ni Juha.
 
Mm na yeye tushaachana, shida mm nataka kuwa karibu na mwanangu, Sina shida na yeye nataka mwanangu niwe karibu nae, Ili niishi nae maana mtoto now ana miaka 6 inaenda
Nenda Mahakamani kafungue kesi km unatoa matunzo ni haki yako kumuona au hata kuishi nae kipindi Cha likizo
 
Una uhakika uyo mtoto ni wako?
 
Mazuzu bado mpoooo. Dem kashasema muachane ww unalilia kukaa nae πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ wajinga ndio waliwao
 
""Anashida na pesa nimtumie 500k, nmemtumia... ""

Sorry kusema hili ila we jamaa una utoto mwingi.

Mnahela za kuchezea sanaaaa.

#YNWA
Na mimi nilitaka kuandika kitu kama hiki, jamaa bado ni mtoto sana au ana mapenzi ya tamthiliya hivi na demu ashajua pa kumuwini Mtoto kashapata na kama ataendelea kuwasiliana na x wake na kumtumia maokoto huu uzi utakuwa na update nyingi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…