Kiukweli walishafika mbali sana, mwaka wa 2 wako pamoja huu! Na kwa mipango ni mingi tayari washafanya ya kujijenga ila ndio hivyo, mwanamke anaweza vunja uaminifu uliojengwa kwa miaka kwa sekunde chache tu na kukosa kufikiri sawa sawa, mwanamke alirudi jana jioni na kuomba msamaha kwa majuto sana kisha akamwambia jamaa kwamba anajua kamkosea pakubwa hastahili msamaha anaona hana nafasi tena kabisa, ikibidi amove on tu na maisha yake, hatoweza kushuhudia jinsi jamaa anavyokosa raha katika uhusiano wao. Jamaa hajamjibu lolote, kakausha tu! Ila nahisi atamfix pahala tu. Akili za wahuni tunazijua wahuni!