Mwanamke Usiingie kwenye ndoa kama una hivi vitu

Mwanamke Usiingie kwenye ndoa kama una hivi vitu

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Ndoa ni safari takatifu, lakini kama ilivyo safari nyingine zozote, inahitaji kuwa tayari kabla ya kuianza. Si kila mtu anafaa kuwa mwenzi wa ndoa, na si kila mtu anafaa kuingia kwenye taasisi hii ya takatifu. Kama mwanamke unajiona katika hali zifuatazo, pengine unapaswa kufikiria tena kabla ya kuingia kwenye ndoa.
images (65).jpeg

1. Kukosa Uwezo wa Kujishusha.

Mwanamke ambaye hawezi kujishusha kwa mumewe, hafai kuolewa. Kujishusha si udhaifu, bali ni ishara ya heshima, upendo, na kujitoa katika uhusiano. Mwanamke anayeona kuwa yeye ndiye mkuu katika ndoa, anakuwa chanzo cha migogoro isiyo ya lazima. Mkipata watoto wa kiume basi fahamu unakwenda kutengeneza bomu kubwa sana la Simps (wanaume dhaifu) kwa sababu wameshaona baba yao akiwa dhaifu chini yako.
images (64).jpeg

2. Tamaa ya Mali na Pesa.


Kama lengo lako kuu la kuolewa ni kupata mali na pesa, basi wazo la ndoa kichwani kwako, ndoa sio chanzo cha kujipatia pesa wala mali. Ndoa inapaswa kujengwa juu ya upendo, heshima, na uelewano, siyo mali na pesa. Mwanamke anayeingia kwenye ndoa akiwa na nia ya kunufaika kifedha au mali, unakuwa ameipotosha kabisa dhamira ya ndoa, na ndoa sio kwa ajili yako.
images (63).jpeg

3. Kushindwa Kutoa Muda wako.

Ndoa inahitaji muda, bidii, na kujitolea. Mwanamke ambaye hawezi kutenga muda wake kwa ajili ya mumewe na familia yake, hafai kuolewa. Ndoa siyo mchezo wa kubahatisha, ni kazi ya kila siku ambayo inahitaji umakini na kujitolea.

images (61).jpeg
Mwanamke ambaye upo tayari kwenda kwenye shughuli za marafiki zako mpaka usiku wa manane nakusihi usiingie kwenye ndoa, utaishia kupata aibu pekee, huwezi kuwa mke wa mtu na kwenda kwenye shughuli mpaka usiku wa manane.

4. Kushindwa Kuheshimu Viapo vya Ndoa.

Kumekuwa na video zinazoonesha wanawake wakifanya mzaha na viapo vya ndoa, Mwanamke ambaye hawezi kuheshimu viapo vya ndoa, hafai kuolewa. Viapo vya ndoa ni takatifu, ni kiapo kinachowafungamanisha na Mungu.
images (63).jpeg

Kuvunja viapo hivi ni dhambi kubwa. Mwanamke anayeingia kwenye ndoa akiwa tayari amepanga kuvunja viapo, au kufikiria talaka anakuwa amemdhuru mumewe na ndoa yao mbele ya Mungu.

5. Kutegemea Sana Ushauri wa Marafiki.


Mwanamke ambaye bado anategemea sana ushauri wa marafiki zake katika maisha ya ndoa, hafai kuolewa. Ndoa ni uhusiano wa wawili, na uamuzi wa ndoa unapaswa kufanywa na wenzi wawili, siyo na marafiki.
images (65).jpeg

Mwanamke anayeendelea kutegemea sana maoni ya wengine, anakuwa amepoteza uhuru wake wa kufikiri na kufanya maamuzi. Achana na ndoa kabsa kama marafiki zako ndo wanashika dira ya maisha yako.

6. Kusimama Kuwasiliana na Wapenzi wa Zamani

Mwanamke ambaye bado anawasiliana na wapenzi wake wa zamani, hafai kuolewa, bonge la red flag hilo. Kuendelea kuwasiliana na wapenzi wa zamani ni ishara ya kutokuwa mwaminifu na kutoheshimu ndoa yako. Mwanamke anayeendelea kuwasiliana na wapenzi wa zamani, anakuwa ameweka ndoa yake katika hatari kubwa.
images (62).jpeg

Kilichomkuta Stamina ndo kitu ambacho wanaume wanaochukulia jambo hili kiwepesi wanaumia. Mwanamke fahamu nani ana umuhimu kwako, mume wako mtarajiwa au wapenzi wako wa zamani.

7. Kushindwa kutoa huduma ya faragha.

Ukiachana na kuzaa na kupata watoto, ila lengo la msingi la huyo mwanaume kukubali kuwa wewe ni kukupa heshima na kukuondolea kadhia ya kuonekana maharage ya mbeya. Huduma ya faragha ni moja ya huduma anbayo wanawake wengi wake za watu wanafeli wenyewe kiasi kwamba mume wako anakuona ni mzazi mwenzake! Neno MZAZI MWENZA ni neno chungu sana, ni sawa na kuishi kama Dada na Kaka.
images (64).jpeg

Mke hauna muda wa kumfanya mumeo akuone wa tofauti, maandalizi dhaifu kiasi kwamba mume anazidi kuona kadhia kukutana na wewe kimwili. Kuna msemo mmoja ulikuwa maarufu kutoka kwa mawifi, "humo ndani hujaenda kula na kujaza choo" wakiwa na maana uzae watoto, lakini kubwa utumikie tendo lenyewe.

8. Body Count kubwa.

Kama mwanamke umepata nafasi ya kukutana na wanaume wengi maishani mwako na kushiriki nao ngono, kaa chini ujitazame vizuri. Body count kubwa sio sifa wala sio kitu cha kujivunia kwa mwanamke.

Wanasaikolojia wamekwisha kuelezea kuhusu Body count na madhara yake kwa mwanamke. Mia Khalifa anajua historia yake itamuandama mpaka kila kesho, hata aolewe na nani, ndani yake anajua kuwa dunia zima inamfahamu, hata akipita mitaa ya Liberty pale Mwanza, watu watajua kuwa Mia Khalifa ni huyu.
images (61).jpeg

Kwa kifupi, kabla ya kuingia kwenye ndoa, fikiria kwa makini kama uko tayari kwa majukumu na changamoto zake. Usiingie kwenye ndoa kwa sababu tu ya shinikizo la jamii, marafiki au tamaa ya mali. Ingia kwenye ndoa kwa sababu ya upendo, heshima, na utayari wa kujenga maisha ya pamoja. Kabla ya kufungua kinywa chako na kusema kiapo hicho ujue maana yake na athari zake.
images (62).jpeg


Harusi ni siku moja au wiki ila ndoa ujue unakwenda kuishi na mtoto wa mwanamke mwenzako maisha yako yote. Ndoa ya Kim ilichukua wiki moja ila alitumia mwezi mzima kutafuta gauni la kuvaa kwenye harusi yake. Jiulize je kama kungekuwa na nyongeza ya maneno "Ehh Mungu nife siku nitakapotoka nje ya ndoa" unadhani wangapi wangechukulia mzaha kiapo cha ndoa?

KIBAYA CHOCHOTE KINACHOENDELEA KWENYE HATUA YA UCHUMBA BASI KITAFANYIKA 10X MARADUFU MKIINGIA KWENYE NDOA!
 
Hiyo #8 kusanya leo wanawake 100 ahidi atakaesema hadharani exactly body count yake unamzawadia 3mill cash aseme let's say 12 njoo nikate kichwa.

Wengi huzunguka kwenye watatu au wawili ukionyesha huamini anakuuliza “hivi unaniona me malaya sana au”,hapo unajishusha kiutu uzima unafanya zamu yako unatembea.
 
Hiyo #8 kusanya leo wanawake 100 ahidi atakaesema hadharani exactly body count yake unamzawadia 3mill cash aseme let's say 12 njoo nikate kichwa.

Wengi huzunguka kwenye watatu au wawili ukionyesha huamini anakuuliza “hivi unaniona me malaya sana au”,hapo unajishusha kiutu uzima unafanya zamu yako unatembea.
Ni bikra tu ambae hatokudanganya kwenye hilo
 
Hiyo #8 kusanya leo wanawake 100 ahidi atakaesema hadharani exactly body count yake unamzawadia 3mill cash aseme let's say 12 njoo nikate kichwa.

Wengi huzunguka kwenye watatu au wawili ukionyesha huamini anakuuliza “hivi unaniona me malaya sana au”,hapo unajishusha kiutu uzima unafanya zamu yako unatembea.
Kilometre zimesoma sana
For sure sio tu sis ambao Bado Kuna watu wako kwenye ndoa na Bado body count zinasoma vibaya mno Yani ni ubaya ubwela 😂😂😂
 
Back
Top Bottom