Mwanamke wa uswahilini

Mwanamke wa uswahilini

1. Hawajui kuigiza wala kuendana na drama za world class life za tiktok, akipenda safari atakunywa na ukimuagizia chakula, hawavungi kukimaliza na kufunga, ukitaka kuona wanawake halisi, nenda uswazi 😁

2. Ni wanawake wavumilivu na wastahimilivu maana wao huamini katika ridhki ndio maana wanaolewa hata na mwanaume anaemiliki chumba kimoja.. Labda uwe mdhembe wa kutafuta ndio utaachwa

3. Wanajua kupika na wana haiba ya kike.. Watoto wa uswazi wanakuzwa kwa ajili ya ndoa kama fanikio na jukumu la kwanza hivyo, wengi huelewa mwanaume anahitaji nini zaidi, kwa maneno na vitendo

4. Hawana choyo na wana utu sanaaaa, yaani kwenye mambo kama msiba hakuna sehemu watu hufarijiwa kwa asilimia zote kama uswazi. Vitu kama sufuria, viti, wapishi na wahudumu sio kitu cha kusababisha stress sababu mashoga na majirani zake watamaliza kazi

5. Ni wanawake wapiganaji, ukisikia kina diamond, ommy dimpoz na wengine wakitoa shuhuda za mama zao kuwapigania, bhasi ujue ni waswazi. Wapo tayari kufanya lolote pale inapoonekana njia kwa familia na watoto wao, ukitaka zile total sacrifice for love, utaikuta kwa wanawake wa uswazi
Umeua, yaani nilikutana naye mmoja, alinipenda hadi kunipigania ila nyumbani hatulii nikamtimua, ila hadi leo ananifahamu haswaaa
 
Back
Top Bottom