Mwanamke wa uswahilini

Mwanamke wa uswahilini

Ngoja tuambiane tabia za wanawake wa uswahilini haya ni baadhi tu wengine mtaongezea kama yapo

1. Wanathamini kuvaa kuliko chakula
2. Hawajui bajeti, ukimpa laki ya matumizi ya kawaida anaenda tafuta mganga
3. Hawana siri kwenye mambo mazuri akinunua kitu atahakikisha kila mtu anajua, ndio maana wanaongoza kwa visherehe visivyo na tija
4. Hawawezi kukaa nyumba yenye geti na eneo lililotulia kwani wamezoea kushinda kwenye miji ya watu
5. Ukiwa na mahusiano ya mapenzi basi familia nzima itajua mama, bibi, shangazi nk
6. Wanapenda mikopo kausha damu, uku hawana biashara yoyote
7. Yupo radhi auze kitu chochote ili atoe mchango wa shughuli

Ongezea mengine kama yapo
Wanaloga bro, kama huna Imani utachukuliwa msukule mpaka ufilisike
 
1) Mwanamke kujipamba.
2) Bajeti si ufanye wewe mtafutaji, laki nayo umeiona pesa ya maana siku hizi?
3) Unataka siri si uhame Uswahilini, nyumba yenyewe wapangaji kibao.
4)Khaa, kwani nyumba ya geti hamna majirazni?
5) Hayo siyo Uswahilini, hukohuko kwenu. Uswahilini hatuna "mahusiano" ama unaoa ama unasepa.

Bila "waswahili" ungejuwa Kiswahili wewe? tupishe huko.

Halafu mtu kama huyo anasema "mimi msomi".

Punguani wahed.
Jibu linajitosheleza
 
Back
Top Bottom