Nilikuwa na mwanamke ambaye nilikuwa nampenda mnoo, naye akasema ananipenda sana, Tukiwa chuo mimi nilikuwa nina kipindi 6 hadi 10 na yeye alikuwa anaingia saa 10 hadi saa 2 nikawa namsubiri atoke kisha namsindikiza kwao kwa daladala. Siku moja akanambie we nenda tu nikasema sawa sasa kuna mshikaji wangu alinichelewesha muda natoka naona pisi yangu inaingia kwenye IST (Vigari visnichi) shwaaa, akaondoka, nikapotezea siku nyingine tupo kwenye daladala akapigiwa simu alipomaliza kuongea akanambia mi nashuka kituo cha mbele, nikwamuuliza amekuja kukufata tena? akanijibi ni rafiki tu. tukateremka wote, jamaa akaja nikamuuliza manzi yangu huyu ni nani yako akanijibu nin mpenzi wangu, dah! niliumia sanaa sikujibu kitu baada yake nikaondoka badaye akanitafuta akanambia alinitania tu.
Tukaendelea ila nilitamani siku ifike ajue kuwa IST sio kitu ya kudharau upendo wangu, Mwenyezi Mungu sio Athumani, saivi nina Magari matatu BMW M5, CROWN, na VANGUARD na huwa napita kumsalimia anapofanyia kazi kuonesha kuwa Wakati wa mungu ni sahihi zaidi. Ila mapenzi bhana, saivi nina Magari anapaparika mnoo.
Tujifunze kuheshimu watu, Maana hatujui nani atakuja kuwa mlango wa Mafanikio Yetu