Mwanamke wangu kacheza na mwanaume mwingine mbele yangu tena kwa kushikana kiuno

Mwanamke wangu kacheza na mwanaume mwingine mbele yangu tena kwa kushikana kiuno

anyway kanizidi miaka 7 huyo dem


Mnaposhauri msisahau huo msitari..naona wengi hamjauona
 
Unapompeleka bar kulewa hapo umeishamshusha hadhi au wewe ndio unapenda walevi
Ila huyo ni wa kupita tu wala asikupe pressure na kuumia
Tafuta wa kuoa la sivyo utakuwa una share tu na wengi BAR
Hapo hujui kama alienda chooni na jamaa
 
Aiseee mwanamke unaweza kukaa bar na mpenzi wako huku ukiwa na wadogo zako wa kike umepigwa wimbo unanyanyuka unamuacha mpenzi wako kakaaa, mnaanza kucheza mziki na mdogo wako then anatokea mwanaume mnaanza kucheza, inafikia hatua kwenye uchezaji mnaanza kushikana viuno mbele ya mpenzi wako, eeety kwamba shemeji yake kwa mdogo wake mwingine.

Mim ndio kilichonitokea jana nikakasirika nikanuna mno, nikaamua niondoke ile naingia kwenye gari mdogo wake akanifuata akanisihi sana niludi nikakae nae

Lakin mimi tayari nishakuwa na kinyongo ukizingatia mitungi niliyokunywa basi bana kukaa kwenye kiti na mdogo wake tukawa tunaendelea mara akaja, iseee nilikuwa nimejitegeza tuuh ashoboke

Nilimtukana matusi mengi mazito mazito mbele ya mdogo wake nikamfukuza sitaki kukaa nae kanuna kaondoka, basi nikakaa na ndugu yake mpaka baa inafungwa nayeye akaondoka.

Mimi nikampa lift mhudumu mmoja mpaka anapoishi [emoji39]...

Je, ndugu zangu kitendo kilichofanywa mbele yangu ingekuwa wewe ungefanya nini ?

Mimi kumtukana jeeeh nimekosea sana ?

Maana mpaka asubuh hii hasira imenijaa sana sitaki hata kumuona na ile sehemu najulikana sana nahisi kanitia aibu naonekana mjinga anyway kanizidi miaka 7 huyo dem

Tayari nimemaliza
Mhhh miaka 7..... Unabemendwa.... tembea na mdg ake

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom