TANZIA Mwanamuziki Hussein Jumbe afariki dunia

Mwanamuziki mkongwe Hussein Jumbe amefariki muda huu wakati akiendelea na matibabu katika Hospital ya Amana, Dar es Salaam.

ea771033-bc4d-4a1e-baf4-1aeb15700fd6.jpg

===========
Updates

Mwanamuziki maarufu wa dansi, Hussein Jumbe amefariki dunia.

Jumbe aliyeitwa Mzee wa Dodo na Mtumishi aliwahi kupitia bendi za Tabora Jazz, Mara Jazz, Urafiki Jazz, DDC Mliman Park ‘Sikinde’ na TOT Band, Juwata Jazz na Mikumi Sound, amefariki leo Jumatatu Aprili 10, 2023 katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.

Habari ambazo Mwananchi zimetufikia hivi punde, Jumbe alikuwa akisumbuliwa na kifua kwa muda mrefu. Mwanamuziki huyo mkongwe atakumbukwa kwa nyimbo nyingi alizozitunga baadhi zikiwa ni Nachechemea, Nani Kaiona Kesho, Isaya na Kiapo.

Msiba upo nyumbani kwa marehemu Twangoma Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
 
Msiba mkubwa kwa wanamuziki wa dansi. Mwanamuziki maarufu wa dansi, Hussein Jumbe amefariki dunia leo Jumatatu Aprili 10, 2023.

Jumbe aliyeitwa Mzee wa Dodo na Mtumishi aliwahi kupitia bendi za Tabora Jazz, Mara Jazz, Urafiki Jazz, DDC Mliman Park ‘Sikinde’ na TOT Band, Juwata Jazz na Mikumi Sound, amefariki leo Jumatatu Aprili 10, 2023 katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.

Habari ambazo gazeti la Mwananchi limezipata ni kuwa Jumbe alikuwa akisumbuliwa na kifua kwa muda mrefu. Mwanamuziki huyo mkongwe atakumbukwa kwa nyimbo nyingi alizozitunga baadhi zikiwa ni Nachechemea, Nani Kaiona Kesho, Isaya, Kiapo na Mapenzi ya Siri.

Msiba upo nyumbani kwa marehemu Twangoma Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.​

jumbe-pic.jpg

Ni huyu alikuwa shabiki sana wa wananchi Yanga? Rest in peace Jumbe.

Napenda kibao cha nachechemea.
 
Mwanamuziki mkongwe Hussein Jumbe amefariki muda huu wakati akiendelea na matibabu katika Hospital ya Amana, Dar es Salaam.

===========
Updates

Mwanamuziki maarufu wa dansi, Hussein Jumbe amefariki dunia.

Jumbe aliyeitwa Mzee wa Dodo na Mtumishi aliwahi kupitia bendi za Tabora Jazz, Mara Jazz, Urafiki Jazz, DDC Mliman Park ‘Sikinde’ na TOT Band, Juwata Jazz na Mikumi Sound, amefariki leo Jumatatu Aprili 10, 2023 katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.

Habari ambazo Mwananchi zimetufikia hivi punde, Jumbe alikuwa akisumbuliwa na kifua kwa muda mrefu. Mwanamuziki huyo mkongwe atakumbukwa kwa nyimbo nyingi alizozitunga baadhi zikiwa ni Nachechemea, Nani Kaiona Kesho, Isaya na Kiapo.

Msiba upo nyumbani kwa marehemu Twangoma Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Nyakati ngumu hazipiti ila watu wagumu hupita, pumzika kwa amani Hussein Jumbe...wasalimie akina TX, Maalim Gurumo na wengineo
 
Back
Top Bottom