TANZIA Mwanamuziki Hussein Jumbe afariki dunia

TANZIA Mwanamuziki Hussein Jumbe afariki dunia

Kwa huu wimbo natumaini alijiandaa na kifo.

R.I.P Hussein Jumbe
Alizushiwa kifo baada ya kuugua sana. Mwamba alipopona akaibuka na hili songi kuwahabarisha waliomtamkia mabaya kwamba bado tupoyupo sana....
 
Mwanamuziki mkongwe Hussein Jumbe amefariki muda huu wakati akiendelea na matibabu katika Hospital ya Amana, Dar es Salaam.


===========
Updates

Mwanamuziki maarufu wa dansi, Hussein Jumbe amefariki dunia.

Jumbe aliyeitwa Mzee wa Dodo na Mtumishi aliwahi kupitia bendi za Tabora Jazz, Mara Jazz, Urafiki Jazz, DDC Mliman Park ā€˜Sikinde’ na TOT Band, Juwata Jazz na Mikumi Sound, amefariki leo Jumatatu Aprili 10, 2023 katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.

Habari ambazo Mwananchi zimetufikia hivi punde, Jumbe alikuwa akisumbuliwa na kifua kwa muda mrefu. Mwanamuziki huyo mkongwe atakumbukwa kwa nyimbo nyingi alizozitunga baadhi zikiwa ni Nachechemea, Nani Kaiona Kesho, Isaya na Kiapo.

Msiba upo nyumbani kwa marehemu Twangoma Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
RIP Nachechemea

Namkumbuka aliimba nyimbo moja nzuri sana ya maombolezo ya Baba wa Taifa Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere
 
BInafsi hata mimi hii nyimbo imenikumbusha mbali sana chozi limetaka kunidondoka nimekumbuka utotoni sidhani kama ni suala la me au ke kwenye kuonesha hisia
Bora umenitetea kuna nyimbo ukisikiliza yaani unajikuta unakumbuka matukio mabaya uliwahi kuyapitia ama huzuni ulizopitia unajikuta unalia 🤦
 
Pumzika kwa amani Hussein Jumbe, napenda kibao chake cha mapenzi ya siri....pole sana kwa familia
 
Niliaanguka ukaninyanyuaa mpakanjiaašŸŽ¶
Sikuweza kusimamaa mimiišŸŽ¶
Hamkukata tamaašŸŽ¶šŸŽ¶ mkajaribuu tenaašŸŽ¶
Mungu akawajaaliašŸŽ¶ nikawashika begaaašŸŽ¶šŸŽ¶

Dah nyimbo zao ziliupendezesha sana wakati wa utoto wangu, japo wao hawajanufaika na sauti zao
 
"Nilianguka mkaninyanyuaa sikuweza kusimama mimi,
Hamkukata tamaa, nikajaribu teeena, Mungu akawajalia nikawashika bega...."

"Siri ya ninii, nini faida yake,
Siri ya ninii, nini hasara zake,
Siri ooh, siri ya mapenzii,
Mapenzi ya siriii, nalia lia"

Rest easy legend,
Umetuburudisha kwa sauti nzuri na mashairi mazuri.
 
Aliamba "Nachechemea" baada ya kusingiziwa kifo, tangu wakati ule mpaka hivi ni karibu miaka 20. Ameondoka kwa wakati wa Bwana. Amen
 
Back
Top Bottom