Mwanamuziki Juma KILAZA na asili ya neno KILAZA

Mwanamuziki Juma KILAZA na asili ya neno KILAZA

Sisi wakongwe tulikuwepo ukumbini wakati Juma Kilaza na Mwinshehe wakipambana
 
Kilaza, haina maana kuwa ni udhaifu. Neno kilaza linatokana na neno "Kulaza". Kulaza maana yake ni kumbembeleza aliyekosa usingizi hata apate usingizi .
Sifahamu kama jina hili kilaza, lilikuwa ni jina lake la ubini, au lilikuwa jina la kimuziki. Lakini haina maana kuwa Juma kilaza alishindwa na Mbaraka Mwishehe, kwenye mashindano ya kupiga solo guiter.
Mimi sijakaa Moro, Lakini nilikuwa shabiki wa muziki wa bendi zote mbili, (Moro Jazzo, na Cuban marimba band, ambiansy).
Juma kilaza hakuwa mpiga solo guiter, yeye ilikuwa ni composer, na mwimbaji (Lead singer, kama Mbaraka mwishehe. Tofauti kati yao ni kuwa Mbaraka alikuwa Composer, Lead vocal, na mpiga solo guiter.
Kwa muda nilipokuwa nikiangalia performance ya bendi hizo mbili, Kuna Kilaza alikuwa akiwalaza watu, kwa mziki safi wenye vina vilivyopangiliwa na pia alikuwa ni master wa kutawala jukwaa kwa uimbaji wake na sauti yake yenye mawimbi.
Kuwashindanisha Mbaraka na Juma Kilaza, si kwa upigaji wa guiter, bali kwa utunzi na uimbaji. Wote walikuwa waimbaji wazuri na watunzi pia.
Sikubaliani na wazo kuwa neno kilaza linatokana na mapungufu aliyokuwa nayo Juma Kilaza. Yawezekana Juma aliitwa kilaza kwa kuwaporomosha chini wapinzani wake kumuziki. 'Kalaga bahho'.
 
CHANZO CHA NENO KILAZA KAMA MTU MWENYE UWEZO MDOGO.

Neno hili lilianza kutumika miaka ya 1970 chanzo chake ni msanii nguli wa kipindi hicho aitwae Juma Kilaza ambaye alijiita yeye ndio gwiji wa kupiga gitaa la solo.

Lakini liliandaliwa pambano la kumpata mpiga gitaa mzuri Tanzania hivyo Pambano hilo lilimpambanisha Juma Kilaza alie kua katika bendi ya Cuban marimba na Mbaraka Mwinsheshe Mwaruka aliye kua katika bendi ya Morogoro Jazz Band.

Hivyo Mwinsheshe alimushinda Juma Kilaza hivyo Kilaza alionekana anauwezo mdogo
Tangu hapo mtu mwenye uwezo mdogo aliitwa Jina lake ambalo ni Kilaza.

Hicho ndio chanzo cha neno Kilaza.
FB_IMG_16357445305925141.jpg
FB_IMG_16357445420567014.jpg
 
Siku za hivi karibuni neno KILAZA limepata umaarufu na kutumika kwa kasi kubwa hapa nchini. Neno KILAZA limepata umaarufu baada ya Rais Magufuli kuwaita VILAZA wanafunzi 7802 (special diploma) waliofukuzwa chuo kikuu cha Dodoma na kuwataka wakatafute vyuo vya saizi yao ya UKILAZA.

Kama lilivyo neno la KIHIYO, nalo KILAZA lina historia yake. Juzi nimeskiliza Honi Sigara wa Baraza la Kiswahili Tanzania akifafanua kuhusu KILAZA, japokuwa alizunguka sana kulitolea ufafanuzi lakini kwa ufahamu wa kawaida alimaanisha ni ''Uwezo mdogo wa kufanya jambo''.

Sigara aliendelea kuelezea kuwa halina maana moja kwa moja na uwezo wa akili, akadai pia kuwa asili ya neno KILAZA ni kwenye Tasnia ya Muziki.

Nikafuatilia kwenye tasnia ya muziki na ndipo nikajua kwamba, hapo kale kwenye muziki wa Dansi kulikuwa na mwanamuziki maarufu aliyejulikana kwa Jina la Juma KILAZA, Mwanamuziki huyo alikuwa na tambo na majigambo kuwa yeye ni bora kuliko gwiji la muziki Mbaraka Mwinshehe na ana uwezo mkubwa wa kutumia vyombo vya muziki kuliko Mbaraka Mwinshehe.

Ili kuondoa doubt, liliandaliwa Pambano kati ya KILAZA na Mwinshehe lakini tofauti na tambo za KILAZA, Mwinshehe alamgaragaza vibaya sana mpinzani wake na KILAZA alionesha UWEZO MDOGO SANA.

Kuanzia hapo neno KILAZA likaanza kukua kwa kasi na kutumika kwa watu wanaoonesha uwezo mdogo wa kufanya jambo.

* Honi Sigara amesema kuwa hili sio neno RASMI la Kiswahili, lakini watalifanyia mchakato na Utafiti na kama wataona linafaa basi watalifanya kuwa neno rasmi.

Asanteni sana.
Mh!
 
Hili Shindano linalosemwa halikuwahi kuwepo popoye ktk Historia
 
Back
Top Bottom