Wee hapo ni siku yako ilikuwa haijafika, sio tena mambo ya gari ndogo or kubwa[emoji848]Ajali na kifo hutokea pasipo wewe kujua,2020 oct 28 nlipata ajali mbaya sana mbele ya shelui nligonga kundi la ngombe ucku walivuka mimi nkiwa speed ...ingekua gari ndogo sidhani kama ningetoka hai
Dah hapo anapomalizia huwa panaleta hisia za ajabu sana aisee...Sijawahi kuuchoka huu wimbo pia. Nausikiliza hata sasahivi.
Akimalizia ''Najua ni ngumu wazi mi kuelezea lakini ninabidi mpenzi kwangu kukwambia.....vile ninavyohisiii.''
Pumzika kwa amani Maunda Zorro. Pole kwa familia nzima ya Zorro.
Hahahaha..Kumbe mtoto kabisa sisi tumepigia picha ya yule malaya aliyemuosha miguu yesu
SawaHapana mimi si askari, mimi ni Civil Engineer. Ile gari ilienda kambini kwasababu mwenye site ndo ZONAL CONSTRUCTON MANAGER wa JKT.
Hiyo siku sitaihasau.
Ameshapumzika.. Tabu iko kwa aliowaachaApumzike kwa Amani Marehemu
Pole Sana Mzee Mwenzagu Zahir Ally Zorro,Mwanamuziki Maunda Zorro, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo (Alhamis ya April 14) baada ya gari alilokuwa amepanda aina ya VITZ kugongana uso kwa uso na lori la mchanga huko Kigamboni, Dar es Salaam.
Maunda Zorro ni mtoto wa muimbaji nguli wa muziki Zahir Ally Zorro pia ni mdogo wa mwanamuziki Banana Zorro.
Maunda Zorro aliwahi kutamba na vibao kama vile 'NATAKA NIWE WAKO' na 'MAPENZI NI YA WAWILI' ambavyo mpaka sasa vinapendwa na wapenzi wa muziki kwani ni aina ya muziki usiochuja.
Apumzike kwa Amani
=============================
Kaka wa marehemu ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Banana Zorro amesema:
"Nimezipata hizo taarifa ndio naelekea Hospitali ya Kigamboni, taarifa ni za kweli tulikuwepo kwenye msiba jioni ya leo wa rafiki yetu mwingine wa karibu, nilikuwa nae Maunda hadi jioni saa 11 hadi 12 nikarudi nyumbani kulala maana msiba ulikuwa Kigamboni na yeye anakaa Tuangoma.
"Chanzo cha kifo ni ajali ya gari, niliachana na Maunda saa 12 jioni ajali amepata mida ya saa 4 usiku, ila sina uhakika sana (wa muda aliopata ajali) hadi nikifika Hospitali maana nilirudi nyumbani nikiwa nimechoka sana."
=============================
MWILI WA MAUNDA KUZIKWA JUMAMOSI
Kaka wa marehemu Maunda Zorro, Banana Zorro ametoa ratiba rasmi ya MAZISHI ya dada yake Maunda Zorro.
Marehemu Maunda Zorro atazikwa siku ya Jumamosi Aprili 16, 2022 nyumbani kwake Twangoma Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
View attachment 2186717
View attachment 2186720
Acha kabisa. Ilisikitisha sana. Wote hivi sasa wako chini ya dongo la zaidi ya tani saba. Funza wanajinoma tu....
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]akiwemo dada yakoDaah bora wangekufa wanawake 50 wa JF kuliko huyu mrembo
Mm sina dada ambaye yupo JF, naomba uwe dada yangu.[emoji1787][emoji1787][emoji1787]akiwemo dada yako
R.I.P
Inawezekana alikuwa anaendesha amelewa maana huyu na bro wake wanakula pombe kinoma
Daaah hii ngoma inanikumbusha mbali sanaDah ngoma yake inayokwenda kwa jina "Nataka Niwe Wako" inazidi kuniliza , Inanikumbusha mbali sana sana . RIP Maunda Zorro.
Maunda Zorro - Nataka Niwe Wako
Source : Bongotrax
ShindwaMm sina dada ambaye yupo JF, naomba uwe dada yangu.