TANZIA Mwanamuziki Maunda Zorro afariki dunia kwa ajali ya gari, mazishi Jumamosi Aprili 16, 2022

TANZIA Mwanamuziki Maunda Zorro afariki dunia kwa ajali ya gari, mazishi Jumamosi Aprili 16, 2022

Ajali na kifo hutokea pasipo wewe kujua,2020 oct 28 nlipata ajali mbaya sana mbele ya shelui nligonga kundi la ngombe ucku walivuka mimi nkiwa speed ...ingekua gari ndogo sidhani kama ningetoka hai
Wee hapo ni siku yako ilikuwa haijafika, sio tena mambo ya gari ndogo or kubwa[emoji848]

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Sijawahi kuuchoka huu wimbo pia. Nausikiliza hata sasahivi.

Akimalizia ''Najua ni ngumu wazi mi kuelezea lakini ninabidi mpenzi kwangu kukwambia.....vile ninavyohisiii.''

Pumzika kwa amani Maunda Zorro. Pole kwa familia nzima ya Zorro.
Dah hapo anapomalizia huwa panaleta hisia za ajabu sana aisee...
Kwa miaka zaidi ya kumi nautumia huo wimbo kwenye simu yangu kama 'ringtone'.
Naupenda mno na nampenda sana Maunda.
Lala salama kipenzi.
 
Mwanamuziki Maunda Zorro, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo (Alhamis ya April 14) baada ya gari alilokuwa amepanda aina ya VITZ kugongana uso kwa uso na lori la mchanga huko Kigamboni, Dar es Salaam.

Maunda Zorro ni mtoto wa muimbaji nguli wa muziki Zahir Ally Zorro pia ni mdogo wa mwanamuziki Banana Zorro.

Maunda Zorro aliwahi kutamba na vibao kama vile 'NATAKA NIWE WAKO' na 'MAPENZI NI YA WAWILI' ambavyo mpaka sasa vinapendwa na wapenzi wa muziki kwani ni aina ya muziki usiochuja.

Apumzike kwa Amani

=============================
Kaka wa marehemu ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Banana Zorro amesema:

"Nimezipata hizo taarifa ndio naelekea Hospitali ya Kigamboni, taarifa ni za kweli tulikuwepo kwenye msiba jioni ya leo wa rafiki yetu mwingine wa karibu, nilikuwa nae Maunda hadi jioni saa 11 hadi 12 nikarudi nyumbani kulala maana msiba ulikuwa Kigamboni na yeye anakaa Tuangoma.

"Chanzo cha kifo ni ajali ya gari, niliachana na Maunda saa 12 jioni ajali amepata mida ya saa 4 usiku, ila sina uhakika sana (wa muda aliopata ajali) hadi nikifika Hospitali maana nilirudi nyumbani nikiwa nimechoka sana."

=============================

MWILI WA MAUNDA KUZIKWA JUMAMOSI

Kaka wa marehemu Maunda Zorro, Banana Zorro ametoa ratiba rasmi ya MAZISHI ya dada yake Maunda Zorro.
Marehemu Maunda Zorro atazikwa siku ya Jumamosi Aprili 16, 2022 nyumbani kwake Twangoma Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

View attachment 2186717
View attachment 2186720
Pole Sana Mzee Mwenzagu Zahir Ally Zorro,
Pole Sana Banana, wanafanikiwa, ndugu, jamaa, marafiki, mashabiki, wasanii na Watanzania Kwa ujumla.

RIP Maunda Zorro.
P
 
Rest in peace Maunda Zoro tutakukumbuka ulijua kuimba Mapenzi ni ya wawili na niwe wako ni ukumbusho uliotuachia.
 
Shangazi mzuri mzuri R .I.P🥰😍😘
UPazE.jpeg
 
Back
Top Bottom