TANZIA Mwanamuziki Maunda Zorro afariki dunia kwa ajali ya gari, mazishi Jumamosi Aprili 16, 2022

TANZIA Mwanamuziki Maunda Zorro afariki dunia kwa ajali ya gari, mazishi Jumamosi Aprili 16, 2022

Juzi tu kuna askari jamaa yetu tumetoka kuzika,gari lake liliogongoana na Lori LA mchanga.

Polisi iangalie uwezekano kudhibiti madereva wa malori ya mchanga-ni matatizo.
Hasa kule kigamboni lori zinakimbia sana na ile njia ya kongowe kuelekea kigamboni ni hatari sana malori yanaenda hovyo sana
 
Malori ya mchanga ni tatizo kubwa Sana ,pamoja na Yale ya kubeba mifugo ,
Hao wa mchanga kuanzia saa moja jioni hasa hasa kwenye hizi barabara za kuingia mitaani akikaa nyuma yako na ukajua ni gari ya mchanga au akiwa anakuja mbele yako mpishe mwache aende hawa jamaa huwa wanafanya vitu vya ajabu barabarani kama maroboti.

RIP kwa msanii wetu
 
akavune alichopanda kwa Mungu sio kwa Mzungu.

mpaka anakufa bado anaendekeza anasa za dunia tu
 
Mimi nimeleta taharifa na picha juu, angesema Sheikh Yahaya ungesadiki?
Usanii tu hata angekufa mtu mwingine angesema katabiri. Utabiri gani hauna hata maelezo ya kutosha wala timeframe ila neno tu tasnia ya burudani. Hata mimi naweza kusema naona umauti kwenye siasa.
Hata akifa mwenyekiti au mwanasiasa yoyote baada ya miezi nasema nlitabiri
 
Back
Top Bottom