Najivunia kulala na mkeo, nimevumilia sana na leo/
nimeamua kusema sijari kama utanikaba koromeo, utanivunja na kuniacha kimeo/
Kamwe sijutii katu, sijutii katu piga kelele jaza umati sihofii watu/
Nimekubuhu mpaka inafika hatua, nimefanya mtaa mzima unajua/
Na sifikirii ni rough...kwa mtindo zaidi ya saba, na maumbile nimejaliwa si haba/
Nilimpa raha kote kwenye gari na valanda, kama mfungwa aliyekutana na kahaba/
Ona mrume ndago bila kiwewe, kila ulipo safiri mi nilipiga misele/
Aliponiita niliitika kuzizima kelele, na nilipofika nilihakikisha anafika kilele/
Alinipeleka mbali kwa misemo moto moto hadithi njoo utamu kolea, ukihisi naongeza chumvi kwa maneno ya uongo ona alama ya meno kwenye mgongo halafu ngojea/
Ni hakika alinikumbuka kila mida, na aliponita niliibuka bila shida/
Alipopata swali aliniona mimi kwanza, akajiita jen nikajiita tarzan believe that/
Alifika na kukaza na kamba, aliweka mizizi ya kukata na panga/
Alichizika utasema mwehu, moyoni aliacha alama kama ronaldo alivyoacha alama bernabeau/
Nilikua siufahamu ugoni, aah kama kufumaniwa ni dhambi na nitapata adhabu motoni....nitaenda na tabasamu moyoni//
Labda wakati ni sasa nimerudi kuenzi nafasi, napenda uhakika silengi bahati/
Naomba ujue kua mkeo, mkeo hakupendi kwa dhati, kumlazimisha ni kumuenzi hayati/
Sasa kwanini usinipige na ulivyojifungia misuli, nivunje mbavu zangu labda utajiskia vizuri/
Fanya maamuzi sasa maana najitia kiburi, niue leo walimwengu watafukia kaburi/
Najiskia uchovu na miayo napiga, ulizia hizi nyayo na nyika/
Nimetoka mbali fanya maamuzi tuhitimishe kikao, maana mimi nina mishe kibao/
Mishe hata wewe unazo mishe unazo badili, fafanua eleza na uweke mifano isawili/
huo ubishi wakujikweza weka kando ukatili, leo ndio mwisho vina navunja ndoa yako batili/
Andika talaka ili tuondoke...maana maamuzi ni yako au chukua panga unichome/
Haukuitendea haki kura yako, kuchagua ndoa wakati sio jambo kubwa kwako....Utakapochukua wasaa utagundua ulimpa saa alipohitaji muda wako/
Anajua kua mkoa mbali unawatoto, anajua kuhusu vikao na safari za uongo/
anajua kuhusu kondomu ulizobana kwenye nguo, na meseji za wasichana wachuo/
Ulimkuta mwema ukamteka kiakili, ukamshawishi mpaka akakupa shehena ya mwili/
Akakupa moyo akihisi utaweka nadhiri, ukajisahau na ukamuonesha asili/ kwamba wewe ni mchafu tu
Kipi unaropoka lakini, ubaya ulipwa kwa ubaya unachokonda ni nini?
Mmoja ametupa na mwingine ameokota yamkini, aliyetupa ni wewe na niliyeokota ni mimi/
Ilikua nisababu ya msongo wa mawazo, na ndio maana uliona wife sio wamoto kama mwanzo/
Uliteseka kiasi ukahisi ndoa ni sumu, na nikachukua maamuzi magumu/
Dongo kwako nilimuokoa nikamvusha bahari, maana muungwana vitendo maneno hayata angusha jabari/
Siku mwili hautagusa sayari, utamkumbuka na utajifunza kujari/
Mpunga umeyumba umeanza kujishuku mzee, umerudi nyumbani baada ya kushindwa kumudu starehe/
Haukuwepo kwenye shida ilipofuzu tarehe, ulikimbia nilikuwepo mimi pekee/
Ngoja nikuudhi, unajua mwanao ananiita dady, nampeleka shule namrudisha nyumbani baada ya kazi?
Nalipa ada, ada usizoweza kutoa, mwanao amefikia balehe na nimemfunza kunyoa/
Nimemfunza ushairi,nimemfunza kufunga kamba za viatu, nimemfunza kufunga tai kisha kamba za viatu/
Nimemfunza kuhusu sheria zinaoongelewa bungeni, na nilienda kumtetea alipoonewa shuleni/
Una hoja yeyote devensively?, maana haujui kama wanalala ama wanaamka safely/
Hujui kuhusu family dinner,wemen days,bithdays zao hujui kuhusu anniversary/
Hujui maumivu aliyopata moyoni, hujui harufu ya chakula alichopasha jikoni/
Haujui kuhusu depression, maana mara mbili nimemkuta amejifunga kamba shingoni/
Nampenda yeye amenifanya nipate ishara, amenipa counselling amenifanya niache sigara/
Anajua chakula nikipendacho, timu niipendayo, kinywaji, anajua even my favorite color/
Wenzio tunatafuta familia ili tujenge, wewe yako ninini? Mkeo ameisaliti ndoa sababu yake ni upweke/...sababu yako ni nini?
You know what they say what goes around comes around men, yeah that's true so i wonder why you changed, you used to be a good man what happened to you?
Nakiri mbele za watu nilishiriki hii dhambi, uvungu wa moyo wangu unasema usaliti ni haki/
nyanyua kisu chako uniue ila naomba uelewe, sijaivunja ndoa yako umeivunja ndoa yako mwenyewe/
It's Scars