TANZIA Mwanamuziki Mkongwe, Boniface Kikumbi Mwanza Mpango (King Kikii) amefariki dunia

TANZIA Mwanamuziki Mkongwe, Boniface Kikumbi Mwanza Mpango (King Kikii) amefariki dunia

Kwema Wakuu?

Niko mahali hapa nasikia taarifa zisizo njema kuhusu huyu Mzee, zina ukweli wowote?
View attachment 3152544
=====

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini Boniface Kikumbi Mwanza Mpango maarufu King Kikii amefariki dunia.

Amefariki Dunia Usiku wa kuamkia leo katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili ambako alikuwa amelazwa.

Mwanamuziki King Kiki Alikuwa Kwa Muda Mrefu akisumbuliwa na Maradhi Mara Kwa Mara

Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa Jina Lake Lihimidiwe, Amen

Chanzo Cha Habari:TBC RADIO

Hapa chini ni baadhi ya kazi zake.

View attachment 3152971
View attachment 3152975

King Kikii

Kikumbi Mwanza Mpango, maarufu kwa jina la King Kiki au Bwana Mukubwa, aliingia nchini akitokea Zaire (DRC) mwanzoni mwa miaka ya 1970 akiwa na Orchestra Fouvette na tangu wakati huo amekuwa mkuzi, mwalimu na mlezi wa vipaji vingi vya muziki.

Kiki alizaliwa Januari 1, 1947, Lubumbashi, DRC.

King ni mtoto wa tano kwa Katambo Wabando Paulino na mama yake Mwanza Jumban,” anasema Kiki.

Akiwa shuleni, darasa la tano, Kiki na wenzake watatu walianzisha kikundi cha muziki wa dansi; wakiimba na kucheza kiasi cha kukubaliwa na uongozi wa shule na kualikwa katika kila sherehe shuleni kwao.

Sifa zao zikazagaa mitaani hasa kutokana na umri wao na ukubwa wa ‘kazi’ waliyokuwa wakiifanya.

Akiwa na umri wa miaka sita tu, Kiki alibahatika kuhudhuria onyesho la mkongwe wa muziki wa Afrika Kusini, Miriam Makeba, na kwa hakika mama huyu ndiye aliyemvutia kuupenda muziki.

Akiwa bado masomoni, mwaka 1958 alianzisha kikundi cha Bantu Negro kilichoubadili muziki wa Afrika Kusini kuwa muziki wa rhumba.

Aliachana na masomo mwaka 1962 na kujiunga na Norvella Jazz, bendi iliyomfikisha Kasai (Mbudji Mai) na kupaunua uzoefu wake kwa kukutana na wanamuziki mahiri kutoka Kinshasa.

Hata hivyo, wazazi wake hawakupenda awe mwanamuziki, hivyo kuwa kizingiti kikubwa katika safari yake ya sanaa.

Kiki na mwanamuziki mwingine maarufu nchini, Fred Ndala Kasheba, walikutana kwa mara ya kwanza huko Katanga, DRC mwaka 1968 katika bendi ya Orchestra Fouvette.

Ni bendi hiyo ndiyo iliyowaleta wakubwa hao nchini kwa mara ya kwanza miaka ya 1970 mwanzoni.

Kiki alihamia rasmi Tanzania mwaka 1977 baada ya kufuatwa na Chibangu Katayi ‘Mzee Paul’ na kujiunga na bendi ya Maquis du Zaire ya jijini Dar es Salaam.

Kutoka DRC, Kiki aliongozana na Nkashama Kanku Kelly, Mutombo Sozy na mpiga besi gitaa maarufu wa Maquis, Ilunga Banza ‘Mchafu’; bila kumsahau mnenguaji, Ngalula Tshiandanda.

Kiki ndiye muasisi wa mtindo maarufu wa Kamanyola ulioacha urithi wa jina la kituo kimojawapo cha daladala katika Barabara ya Shekilango, Sinza.

‘Kamanyola bila jasho’, kwamba unacheza kwa kujidai,”

Miongoni mwa vibao maarufu vilivyotungwa na King Kiki ni ‘Nimepigwa Ngwala’, ‘Kiongo’, ‘Kyembe’, ‘Sababu ya Nini’ na ‘Krisimasi Bonane’.

Wanamuziki alioshirikiana nao wakati huo ni akina Mbuya Makonga ‘Adios’, Mutombo Lufungula ‘Audax’, Mukumbule Lolembo ‘Parashi’, Kasongo Mpinda ‘Clyton’, Mbombo wa Mbomboka, Tshimanga Kalala Assosa, Kiniki Kieto, Masiya Radi ‘Dikuba Kuba’, Issa Nundu na Tabia Mwanjelwa.

Baadaye Kiki akajiunga na Orchestra Safari Sound (OSS) iliyokuwa na makao yake Kimara Resort na kukutana na akina Skassy Kasambula, Monga Stani Liki, Mobali Jumbe, Kalala Mbwembwe, Tshibanda Sony na Kabeya Badu.

Huko akaibuka na mtindo wa ‘Masantula Ngoma ya Mpwita’ na kushiriki kuimba na kutunga nyimbo kama ‘Mimi Msafiri’, ‘Mama Kabibi’ na nyingine nyingi, kabla ya kuanzisha bendi yake ya King Kiki Double O, iliyokuwa ikitumia mtindo wa ‘Embalasasa’.

Mwaka 1994 akaungana na Kasheba kuunda bendi ya Zaita Musica iliyopata umaarufu kwa wimbo wa ‘Kesi ya Kanga’ na ni hapo ndipo mtindo wa ‘Kitambaa Cheupe’ ulipozaliwa.

Mtindo huu uliipa umaarufu mkubwa bendi ya La Capitale (Wazee Sugu) aliyoiunda mwaka 2003, baada ya kifo cha Kasheba.

Mwaka 1997, Kiki alipata uraia wa Tanzania baada ya kuishi nchini kwa miaka mingi.

Bwana Mukubwa Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kiki’ ni baba wa watoto kadhaa, huku binti mmoja pekee ndiye aliyefuata nyayo zake.

Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa simu namba: 0784331200,
Jabali la mziki limeanguka, pumzika kwa amani Mfalme Kikii
 
King Kikii aliishi uzeeni kwa kutegemea perfomance za jukwaani na siyo mirabaha ya kazi zake alizowahi kufanya ambazo zinachezwa sana.....

Ndugu, haya mashirika COSOTA, BASATA, TBC ni majinamizi kwa wasanii
Hayo mashirika si yameanzishwa juzi juzi tu. Wala hamna haja ya kulaumu
 
Mwanae wa kike ndiye mmiliki
Alihojiwa TBC akasema zile Bar hazimuhusu yeye na Familia yake hata kutumika Jina la Kitambaa Cheupe kwenye zile Bar yeye hanufaiki na chochote, mwisho wa kunukuu

Kwa hio sio za mtoto wake
 
RIP Legend.

"Kitoto Kaanza Tambaa" ni wimbo ninaoupenda sana.

Ni wimbo unaozungumzia mtu anayeifikiria familia yake, anayefikiria mtoto mdogo anayeanza kutambaa maisha yake yatakuwaje, mtu anayefungua njia kitoto kaanza tambaa, mtu anayefikiria familia yake italelewa vipi, mtu wa kujali familia.

"Watoto wa kwangu, nani atawaleaa?
Familia ya kwangu, nani atawaleaa?
Mzigo wa kwangu, nani atauleaa?
Twende, fungua njia, kitoto kaanza tambaa"

Maudhui kama haya yanatoweka kwenye nyimbo nyingi za siku hizi.

View: https://youtu.be/0L0PseRXvmg?si=sJZqLplB6ZnClUcE

Hawa watu walikuwa wanaimba nyimbo kuhusu maisha, ndio maana hata bongo fleva ilipokuja mwanzoni nayo ilikuwa na maudhui sana. Kulikuweko na party songs ila na story telling songs kuhusu maisha. Nyimbo za aina hii ni ngumu sana kuchuja.
 
Huenda 90% ya matibabu yake yaligharamiwa na mapato ya baa za kitambaa cheupe. Bintiye ndiye mkurugenzi wa zile Bar.
Mboni Mzee alikataa alipohojiwa na TBC au alikua anatuigizia? Alisema zile Bar hazimuhusu yeye na Familia yake yaan hawanufaiki kwa chochote kutokana na zile za Kitambaa Cheupe yaan haziwahusu, nyinyi haya mnayoyasema mmeyatoa wapi?
 
Alihojiwa TBC akasema zile Bar hazimuhusu yeye na Familia yake hata kutumika Jina la Kitambaa Cheupe kwenye zile Bar yeye hanufaiki na chochote, mwisho wa kunukuu

Kwa hio sio za mtoto wake
Yupo sahihi ila haliondoi ukweli kwamba biashara ni ya mtoto wake. Hakuna asiyejua kuwa mtoto wa kike ndiye humtunza baba yake uzeeni.
 
Yupo sahihi ila haliondoi ukweli kwamba biashara ni ya mtoto wake. Hakuna asiyejua kuwa mtoto wa kike ndiye humtunza baba yake uzeeni.
Sikia mkuu alihojiwa na TBC akiwa amelala kitandani walimfuata nyumbani kwake, wakamuuliza hilo swali zile Bar zinakuhusu wewe mboni zinatumia Jina la Wimbo wako? Mzee akasema zile Bar hazinihusu wala Familia yangu haihusiki na zile Bar na hakuna chochote tunachopata kutokana na kutumika Jina la Wimbo wangu wa Kitambaa Cheupe km Jina la Bar
 
Kwahio we unaamini hilo sababu yeye kasema? Halafu kila siku yule mwanae yupo site anasimamia ujenzi wa bar za kitambaa cheupe na juzi alifungua ya Mbagala? Ya Tabata iliungua akafungua upya na kisha kaongeza mbagala.
 
Mimi najua Mzee Kingi mutu ya Mungu uongo dhambi km ingekua ni hivyo katuongepea atajua mwenyewe atakachojibu huko anakokwenda ila alijibu hivyo mbele ya camera za TBC 1

Ngoja niisake ile Video ogopa Mungu ogopa teknolojia nakuja kuiweka hapa uone anavyojibu
 
King Kiki binafsi anaweza akawa hanufaiki hilo sikatai ila kuniambia familia yake hainufaiki kabisa ni uongo mkubwa. Labda kama hio familia anayozungumzia haimuhusishi yule binti yake ambaye ndio anamiliki hio brand ya kitambaa cheupe.
 
Sikiliza mkuu, nitasema kwa mara ya mwisho alisema yeye hausiki na Bar za Kitambaa Cheupe na Familia yake akiwemo yeye hawanufaiki na chochote ndio akaambiwa na mtangazaji aongee na watanzania akaanza kuomba msaada na kujielezea mbele ya camera kwa hio unataka kusema Mzee ametuongopea kabla hajafa?

Ngoja niifukue ile video huku nikuletee umsikie mwenyewe maana huamini ukiambiwa
 
Sawa mkuu
 
Wakati wa ujana wetu alitutumbuiza sana hasa alipohamia Safari Sound na kuanza kutoa ushindani mkubwa sana dhidi ya Marquiz chini ya mtindo wao wa Masantula. Enzi hizo kila jumapili Safari resort pale Kimara ilikuwa inajaa sana

Mungu alizae roho yake pema peponi
 
Back
Top Bottom