TANZIA Mwanamuziki Mkongwe, Boniface Kikumbi Mwanza Mpango (King Kikii) amefariki dunia

TANZIA Mwanamuziki Mkongwe, Boniface Kikumbi Mwanza Mpango (King Kikii) amefariki dunia

RIP Legend.

"Kitoto Kaanza Tambaa" ni wimbo ninaoupenda sana.

Ni wimbo unaozungumzia mtu anayeifikiria familia yake, anayefikiria mtoto mdogo anayeanza kutambaa maisha yake yatakuwaje, mtu anayefungua njia kitoto kaanza tambaa, mtu anayefikiria familia yake italelewa vipi, mtu wa kujali familia.

"Watoto wa kwangu, nani atawaleaa?
Familia ya kwangu, nani atawaleaa?
Mzigo wa kwangu, nani atauleaa?
Twende, fungua njia, kitoto kaanza tambaa"

Maudhui kama haya yanatoweka kwenye nyimbo nyingi za siku hizi.


View: https://youtu.be/0L0PseRXvmg?si=sJZqLplB6ZnClUcE
 
kuna ngoma moja inaitwa kasongo ni balaa kuna club moja Stockholm mzungu mmoja DJ ndio ngoma yake kila weekend itabidi ajulishwe kuwa mwenye ngoma yake katambaa, sijui mzungu aliijuaje hiyo ngoma maybe alishakujaga bongo enzi hizo.
 
RIP,
Nimeandika neno Hilo hapo kwa mazoea Tu ila najua jamaa yupo ila kaacha kaacha kuutumia MWILI huu na kuhamia kwenye "dimension" nyingine
 
Huyu mzee napenda nyimbo zake.Daaah,RIP.
Kwa waliomfahamu ,je,ana asili ya congo?Maana nikisikiliza mziki wake una vionjo na maneno yenye asili ya congo.Naomba ufafanuzi.
 
Uchwa umezi Bongo haki ya Mungu, tunaelekea kubaya sasa.

Tangazo la kifo cha nguli wa Kitambaa cheupe lina picha ya Samia ili iweje?
Screenshot_20241115_133320.jpg




Aiseee
 
Back
Top Bottom