Mwimbaji wa Marekani R. Kelly amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa makosa ya unyanyasaji wa kingono.
Mnamo Septemba, mahakama ya New York ilimtia hatiani msanii huyo wa R&B, mwenye umri wa miaka 55, kwa uhalifu wa ulaghai na ulanguzi wa ngono uliofanywa kwa zaidi ya miongo mitatu katika tasnia ya muziki.
Mzaliwa huyo wa Chicago - ambaye jina lake halisi ni Robert Sylvester Kelly - tayari amekaa gerezani kwa takriban miaka mitatu.
Kwa sasa anakabiliwa na mashtaka tofauti ya uhalifu katika kesi nyingine tatu.
NGOZI NYEUSI TUNAONEWA SANA.
View attachment 2276937