Mwanamuziki Robert Kelly (R. Kelly) afungwa kifungo cha miaka 30 jela

Mwanamuziki Robert Kelly (R. Kelly) afungwa kifungo cha miaka 30 jela

R.kelly hayo yasinge mkuta kuna kipindi nchi nyingi zilipenda hapate uraia ila kwa vile utamu wa USA na nyumbani basi 30 ndio unatumia mpaka kufa kwako
Ni wakati Gani na ni nchi zipi zilimtaka?
 
CHANZO ,REUTERS

Mwimbaji wa Marekani R. Kelly amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kutumia hadhi yake kuendesha mpango wa kuwadhalilisha kingono watoto na wanawake.

Mnamo Septemba, mahakama ya New York ilimtia hatiani msanii huyo wa R&B, mwenye umri wa miaka 55, kwa makosa ya ulanguzi na biashara ya ngono.

Mzaliwa huyo wa Chicago - ambaye jina lake halisi ni Robert Sylvester Kelly - pia alipigwa faini ya $ 100,000 (£ 82,525).

Kwa sasa anakabiliwa na mashtaka tofauti ya uhalifu katika kesi nyingine tatu.

Kelly - anayejulikana kwa nyimbo maarufu kama I Believe I Can Fly na Ignition - alipatikana kuwa alitumia hali yake ya umaarufu na nyanja ya ushawishi kuwavutia wanawake na watoto katika unyanyasaji wa kijinsia kwa zaidi ya miongo miwili

Katika hukumu yake siku ya Jumatano, Jaji wa korti ya Wilaya ya Marekani Ann Donnelly alisema mtu mashuhuri alitumia ngono kama silaha, na kuwalazimisha waathiriwa wake kufanya mambo yasiyoweza kuelezeka na kuwaambukiza na magonjwa yasiyotibika.

Adhabu hiyo, alisema, itakuwa kama kizuizi dhidi ya kufanya uhalifu kama huo katika siku zijazo.

Majaji katika kesi ya Kelly ya wiki sita huko Brooklyn walisikia jinsi alivyosafirisha wanawake kati ya majimbo tofauti ya Marekani , akisaidiwa na mameneja, walinzi na wanachama wengine wa msafara wake .

Mahakama pia ilisikiliza jinsi Kelly alipata hati za ndoa na mwimbaji Aaliyah kinyume cha sheria alipokuwa na umri wa miaka 15 mwaka wa 1994, miaka saba kabla ya mwimbaji huyo kufariki katika ajali ya ndege.

Cheti hicho, kilichovuja wakati huo, kiliorodhesha umri wa Aaliyah kuwa 18. Ndoa hiyo ilibatilishwa miezi kadhaa baadaye.

Waendesha mashtaka wa serikali walikuwa wamependekeza kwamba Kelly ahukumiwe kifungo cha zaidi ya miaka 25, kutokana na uzito wa uhalifu wake na "haja ya kulinda umma dhidi ya uhalifu zaidi".

Lakini mawakili wake walitaka kifungo cha miaka 10 - kiwango cha chini cha lazima kwa kuhukumiwa kwake - au chini ya hapo.

Walionyesha Kelly kama aliyekua katika hali ya umaskini katika maisha yaliyojaa unyanyasaji wa nyumbani na kuteswa kuanzia akiwa na umri mdogo
 
Waafrika tukipata mali tunaendekeza sana hanasa. Mwenyezi Mungu amsaidie kwenye rufani
 
Hapa inshu siyo mtu mweusi au mweupe.
Jela kivyovyote vile ukiona mtu kahukumiwa kwenda huko, siyo jambo la kukenua meno na kuchekelea.

Jela unaweza kwenda hata wewe, iwe umetenda kosa au haujatenda.
Utashangaa badae akikaa miaka kadhaa ataachiwa watasema alifungwa kimakosa ,lengo ni kujeruhi nafsi za wanadamu
 
Safi sana akafie jela
Kwa wasiojua tu huyu jamaa alikutwa kwenye laptop yake images za watoto wadogo mpaka miaka miwili wakiwa uchi akiwa ame download images zaidi ya Elfu tatu

Amebaka sana ameshiriki ngono kwa underage
Hakuna ubaguzi hapo bali alitenda madhambi yote
Kuna watu washenzi sana hivi unaanzaje kuwa na mapenzi ya kuangalia uchi wa mtoto wa miaka miwili au mitatu kama sio sicko?

Jeffrey Epstein alikuwa mweupe kafa na dhambi zake na alikuwa rafiki mkubwa wa Prince Andrew na watu wamemchukia Andrew kuwa na rafiki wa hivyo
Nae alikuwa na kesi kama hii hii ya Kelly na alihukumiwa miaka 20 jela na baadae kukutwa kafa jela ya Manhattan
 
Hii kesi ni ngumu sana kwa huyu jamaa,ila kama ni kweli aliyafanya hayo,hataweza kukwepa hiyo adhabu kwani zinaa haijawahi kumuacha mtu salama...
 
Mwimbaji wa Marekani R. Kelly amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa makosa ya unyanyasaji wa kingono.

Mnamo Septemba, mahakama ya New York ilimtia hatiani msanii huyo wa R&B, mwenye umri wa miaka 55, kwa uhalifu wa ulaghai na ulanguzi wa ngono uliofanywa kwa zaidi ya miongo mitatu katika tasnia ya muziki.

Mzaliwa huyo wa Chicago - ambaye jina lake halisi ni Robert Sylvester Kelly - tayari amekaa gerezani kwa takriban miaka mitatu.

Kwa sasa anakabiliwa na mashtaka tofauti ya uhalifu katika kesi nyingine tatu.


NGOZI NYEUSI TUNAONEWA SANA.
View attachment 2276937
Mkuu Ghislaine Maxwell kahukumiwa miaka 20 kwa kusaidia unyanyasaji. Hakuna suala la rangi hapa. Tatizo ndugu zetu wengi wakipata pesa na umaarufu wanageuka miungu. Wanataka kulazimisha kila wanachotaka.
 
Back
Top Bottom