Mwananchi aliyefiwa mtoto wake Muhimbili adaiwa kutakiwa kulipia Tsh. 10,695,000 ili kuikomboa maiti

Mwananchi aliyefiwa mtoto wake Muhimbili adaiwa kutakiwa kulipia Tsh. 10,695,000 ili kuikomboa maiti

The Palm Beach

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
1,967
Reaction score
4,267
Nisiseme mengi, mimi nimeleta humu Ili kuibua mjadala wa Sera ya Afya ya CCM na makandokando yake katika sekta na huduma za kiafya hapa nchini.

Hayo chini ndio maelezo ya ushuhuda wake aliyotuma kwa wanagrupu wenzake kule WhatsApp ili wamsaidie kumchangia pesa aweze kugomboa maiti wake ili akazike. Nimekopi na kupesti kama yalivyo. Nimeondoa majina yake na ya maiti wake kwa kuwa sikupata idhini yake kuposti kama ilivyo.

Ufafanuzi na utambulisho wa BABA Mfiwa

"..Tunasikitika kuwataarifu kuwa tumepata msiba wa mtoto, amefia Muhimbili ICU baada ya kukaa toka 11th May, 2024 na kufa 11th June, 2024 jioni.

"Ni binti wa....... (ni kijana wa kaka yetu......... kijana wa mama mdogo wa...........).

"Alikuwa ndiye anamtunza sana Mzee pale Kong'ongo hadi Mzee alipofariki, anaishi hapo hapo na MSIBA UKO HAPO HAPO. Inawezekana maziko yakawa leo tarehe 13 saa 10 jioni kama tukifanikiwa kupewa maiti Muhimbili.

Kikwazo ni Bill ambayo million 10,695,000/=. Wametupunguzia 2,000,000/= Muhimbili hospitali.

Deni tunalodaiwa ni Tsh. 8,695,000/= Ili turuhusiwe kuitoa maiti mochwari. Tumelia sana lakini wanataka tutafute 3,000,000/= kama advance kwa sasa ili watupatie mwili kwenda kuzika.

Wametuambia pia tuache kadi ya NIDA ya baba wa mtoto (marehemu). Balance itakayobaki tumeambiwa tutalipa polepole.

Ahsanteni sana."

Why is this?
 
Sera ya Bima ya Afya ilikuwa mbovu toka ilipoanzishwa, Kwa sababu sio endelevu na haikufanyiwa tathimini na wataalamu zaidi ya wanasiasa, kuweka Sera ambazo haziendani na uhalisia , upigaji, ubinafsishaji wa watoa huduma, ukopeshaji Kwa watoa huduma wa vifaa na majengo, wakati NHIF haina mamlaka juu ya hao watoa huduma .
 
Umesoma mpaka mwisho??
 
Mkapa ndio alianzisha haya mavi yanayoitwa NHIF!
 
Mkapa ndio alianzisha haya mavi yanayoitwa NHIF!
Sera ambayo ina changiwa na asilimia ndogo ya raia wako chini ya 10% haiwezi kudumu, na watunga Sera wetu walifuata , wataanza kuzijenga hospitali za watoa huduma kabla ya kujiimarisha mfuko wenyewe, na ofisi zikazidi kuongezea na magari ya offisini , bila kuwekeza zaidi kwenye sababu Kuu ya kuanzisha kwao.
 
Inatokea nini asipolipa, au wasipompa mwili wa marehemu wake?

CHURA kasema usicheze na UCHUMI WAKE, labda hiyo ndio theory behindi huozo huo.

Marehemu kawa ghali kiasi hicho ghafla, hata kumfanya mwenye marehemu kushindwa kumnunua kutoka mortuary.

Yani Gharama ya kumtibu ilikuwa rahisi kuliko gharama ya kuutoa mwili wa marehemu mortuary.
 
Nisiseme mengi. Mimi nimeleta humu Ili kuibua mjadala wa sera ya afya ya CCM na makandokando yake ktk sekta na huduma za kiafya hapa nchini.

Haya chini👇👇 ndio maelezo ya ushuhuda wake aliotuma kwa wanagrupu wenzake kule WhatsApp ili wamsaidie kumchangia pesa aweze kugomboa maiti wake Ili akazike. Nimekopi na kupesti kama yalivyo. Nimeondoa majina yake na ya maiti wake.

"Ufafanuzi na utambulisho wa BABA Mfiwa".

"..Tunasikitika kiwataarifu kuwa tumepata msiba wa mtoto, amefia Muhimbili ICU baada ya kukaa toka 11th May 2024 na kufa 11th June 2024 jioni.

Ni Binti wa....... (ni kijana wa Kaka yetu......... kijana wa Mama mdogo wa...........)

Alikuwa ndiye anamtunza sana Mzee pale Kong'ongo hadi Mzee alipofariki), anaishi hapo hapo na MSIBA UKO HAPO HAPO inawezekana maziko yakawa Leo tarehe 13 saa 10 jioni kama tukifanikiwa kupewa maiti Muhimbili.

Kikwazo ni Bill ambayo million 10,695,000/=. Wametupunguzia 2,000,000/= Muhimbili hospitali.

Deni tunalodaiwa ni TZS 8,695,000/= Ili turuhusiwe kuitoa maiti mochwari. Tumelia sana lakini Wanataka tutafute 3,000,000/= kama advance kwa sasa ili watupatie mwili kwenda kuzika.

Wametuambia pia tuache kadi ya NIDA ya baba wa mtoto (marehemu). Balance itakayobaji tumeambiwa tutalipa polepole.

Ahsanteni sana."

Why is this?
Bima ya afya ni muhimu wana

Tukate bima za afya
 
Back
Top Bottom