Mwananchi aliyefiwa mtoto wake Muhimbili adaiwa kutakiwa kulipia Tsh. 10,695,000 ili kuikomboa maiti

Mwananchi aliyefiwa mtoto wake Muhimbili adaiwa kutakiwa kulipia Tsh. 10,695,000 ili kuikomboa maiti

Sijui watu weusi ni nili tutaachana na ujinga,mfano fikiria umekomboa maito million kumi,then uabze michakato ya gharama za kuzika Tena pengine ifike million 8 pamoja na kulisha watu.Ni Bora nikae kimya watazikaga wenyewe .
 
Hapo kuna makubaliano kwani ndugu?

Walichopewa ni bill ya maiti na siyo matibabu

Kwa maoni yangu, nafikiri, ni lazima kuwe na utaratibu wa kufuta gharama yoyote ya matibabu iwapo mgonjwa atafia hospitalini..

Hawa wapewe bill ya kutunza maiti tu kule mochwari kwa siku mbili au tatu ambayo Nina hakika haizidi 300,000.

Lakini serikali kumwomba mwananchi wa kawaida kama huyu mamilioni yote hayo kwa mtu aliyekwishafariki kwa wao kushindwa kuokoa uhai wake, mimi naona sio sahihi!!
Naheshimu maoni yako lakini naona ugumu katika utekelezaji wake. Huyu inaonekana ni rahisi kufuta deni kwa kuwa alikuwa hajalipa. Vipi kwa ambaye anakuwa kishalipa na hadaiwi chochote ikatokea bahati mbaya akafariki, na huyo unapendekeza nndugu zake warejeshewe hela waliyolipa au wampotezee? Ila wazo lako likikubaliwa lisiishie hospitali tu liende hadi shuleni/vyuoni ambapo kama mzazi kalipa ada na mtoto akafeli basi ada irushwe
 
Naheshimu maoni yako lakini naona ugumu katika utekelezaji wake.
Hili la kuheshimiana na kuheshimu maoni na mitazamo ya wengine ni zuri💪
Huyu inaonekana ni rahisi kufuta deni kwa kuwa alikuwa hajalipa.
Kwa wapenda pesa kama CCM, si rahisi. Wanaweza hata kuwafungulia mashitaka
Vipi kwa ambaye anakuwa kishalipa na hadaiwi chochote ikatokea bahati mbaya akafariki, na huyo unapendekeza nndugu zake warejeshewe hela waliyolipa au wampotezee?
Hawa walikuwa na uwezo ndio maana wamelipa. Tunapotunga sera fulani, basi hiyo sera lazima isiwe na ubaguzi. Sipendekezi hili
Ila wazo lako likikubaliwa lisiishie hospitali tu liende hadi shuleni/vyuoni ambapo kama mzazi kalipa ada na mtoto akafeli basi ada irushwe
That's irrelevant comparison!

Huyu aloyefeli mtihani yuko hai. Kwa makosa yake tu fulani fulani e.g uvivu, uzembe, carelessness nk kafeli.

Nevertheless, waliofeli mitihani mashuleni/vyuoni ziko options nyingi wanazoweza ku - opt ili kurekebisha makosa yao with very low cost e.g kuna kitu kinaitwa supplementary exams, resitting exams nk

Kwa uhai wa mtu, there's no supplementary. Hakuna mbadala

Mtu akishakufa, that is the end of everything about him/her!
 
Nadhani anachodaiwa sio gharama za 'kukomboa maiti' kama unavyodai ila ni gharama za matibabu alizopata akiwa anatibiwa. Kama unaona hastahili kudaiwa basi ata wagonjwa wanaokuwa wamelipa gharama za matibabu na ikatokea wakafariki basi nao ungependekeza wawe wanarudishiwa pesa wanazolipa. Binafsi naona Muhimbili wamejali uhai kwanza na ndio maana waliendelea kutoa huduma bila kujali deni limefikia kiasi gani. Kama ni kweli wahusika hawana uwezo wa kulipa kuna utaratibu mzuri tu wa kufuata ili jambo lao lifanyiwe kazi]
Shida sio kudaiwa Shida nikushikilia maiti kama dhamana ya deni kulipwa Hilo jambo kwako unaona ni sawa?
 
Shida sio kudaiwa Shida nikushikilia maiti kama dhamana ya deni kulipwa Hilo jambo kwako unaona ni sawa?
Deni tunalodaiwa ni Tsh. 8,695,000/= Ili turuhusiwe kuitoa maiti mochwari. Tumelia sana lakini wanataka tutafute 3,000,000/= kama advance kwa sasa ili watupatie mwili kwenda kuzika.

Wametuambia pia tuache kadi ya NIDA ya baba wa mtoto (marehemu). Balance itakayobaki tumeambiwa tutalipa polepole.

Ahsanteni sana."
 
Nadhani anachodaiwa sio gharama za 'kukomboa maiti' kama unavyodai ila ni gharama za matibabu alizopata akiwa anatibiwa. Kama unaona hastahili kudaiwa basi ata wagonjwa wanaokuwa wamelipa gharama za matibabu na ikatokea wakafariki basi nao ungependekeza wawe wanarudishiwa pesa wanazolipa. Binafsi naona Muhimbili wamejali uhai kwanza na ndio maana waliendelea kutoa huduma bila kujali deni limefikia kiasi gani. Kama ni kweli wahusika hawana uwezo wa kulipa kuna utaratibu mzuri tu wa kufuata ili jambo lao lifanyiwe kazi
 
Back
Top Bottom