Mwananchi aliyefiwa mtoto wake Muhimbili adaiwa kutakiwa kulipia Tsh. 10,695,000 ili kuikomboa maiti

Mwananchi aliyefiwa mtoto wake Muhimbili adaiwa kutakiwa kulipia Tsh. 10,695,000 ili kuikomboa maiti

Nisiseme mengi. Mimi nimeleta humu Ili kuibua mjadala wa sera ya afya ya CCM na makandokando yake ktk sekta na huduma za kiafya hapa nchini.

Haya chini👇👇 ndio maelezo ya ushuhuda wake aliotuma kwa wanagrupu wenzake kule WhatsApp ili wamsaidie kumchangia pesa aweze kugomboa maiti wake Ili akazike. Nimekopi na kupesti kama yalivyo. Nimeondoa majina yake na ya maiti wake.

"Ufafanuzi na utambulisho wa BABA Mfiwa".

"..Tunasikitika kiwataarifu kuwa tumepata msiba wa mtoto, amefia Muhimbili ICU baada ya kukaa toka 11th May 2024 na kufa 11th June 2024 jioni.

Ni Binti wa....... (ni kijana wa Kaka yetu......... kijana wa Mama mdogo wa...........)

Alikuwa ndiye anamtunza sana Mzee pale Kong'ongo hadi Mzee alipofariki), anaishi hapo hapo na MSIBA UKO HAPO HAPO inawezekana maziko yakawa Leo tarehe 13 saa 10 jioni kama tukifanikiwa kupewa maiti Muhimbili.

Kikwazo ni Bill ambayo million 10,695,000/=. Wametupunguzia 2,000,000/= Muhimbili hospitali.

Deni tunalodaiwa ni TZS 8,695,000/= Ili turuhusiwe kuitoa maiti mochwari. Tumelia sana lakini Wanataka tutafute 3,000,000/= kama advance kwa sasa ili watupatie mwili kwenda kuzika.

Wametuambia pia tuache kadi ya NIDA ya baba wa mtoto (marehemu). Balance itakayobaji tumeambiwa tutalipa polepole.

Ahsanteni sana."

Why is this?
Hiyo pesa imejumuishwa kwenye bajeti ya pato la serikali 2024/2025, tukifa wengi serikali yetu itapata pato kubwa, tuoneshe uzalendo.
 
Nisiseme mengi. Mimi nimeleta humu Ili kuibua mjadala wa sera ya afya ya CCM na makandokando yake ktk sekta na huduma za kiafya hapa nchini.

Haya chini👇👇 ndio maelezo ya ushuhuda wake aliotuma kwa wanagrupu wenzake kule WhatsApp ili wamsaidie kumchangia pesa aweze kugomboa maiti wake Ili akazike. Nimekopi na kupesti kama yalivyo. Nimeondoa majina yake na ya maiti wake.

"Ufafanuzi na utambulisho wa BABA Mfiwa".

"..Tunasikitika kiwataarifu kuwa tumepata msiba wa mtoto, amefia Muhimbili ICU baada ya kukaa toka 11th May 2024 na kufa 11th June 2024 jioni.

Ni Binti wa....... (ni kijana wa Kaka yetu......... kijana wa Mama mdogo wa...........)

Alikuwa ndiye anamtunza sana Mzee pale Kong'ongo hadi Mzee alipofariki), anaishi hapo hapo na MSIBA UKO HAPO HAPO inawezekana maziko yakawa Leo tarehe 13 saa 10 jioni kama tukifanikiwa kupewa maiti Muhimbili.

Kikwazo ni Bill ambayo million 10,695,000/=. Wametupunguzia 2,000,000/= Muhimbili hospitali.

Deni tunalodaiwa ni TZS 8,695,000/= Ili turuhusiwe kuitoa maiti mochwari. Tumelia sana lakini Wanataka tutafute 3,000,000/= kama advance kwa sasa ili watupatie mwili kwenda kuzika.

Wametuambia pia tuache kadi ya NIDA ya baba wa mtoto (marehemu). Balance itakayobaji tumeambiwa tutalipa polepole.

Ahsanteni sana."

Why is this?
Hii nayo ni hbr au chuki kwa serikali ndiyo inakusumbua. Hiyo ni bill ya matibabu, cha ajabu ni nini we bwege?
 
Sera ya Bima ya Afya ilikuwa mbovu toka ilipoanzishwa, Kwa sababu sio endelevu na haikufanyiwa tathimini na wataalamu zaidi ya wanasiasa, kuweka Sera ambazo haziendani na uhalisia , upigaji, ubinafsishaji wa watoa huduma, ukopeshaji Kwa watoa huduma wa vifaa na majengo, wakati NHIF haina mamlaka juu ya hao watoa huduma .
Tuliza makalio uelewe
 
Hata kama n mm ndio nimekufa nisingependa ndugu zangu watoe hiyo pesa ili kuuchukua mwili wangu 😎
Mimi nasemaga hata wautupe mzoga wangu porini au wauache nizikwe na greda la halmashauri ni sawa tu. Sitakuwepo. Sitasikia maumivu yo yote. Shida hizi zingine ni mbwembwe za binadamu tu.

Uzikwe na dunia nzima kama Mandela, Papa John Paul II na Princes Diana; au uliwe na simba Serengeti na mzoga wako usionekane tena - kimsingi kuna tofauti gani kwako wewe marehemu? 🤔🤔🤔
 
Suala la kukomboa maiti mahospitalini serikali ifikirie mara mbili! Serikali i-subsidize kutunza watanzania wenzetu waliotangulia mbele za haki. Inatia uchungu sana.
Ni hii serikali kupitia SSH ilihaidi timu ya taifa stars kitita cha mil100! Ikiifunga Zambia (chipolopolo). Sasa inashindwaje kulipa hiyo bill?

Povu ruksa, nimekaa hapa.
 
Bima gani!,Bima inayoweza kusaidia gharama za matibabu ni ile ya waajiriwa lakini ikiwa wewe sio muajiriwa inakubidi ukate zile wanaita za vifurushi ambazo ni utapeli mtupu kwa sababu zenyewe zina gharamia huduma chache za gharama za chini kama kumuona daktari,vipimo vidogo vidogo vya maabara,dawa kama panadol,antibiotics zile wanaita 1st line,x-ray na ultrasound lakini vipimo kama CT scan ni mara moja kwa mwaka na unatakiwa uchangie cash kwa asilimia fulani,MRI utajijua mwenyewe yaani kwa ujumla msaada wake ni kidogo sana.
Msisikilize wanasiasa ni waongo sana.
Unahitaji elimu ya bure

Sisi tumeamua kukata hizo kwa ndugu zetu na zinafanya kazi

Nhif wana shida ya advocacy tu… lakini vitita vipo Tena vizuri sana
 
Mpumbavu wewe,mimi nimehudhuria kliniki kadhaa pale Muhimbili ikiwemo ya Gastrointestinal na ya Macho vipimo na matibabu mengi zaidi ya 80% unaambiwa havilipiwi na hiyo bima yako ya vifurushi na kwa bahati mbaya sana ikitokea hivyo utatozwa kama mgonjwa wa private,mfano kuna kipimo kimoja cha macho bima(hiyo ya vifurushi) hailipii sasa utatakiwa ulipie cash unatozwa TSh 100,000 (private category) lakini kipimo hikohiko mgonjwa ambaye hana bima kabisa yeye anatozwa kwa category ya public atalipia 60,000,sasa hapo hiyo bima imekusaidia nini!
Nimefanya OGD 137,000 na nimebana mishipa kwenye koo kwa mara moja ni zaidi 400,000 zote hizo nimelipia cash.
Mpumbavu wewe, mama yako, baba yako, bibi zako, babu zako, kichwa chako, diagnosis zako zote, treatments zote ulizopata, Kama una vitoto navyo vipumbavu…. Pumbavu hadi vyombo ubagyotumia kula na kila kitu kinachokuhusu.. hata hiyo mishipa uliyobana ni pumbavu

Kuna packages mbalimbali za bima inategemea ndugu zako wanakuchangia kiasi gani

Na Kama hutaki nhif kuna nyingine za strategis, alliances etc

Mara bima Acha upumbavu

Hutaki bima funga nyoro

Nalaaabuk wahed
 
Back
Top Bottom