Mwananchi aomba siku ya Ijumaa iwe siku ya Mapumziko

Mwananchi aomba siku ya Ijumaa iwe siku ya Mapumziko

Nao Wasabato wakikaza, na dini nyingine ikija wakichagua j3 kama siku ya kusanyiko itakuwaje?
Huyo mtu katumwa
 
Katika Mashindano ya Kuhifadhi Qoran kwa Wasichana yanayofanyika kwenye Uwanja wa Mkapa, Mmoja wa Wananchi alipopata nafasi ya kutoa salamu, Amewaomba wanaohusika kuifanya Ijumaa kuwa Siku ya Mapumziko kama ilivyo Jumapili ambapo amedai badala yake Jumamosi iwe siku ya kazi.

Akitetea hoja yake amesema kwamba, Siku ya Ijumaa Maofisi ya umma yanakuwa hayana wafanyakazi kwa vile wengi wao wanakuwa wakijiandaa na Ibada, jambo linaloleta usumbufu kwa Wananchi, ili kuondoa usumbufu huo ni bora siku hiyo ikawekwa kuwa ya mapumziko na Jumamosi ifidie.

Soma Pia: Rais Samia akishiriki tamasha la Mashindano ya Kuhifadhi Quran kwa Wanawake


Binafsi Naunga Mkono hoja yake
Mapumziko yaanze alhamisi
 
Huyu tahira katumwa.
Kwanini hajazungumzia haki ya Wasabato?
Swali: Kama Ijumaa sala inaanza saa sita maana yake maandalizi yanafanyika saa 4 mpaka saa 5. Hiyo saa tano alienda ofisi ya umma na kuacha Sala ya Ijumaa?
 
Naona mapumziko tuanze ijumaa mpka j2
Hapa makundi yote ya dini naona yatakuwa yamezingatiwa
Siku za kazi kazi ni 24hrs
 
Hizi timu Tatu za dar es salaam ni taasisi za dahwa. Huwa nashangaa Imani nyingine wanajinadibu timu yetu. Ona hata wakiitisha sala kuiombea timu aina ya wsombaji na aina yasombi

Hakika inashangaza mtu wa Njombe n.k huko bara au visiwani kujinasibu na timu hizi.

Brazil huwezi kuta Botafogo de Futebol e Regatas ya Rio ikawa inashabikiwa kwa ukubwa huko Sao Paolo au timu ya Sport Club Corinthians Paulista yenye makao yake Sao Paolo ikawa inaenziwa Rio de Janeiro.

Timu hizi za Kariakoo zina wenyewe, huwezi kuona mtu wa mitaa hii ya Kariakoo mzaliwa hospitali za Ocean Road, Hindu Mandal n.k au mwenyeji wa Dar es Salaam hii kushabikia Mashujaa FC ya Kigoma n.k
 
Huko Zanzibar wakati WA mfungo Wanafunzi hawaendi shule mwezi mzima
 
Hawa vijana wa mnyaazi mungu wana matatizo ya akili kweli hakuna hoja yoyote ya msingi aliyo ongea kuunga mkono upuuzi alioongea
 
Ni suala zuri sana! Ijumaa kuwa siku ya mapumziko ila kuna maswali haya ya kujiuliza:
1. Endapo tukifanya Ijumaa iwe siku ya mapumziko, Je ikitokea Alhamis kuna sikukuu ya kitaifa pamoja na Jumatatu, je ni sahihi watu kufanya kazi siku tatu katika wiki inayofuata?
2. Leo mmeomba Ijumaa iwe siku ya mapumziko kwa misingi ya dini, je na waumini wa dini zingine wanayo haki ya kuomba siku kama Jumatatu, Jumanne, Jumatano na Alhamis ziwe siku za mapumziko.

NB:
“YEYE NDIYE ALIYEFANYA ARDHI IWE INAWEZA KUTUMIKA (Kwa kila myatakayo) KWA AJILI YENU. BASI NENDENI KATIKA PANDE ZAKE ZOTE NA KULENI KATIKA RIZIKI YAKE, NA KWAKE YEYE NDIO MAREJEO (yenu nyote)” (67: 65)
“NA ITAKAPOKWISHA SWALA (kuswaliwa) TAWANYIKENI KATIKA ARDHI MTAFUTE FADHILA ZA ALLAH……….” (62:10).


Nae Bwana Mtume Rehema na Amani zimminikie – anasema katika hadithi – Qudsi:

“ Hakika Allah anasema: Ewe mja wangu wee! Utikise mkono wako nikuteremshie riziki”
”BASI NENDENI KATIKA PANDE ZAKE ZOTE NA KULENI KATIKA RIZIKI ZAKE……” (67:15).

Someni Surah al-Najm (53:39), pia Surah al-Anfal (8:71) mpate kufahamu Allah anatuhimiza kufanya kazi lakini tusisahau swala.

Assalamu Alaikum Warahmatullahi wabarakatuhu
 
Baada ya hili ombi la huyu Mzee, ombi jingine litafuata mfano mfungo wa Ramadhani nini tuiombe serikali yetu tukufu Tanganyika ilifanyie kazi ili mfungo uende vizuri sote tupate thawabu nchini Tanzania?
 
Hv Kwan wkeend, yaan jumamosi na jumapili ziliwekwa kutokana na ishu za ibada? Tuanzie kwanza hapa
 
Kuna ugumu happ, ukiweka ijumaa kuwa mapumziko alafu jumamosi iwe siku ya kazi alafu jumapili mapumziko alafu jumatatu siku ya kazi

Huo ni mchanganyiko ambao ni mgumu mno. It's impossible
 
Alitakiwa aombe Ijumaa iwe pumziko kwake binafsi wala Siyo swala la Dini maana Qur'an inamtaka akishamaliza kuswali akatafute riziki.Ina maana akafanye Kazi.Wale waumini wa Biblia wanajua Siku ya 7 ni Kupumzika,kustarehe na Kufanya Ibada.Hawasubiri kupangiwa na mwanadamu wala Serikali maana Mungu alishatoa agizo hata kabla ya gharika.Na akakumbusha tena Kupitia Kwa Musa (Rejea Kutoka 20:8-11).Ikumbuke Siku ya Sabato uitakase.Hata ukiweka bunduki Sabato tutaabudu,Sabato tutapumzika,Sabato hatufanyi Kazi.Nikiwa JKT kuna afande alitutisha kutuua.Tukamwambia huna hayo Mamlaka.By the way Sabato Njema wajoli wa Bwana.
 
Mimi nashauri tuanishe mfumo wa kulipana kwa masaa badala ya mwisho wa wiki, au mwezi kama ilivyo sasa.

Huu mfumo ukianzishwa, hakuna mtu mwenye akili timamu atalilia muda wa mapumziko ili akaswali/akasali. Badala yake watu watakuwa busy kufanya kazi kwa masaa mengi zaidi tu ili mwisho wa mwezi wapate mishahara minono.
Sahihi, naunga mkono hoja.
 
Back
Top Bottom