DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kabisa mkuu, huyu Dr anapaswa kuchunguzwa vyeti vyake na post mortem ifanyike upya.
 
kupasuka bandama ni dalili ya cancer ya damu?
 
Katika michango yoote iliyotolewa katika thread hii, comment hii imetolewa na mtu mwenye akili tulivu, mwenye kutafakari mambo kwa kina na kifanisi sana.

Jamani hivi kweli mwalimu aweza kuadhibu mtoto kwa nguvu ya juu ya kadiri, eti mangumi?

Walimu watumie miongozo gani kulea watoto wetu mashuleni sasa?

Najiuliza nabakia njia panda.

Nadhani jambo hili lifanyiwe uchunguzi huru ili haki itendeke pasiwe na bias ya kumbeba yeyote.

Mkasa huu unaleta simanzi sana, lakini usichukuliwe kwa mihemko ama kiushabiki, hapana.

Natanguliza pole zangu za dhati kwa wafiwa pamoja na walimu pia.
 
Yaani upo field hujui hata kam uta graduate unaanza kupig watot ngumi et hasira aisee
 
Kweli kabisa mkuu. Kwanza hii criminal offence lakini waziri anataka ipelekwe kwenye dawati la jinsia ili iweje? Kwani huu ni mgogoro wa ndoa? Hii moja kwa moja ni criminal case wala haina uhusiano wowote na masuala ya jinsia.

Nchi hii ina viongozi mbumbumbu sana. Mtu anaona kabisa mwananchi kakosea njia bado anasmsisitiza aende huko huko. Na inawezekana hata mkuu wa dawati alimshauri aende mahakamani lakini kwa kuwa waziri alimshauri amuone mtu wa dawati basi akawa amebaki njia panda.

Hili nitukio la ajabu sana kutendeka katika nchi inajidai kuzingatia haki za raia. Katika kesi kama hii haki iko wapi sasa?
 
Ujinga ujinga tu. Wewe ulipigwa ngumi za bandama ulipokuwa drs la 1?
 
Nyie wenzetu mnaishi nchi Gani mwanamme mzima mwenye familia anabaka kitoto Cha miaka mi3 sembuse mwalimu kumpiga ngumi mtoto wa miaka 7?
 
Tatizo sio limempata nani? Suala ni uhalisia wa jambo husika. Je, ungekuwa wewe ni huyo Mwalimu unapewa tuhuma zisizo na uhalisia na kuhukumiwa na jamii ungejisikiaje?
Umemchapa mtoto, kafa lazima ujieleze kilichotokea sio unafichwa fichwa kama mwali. Kama ulimchapa kwa weledi kwanini unafichwa fichwa? Unatetea ujinga ujinga tu.
 
Tafuta ndugu zako mkafanye fujo hapo shulen hakikisha iwe fujo mpka waandishi wa habari waje shule ifungwee kwa muda .. hapo tatizo lako litakuwa limesikika kikamilifu. Au chukua maiti ya mwanao beba mpka shule
 
Wewe Hakimu tuambie namna gani fimbo za Mwalimu zimemuua huyo mtoto na kumletea cancer ya damu?
Acha kutetea ujinga. Huyo mwalimu aliyemchapa anatakiwa aeleze ni nini kilitokea. Mtoto kafariki unatetea pasiwe na maelezo ya aliyemtandika?

Kansa ya damu hata kama alikuwa nayo inaua baada ya fimbo? Mtu mzima tu tena mzee wa miaka 90 mwenye magonjwa yote unayoyajua wewe ukimwingiza ndani kwako akafia huko na hukumgusa unawajibika kutoa maelezo, huyo mwalimu kwanini asijulikane akajieleza?
 
inauma sana asee Mungu akutie nguvu
 
Mkuu inakuja akilini eti mtoto wa darasa la kwanza kachelewa namba then mwalim ampige ngumi? Hivi kweli? Hapa kuna vilivojificha watoto skuhz wanadanganya sana.

Ukute mtoto alipigana na wenzake au alipata kiajali flan kikampelekea kupata maumivu na majeraha yalompelekea kufa lakini aliogopa kusema ukweli kwa wazaz bas akamsukumizia mwalim aliyemuadhibu labda kwa ka kiboko kamoja au tuwili twa miguuni au mkononi
 
jaribu pia kwenda kufungua kesi kwenye vyombo vya usalama
 
Nyie wenzetu mnaishi nchi Gani mwanamme mzima mwenye familia anabaka kitoto Cha miaka mi3 sembuse mwalimu kumpiga ngumi mtoto wa miaka 7?
Swala la kubaka linasabbshwa na vitu tofaut kabsa na swala tunaloongelea hapa.

Obviously mwalim kumpiga ngum mtoto wa darasa ya kwanza ni swala fikirishi sana.

Lakini ukiambiwa mtu mzima kambaka mtoto wa miaka 10 utaenda Moja kwa moja kwenye maswala kama imani za kishirikina na matamanio ya mwili yaliyomshinda mtekelezaj wa kosa hilo.

Mwalim sawa kuna mambo ya hasira lakini sio kiasi cha kumpiga mtoto ngumi ya mbavu mpaka kumjeruhi bandana nakataa
 
Ukweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…