DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Pole sanaa mkuu... lkn inawezekana ilikua bahati mbaya mpaka ikapelekea umauti wa mwanao, pia walimu wengi wana na matatizo ya afya ya akili, amini ivo.. msamehe tu hata akikamatwa leo, uhai wa mwanao hautarejea.. pole sanaa Mungu akutie nguvu kwenye hili gumu.
 
Kingine wazazi na walezi wengi huwa hawatilii maanani medical form zitolewazo na taasisi kama shule kwa wanafunzi kipindi wanapohitaji kujiunga na shule.

Unakuta mzazi anampa pesa kidogo mtaalam wa afya, kisha mtaalam anajaza tu mtoto yupo sawa. Kumbe unakuta mtoto anamashida yake mengi ya kiafya. Pengine angempimwa na kukutwa na shida flani, basi angejumuishwa katika kundi la watoto wanaohitaji special care and treatment mashuleni.
 
Ulikuwepo wakati akipigwa hizo ngumi? Umeambiwa Kansa ya damu inaweza kusababisha kupasuka kwa bandama( Kitaalam I naitwa Spontaneous Rupture of Spleen) bado umekazana kusema alipigwa ngumi!
Ww jamaa kama ni Dr basi unajidhalilisha humu ndani, yaani umen'gan'gania Spontaneous rupture of spleen tu, ushaambiwa dogo alichapwa fimbo kwann usianzie hapo kwanza? Hiyo sababu unayotuletea humu ndani inge make sense kama huyo marehemu asingekuwa amekumbana na tukio lolote.
 
Hakuna mwalimu anayeweza kumpiga mtoto ngumi tena mtoto wa darasa la kwanza, huyo mtoto labda alipigana na wenzake au alipata ajali, uchunguzi wa kina ufanyike. Kuchelewa namba hakuwezi kumfanya mwalim ampigie mtoto ngumi ya tumboni.

Nimulize kitu hapa.

Siku hiyo adhabu ilipotekelezwa na huyo mwalimu kwa marehemu je ni wanafunzi wangapi walikuwa wamechelewa namba?

Hiyo ngumi alipigwa huyo marehem tu au walipigwa wanafunzi zaid ya huyo marehemu?

Hiyo adhabu ilitolewa katika mazingira gani? ili ushahidi uwe wa kina zaidi

Zaidi ya yote niseme kwamba, poleni sana wazaz, ndugu, jamaa na wote tulioguswa na msiba huu. Mungu amrehemu marehemu! Amina.
Your reasoning faculty paralysed
 
Ulikuwepo wakati akipigwa hizo ngumi? Umeambiwa Kansa ya damu inaweza kusababisha kupasuka kwa bandama( Kitaalam I naitwa Spontaneous Rupture of Spleen) bado umekazana kusema alipigwa ngumi!

Kwanini mnalazimisha chuki zenu, na roho mbaya za Kitanzania zitamalaki juu ya Walimu wanaofanya kazi ngumu ya kuwalea watoto wenu wenye malezi mabaya ya single mothers?
Nipo pamoja nawew
 
Ulikuwepo wakati akipigwa hizo ngumi? Umeambiwa Kansa ya damu inaweza kusababisha kupasuka kwa bandama( Kitaalam I naitwa Spontaneous Rupture of Spleen) bado umekazana kusema alipigwa ngumi!
Acha UJINGA. Wewe ndo huyo mwalimu? Mwalimu amekataa kuwa hakumpiga ngumi kama madai ya mzazi anavyosema? Huyo mwalimu yupo wapi aseme kuwa hakumpiga mangumi na mateke? Hapa hoja ni upatikanaji wa huyo mwalimu ambaye tukio la kifo limeanzia kwake. Ajieleze. Alimpiga mtoto kwa kiwango gani.
 
Naitwa Janeth Shayo, mkazi wa Uru, Moshi. Naomba unisaidie kupaza sauti mwanangu Jonathan Makanyaga (07) mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Mrupanga, ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inataka kupindishwa.

Tar.28/02/2024 mwanangu alienda shuleni akiwa mzima. Alipofika aliadhibiwa kwa kuchelewa "namba". Alipoingia darasani alianza kutokwa damu puani na mdomoni. Akarudishwa nyumbani. Nilipomkagua nikamkuta na majeraha yaliyovilia damu mgongoni, kwenye mbavu na mguuni.

Kesho yake nikaenda nae shuleni kutaka kuoneshwa mwalimu aliyemfanyia ukatili mwanangu. Lakini Mwalimu mkuu akaomba nibaki nje. Akaingia na mwanangu ofisi ya walimu na kumtaka amtambue Mwalimu aliyemuadhibu. Mwanangu akamtanbua. Mwalimu Mkuu akaniambia wameshamfahamu ni mwalimu wa "Field" hivyo atazungumza nae.

Wakanipa 20,000/= za matibabu. Nikampeleka mwanangu zahanati. Kesho yake akazidi kutoka damu, na kulalamikia maumivu sehemu za mbavu. Nikampeleka hospitali ya masista. Daktari akaniambia bandama imejeruhika ndio sababu ya kutoka damu mdomoni. Mtoto alidai pamoja na viboko alivyochapwa, Mwalimu pia alimpiga ngumi tumboni. Huenda ndiyo iliyopasua bandama.

Hali yake ilizidi kuwa mbaya tukapewa rufaa kwenda KCMC. Akatakiwa kufanyiwa upasuaji. Gharama 350,000/= lakini sikuwa nayo. Nikapiga simu shuleni wakasema tuombe afanyiwe halafu watalipa baadae. Hata hivyo kabla hajafanyiwa hali yake ikazidi kuzorota, akashindwa kupumua, akawekwa kwenye Oxygen. Akashindwa kula, akawekewa mpira wa chakula. Baada ya siku chache akafariki 😭.

Lakini ripoti ya hospitali inasema mwanangu amekufa kwa kansa ya damu. Kansa gani ya damu inayomuua mtoto kwa wiki mbili? Na kwanini hiyo kansa itokee baada ya kuadhibiwa shuleni? Kwanini Mwalimu aliyemuadhibu mwanangu anafichwa, na sipewi haki ya kumfahamu?

Nalazimishwa nichukue maiti nikazike lakini nimekataa. Nataka uchunguzi huru. Nimeenda dawati la jinsia kulalamika nikapuuzwa. Nimepiga simu kwa Waziri Dkt. Gwajima D akanipa namba ya mtu wa kunisaidia. Nilipopiga kumbe ni yuleyule Mkuu wa dawati la jinsia aliyenipuuza. Nikamrudia Gwajima akasema niwasiliane nae huyohuyo. Nimekosa pa kulilia haki ya mwanangu Jonathan
Waliohusika na kumdhulumu haki ya kuishi mtoto huyu wote wawajibishwe.

Ifikie hatua kuongezwe kigezo cha utimamu wa afya ya akili hasa empathy kwa watumishi wanaohudumia wasio na uwezo/mamlaka juu yao ikiwemo madaktari na waalimu wa watoto wadogo.
 
Hakuna mwalimu anayeweza kumpiga mtoto ngumi tena mtoto wa darasa la kwanza, huyo mtoto labda alipigana na wenzake au alipata ajali, uchunguzi wa kina ufanyike. Kuchelewa namba hakuwezi kumfanya mwalim ampigie mtoto ngumi ya tumboni.

Nimulize kitu hapa.

Siku hiyo adhabu ilipotekelezwa na huyo mwalimu kwa marehemu je ni wanafunzi wangapi walikuwa wamechelewa namba?

Hiyo ngumi alipigwa huyo marehem tu au walipigwa wanafunzi zaid ya huyo marehemu?

Hiyo adhabu ilitolewa katika mazingira gani? ili ushahidi uwe wa kina zaidi

Zaidi ya yote niseme kwamba, poleni sana wazaz, ndugu, jamaa na wote tulioguswa na msiba huu. Mungu amrehemu marehemu! Amina.
Wewe hujaguswa na msiba huu, na umeshahitimisha kuwa marehemu alipigana na wenzake au alipata ajali, mimi wakati nasoma tena nikiwa mdogo kabisa kuna mwalimu wa hesabu liyeitwa Marandu,aliwahi kuniambia kabisa kuwa ananichukia bila sababu yoyote, nilipomweleza mzazi wangu akanihamisha shule fasta, mwalimu kama huyo angeweza kuniua bila sababu yoyote!!
 
Acha UJINGA. Wewe ndo huyo mwalimu? Mwalimu amekataa kuwa hakumpiga ngumi kama madai ya mzazi anavyosema? Huyo mwalimu yupo wapi aseme kuwa hakumpiga mangumi na mateke? Hapa hoja ni upatikanaji wa huyo mwalimu ambaye tukio la kifo limeanzia kwake. Ajieleze. Alimpiga mtoto kwa kiwango gani.
Hapa tumepeta maelezo ya mzaz tayr ushachagua upande, nikulize maelezo ya mwalim umeyapata?

Mzaz n mwanadam kam tulivo wengine anaweza kudanganya pia ndomana hata mahakamani pande mbili zote husikilizwa na ushahidi wao huzingatiwa
 
Swala la kubaka linasabbshwa na vitu tofaut kabsa na swala tunaloongelea hapa.

Obviously mwalim kumpiga ngum mtoto wa darasa ya kwanza ni swala fikirishi sana.

Lakini ukiambiwa mtu mzima kambaka mtoto wa miaka 10 utaenda Moja kwa moja kwenye maswala kama imani za kishirikina na matamanio ya mwili yaliyomshinda mtekelezaj wa kosa hilo.

Mwalim sawa kuna mambo ya hasira lakini sio kiasi cha kumpiga mtoto ngumi ya mbavu mpaka kumjeruhi bandana nakataa
Walimu wengi Wana matatizo ya afya ya akili, stress kibao tukio kama hilo sio la kwanza kutokea, Kuna Ile ilitokea Kagera kama sijasahau walimu walipiga mwanafunzi mpaka wakaua na kesi ilienda mahakamani na wakahukumiwa kifungo gerezani.
 
Ww jamaa kama ni Dr basi unajidhalilisha humu ndani, yaani umen'gan'gania Spontaneous rupture of spleen tu, ushaambiwa dogo alichapwa fimbo kwann usianzie hapo kwanza? Hiyo sababu unayotuletea humu ndani inge make sense kama huyo marehemu asingekuwa amekumbana na tukio lolote.
Mimi nipo kusema ukweli na sio kufurahisha watu. Narudia tena kwa dalili anazoeleza mama wa mtoto zinaendana na ugonjwa husika uliomuua mtoto kulingana na ripoti ya Madaktari bingwa na wabobezi kutoka KCMC. Anything against that ni uongo unless proven otherwise.

Labda nikuulize tu km wewe sio hii Gen Z, haujawahi kuchapwa na Mwalimu? Je, ulikufa? Kwa sisi tuliosoma zamani kidogo tumechapwa sana na tumeshuhudia wenzetu wakichapwa na adhabu za kung'oa visiki n.k na hatukuwahi kushuhudia mwanafunzi kafa

Tatizo la hiki kizazi cha single mothers ni malezi mabovu yanayotengeneza kizazi cha hovyo kwa kuleta hasira za kutelekezewa watoto kila mahali hata shuleni.
 
Wewe hujaguswa na msiba huu, na umeshahitimisha kuwa marehemu alipigana na wenzake au alipata ajali, mimi wakati nasoma tena nikiwa mdogo kabisa kuna mwalimu wa hesabu liyeitwa Marandu,aliwahi kuniambia kabisa kuwa ananichukia bila sababu yoyote, nilipomweleza mzazi wangu akanihamisha shule fasta, mwalimu kama huyo angeweza kuniua bila sababu yoyote!!
Sijasema direct kwamba alipata ajali nimesema pengine mtoto alipata ajali.

Hafu mwalim kukwambia anakuchukia ni vzr kwasababu alieleza na kuzionesha hisia zake waz waz kuliko angezificha halafu akaishia kukuoneshwa kwa vtendo
 
Kama ripoti ya Daktari inaonesha mwanao alikuwa na Kansa ya Damu ( dalili zote unazoelezea zinaendana) kwanini unalazimisha ionekane Mwalimu ndio kamuua mwanao?

Kuchapwa viboko kungekuwa kunaua tungeshakufa wengi sana tuliosoma zamani. Mnataka kutengeneza kizazi gani cha watoto wasiochapwa?

Kwanini mnataka kuleta malezi ya Kizungu watoto wa Kitanzania wenye mazingira na tamaduni tofauti katika malezi na makuzi?

All in all may His Soul Rest in Eternal Peace. Amen. Kuendeleza hii kesi ni kumkosea Marehemu kwa kulazimisha kitu kisichokuwepo.
Kansa inaweka na alama za kupigwa mwilini, na mtoto kama kaeleza alipigwa tumboni? Atakuwa amewahiwa hospital dr akapewa cha kupewa akaandika hivo kwenye report, hayo mambo yapo hata postmortem zinapindishwa saana hasa upande wa mashtaka wakiwa hawana kitu
 
Back
Top Bottom