DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Unamfundisha ujinga? Kumuachia Mungu ndiyo nini?
Watu sijui hawana watoto? Yaani wanaropoka tu. Umekaa nyumbani unamsubiri mtoto anakuja na majeraha ya fimbo za mwalimu unaenda shule kuuliza unafichwa fichwa baada ya siku mbili mtoto anafariki mtu anakuambia umwachie MUNGU?
 
Tunaposhindwa kushughulikia Maswala ya Unyanyasaji Kwenye Jamii tunatengeneza Hasira za Visasi..

Naona kabisa kama huyu mama hatapatiwa haki tunatengeneza long-term resentment stemming from prolonged abuse na inaweza kupelekea revenge, Yenye kisasi kikubwa Sana sio tu Cha ajabu!

ningemuomba Dkt Gwajima Dkt. Gwajima D Atume Busara zake Kutatua hili swala..

Tunatengeneza Raia Wakatili kwa kuyapuuza machungu yao..

Kukaa na machungu Mda mrefu na kuhisi Serkali haimsikilizi kuna Pelekea huyu mama Kuwa vindictiveness...

Na anaweza kufanya Chochote kwa sababu anahisi Shule yote imemkosea kumficha mhalifu na kwa kuwa hana cha kupoteza Huenda anaweza akasukumwa na Roho ya Hasira na kisasi akachoma hata shule..

Je tumewahi kujiuliza madhara ya kupuuza Hasira ya kutokukutiliwa maanani na kubezwa?

Ni maumivu makali hasa unapojua umekosewa lakini wakosaji wanatetewa..

Ukiwa kama Mmoja ya Mawaziri Nao waamini sana nakuomba hili swala kishughulikie hao walimu wanao uwezo wa kufanya chochote baada ya kuona Tayari wamekwisharibu "Zingatia hilo" wanao uwezo wa kujitetea je umejiuliza Huyo mama yeye atatetewa na nani??

Kuhusu Mama namshauri kwa Busara kabisa Kama uchunguzi umeshafanyika baada ya yeye kutoa Taarifa polisi..

Bhasi ni vyema akazike mwili Huku akisubiri Serkali ifanye majukumu yake..

NB:
"Vindictive personae ultio crudelior est quam omnes, ob inimicitias quas tenet."


"The VENGEANCE of the Vindictive person, Is the cruelest Revenge Than all, Cuz of the grudges it holds..."

CC: Dkt. Gwajima D
 
Inatokea gafla au inaanza taratibu?
Inaweza kutokea ghafla au taratibu kama miongoni mwa dalili za ugonjwa husika. Na yote hiyo hutokana na kupungua sana kwa chembe sahani hivyo kupelekea kuvuja kwa damu chini ya ngozi na misuli ( severe thrombocytopenia)
 
Kama ripoti ya Daktari inaonesha mwanao alikuwa na Kansa ya Damu ( dalili zote unazoelezea zinaendana) kwanini unalazimisha ionekane Mwalimu ndio kamuua mwanao?

Kuchapwa viboko kungekuwa kunaua tungeshakufa wengi sana tuliosoma zamani. Mnataka kutengeneza kizazi gani cha watoto wasiochapwa?

Kwanini mnataka kuleta malezi ya Kizungu watoto wa Kitanzania wenye mazingira na tamaduni tofauti katika malezi na makuzi?

All in all may His Soul Rest in Eternal Peace. Amen. Kuendeleza hii kesi ni kumkosea Marehemu kwa kulazimisha kitu kisichokuwepo.
Aisee wewe ni mpumbavu wa siku ya leo. Kwa sababu wewe ulichapwa kama punda na hukufa basi viboko haviui? Unatania au umelewa? Ni mara yako ya kwanza kusikia mtu kafa kwa viboko, tena kiboko kimoja tu? Ficha ununda wako.
 
Siku aliyorudi na majeraha ilitakiwa ukachukue pf 3 polisi daktari aliesema bandama imepasuka angeijaza na ingekua ushahidi wa awali alafu ndo ungeendelea na mambo mengine sahivi baada ya kufariki dokta akifanya Postmortem akisema kafa kwa kansa ya damu hiyo ndo ripoti itakayokubalika.
 
Hospitali zetu nazo, mtoto akifikishwa hospitali na majeraha yanayoashiria unyanyasaji wa aina yoyote wanapaswa kuwaita polisi mara moja.
Hapa watetezi wa huyo mwalimu hawapahoji, wanakomaa na ripoti ya mwisho ya kansa kama chanzo cha kifo.
 
Mimi naamini zaidi maelezo ya Daktari nikilinganisha na dalili za ugonjwa naona kabisa vinashabihiana
Kwa hiyo hilo suala la majeraha na madai ya mtoto kupigwa kikatili unayafuta sababu kansa huwa inapelekea kuvuja damu?

Unayafuta bila kumsikia mtuhumiwa? Unayafuta bila kujua mtoto alipokelewa na daktari akiwa kweli na majeraha au la? Unayafuta bila kufikiri iwapo mtoto alikuwa na majeraha kwanini daktari hakuhusisha polisi?

Wewe ndo huyo mwalimu mkuu nini?
 
Siku aliyorudi na majeraha ilitakiwa ukachukue pf 3 polisi daktari aliesema bandama imepasuka angeijaza na ingekua ushahidi wa awali alafu ndo ungeendelea na mambo mengine sahivi baada ya kufariki dokta akifanya Postmortem akisema kafa kwa kansa ya damu hiyo ndo ripoti itakayokubalika.
Huyo Daktari wa mwanzo atakuwa ni CO yeye alivyoona bandama ina shida na michirizi ya kuvilia damu basi akajua ni kipigo. Hajui km Kansa ya damu husababisha vyote hivyo.

Huyo ndio chanzo cha sakata lote hili kwa sababu ya ukihiyo wake. Ndio maana nchi zilizoendelea hakuna kitu kinaitwa CO.

Tatizo la nchi hii ni kuruhusu afya zetu zichezewe hovyo kuanzia na hawa waganga matapeli wa tiba mbadala, wauza maduka ya dawa na hawa maCO.
 
Mmh ! Uthibitisho wa hyo ngumi alopgwa dogo ndo italeta uzito kwen jambo lako vingnevyo..Pole kwa msiba
Hatua ya kwanza ya uthibitisho ni huyo mwalimu kusema kilichotokea. Kama suala ni maisha yake kuwa hatarini utlist angekuwa kashikiliwa na polisi ingeeleweka. Tatizo hapa ni huyo mwalimu anayetuhumiwa anafichwa.
 
Aisee wewe ni mpumbavu wa siku ya leo. Kwa sababu wewe ulichapwa kama punda na hukufa basi viboko haviui? Unatania au umelewa? Ni mara yako ya kwanza kusikia mtu kafa kwa viboko, tena kiboko kimoja tu? Ficha ununda wako.
Wewe pia ficha ujinga wako uniambie ni nani alikufa darasani kwako kwa kuchapwa finbo zaidi ya matukio ya kusimuliwa?
 
Kwa hiyo hilo suala la majeraha na madai ya mtoto kupigwa kikatili unayafuta sababu kansa huwa inapelekea kuvuja damu?

Unayafuta bila kumsikia mtuhumiwa? Unayafuta bila kujua mtoto alipokelewa na daktari akiwa kweli na majeraha au la? Unayafuta bila kufikiri iwapo mtoto alikuwa na majeraha kwanini daktari hakuhusisha polisi?

Wewe ndo huyo mwalimu mkuu nini?
Nayafuta kulingana na ripoti ya Madaktari bingwa wabobezi kutoka KCMC waliothibutisha kitaalam kuwa mtoto kafa kutokana na cancer ya damu. Una lolote la kitaalam kupingana na ripoti ya Madaktari?
 
Back
Top Bottom