DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Huyo Daktari wa mwanzo atakuwa ni CO yeye alivyoona bandama ina shida na michirizi ya kuvilia damu basi akajua ni kipigo. Hajui km Kansa ya damu husababisha vyote hivyo.

Huyo ndio chanzo cha sakata lote hili kwa sababu ya ukihiyo wake. Ndio maana nchi zilizoendelea hakuna kitu kinaitwa CO.

Tatizo la nchi hii ni kuruhusu afya zetu zichezewe hovyo kuanzia na hawa waganga matapeli wa tiba mbadala, wauza maduka ya dawa na hawa maCO.
Hizi ni assumption zinaweza kuwa sawa au zisiwe sawa. Wewe umehitimisha kwa assumptions. Hali ya huyo mtoto hukuiona.

Ulitakiwa kuhoji iwapo kweli mtoto alipigwa na kama alipigwa kwa kiwango gani na majibu anayo mhusika anayetuhumiwa ila uhoji hilo. Hili si tukio la kwanza la mwalimu kuua mtoto.
 
Inaweza kutokea ghafla au taratibu kama miongoni mwa dalili za ugonjwa husika. Na yote hiyo hutokana na kupungua sana kwa chembe sahani hivyo kupelekea kuvuja kwa damu chini ya ngozi na misuli ( severe thrombocytopenia)
Wewe umepewa mlungula upindishe maelezo mimba yenyew haitokei gafla iwe michirizi ndo itoke gafla sababu ya saratani
 
Nayafuta kulingana na ripoti ya Madaktari bingwa wabobezi kutoka KCMC waliothibutisha kitaalam kuwa mtoto kafa kutokana na cancer ya damu. Una lolote la kitaalam kupingana na ripoti ya Madaktari?
Unajua una utoto mwingi? Mtoto mwenye kansa hawezi kupigwa kikatili? Tuseme tu alikuwa nayo hiyo kansa, inazuia vipi kupigwa? Hapa tunachojadili ni nini? Madai ya mtoto kupigwa. Umeshathibitisha kuwa mtoto hakupigwa kwa kiwango ambacho si sahihi?

Tena kupiga mtoto mgonjwa ilitakiwa ndo uwe aggressive zaidi kuwa kama alikuwa na kansa walimu hawakujua hali yake? Mzazi hakujua hali ya mtoto? Hiyo kansa ilijificha mpaka siku ya kipigo ndo iibuke kumuua? Ulipaswa kujiuliza maswali kabla ya kumtetea huyo mwalimu kuwa hausiki kabisa.

Hakuna mtu anataka mwalimu ahukumiwe bila makosa, ila tukio limetokea, kuna tuhuma, huwezi zipuuza tu bila kusikia upande wa mtuhumiwa.
 
U
Wewe umepewa mlungula upindishe maelezo mimba yenyew haitokei gafla iwe michirizi ndo itoke gafla sababu ya saratani
Unapingana na uhalisia? Unafikir yeye ndio wa kwanza kupata hiyo michirizi ya kuvilia damu kutokana na cancer ya damu?
 
Wewe pia ficha ujinga wako uniambie ni nani alikufa darasani kwako kwa kuchapwa finbo zaidi ya matukio ya kusimuliwa?
Kumbe nalumbana na Idiot aliyeshindakana? Mpaka awe alikufa darasani kwangu? Mimi nimeshuhudia kwa jirani yangu na siyo hilo tu kuna cases nyingi watu wamefungwa kwa sababu ya kuua kwa fimbo.
 
Naitwa Janeth Shayo, mkazi wa Uru, Moshi. Naomba unisaidie kupaza sauti mwanangu Jonathan Makanyaga (07) mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Mrupanga, ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inataka kupindishwa.

Tar.28/02/2024 mwanangu alienda shuleni akiwa mzima. Alipofika aliadhibiwa kwa kuchelewa "namba". Alipoingia darasani alianza kutokwa damu puani na mdomoni. Akarudishwa nyumbani. Nilipomkagua nikamkuta na majeraha yaliyovilia damu mgongoni, kwenye mbavu na mguuni.

Kesho yake nikaenda nae shuleni kutaka kuoneshwa mwalimu aliyemfanyia ukatili mwanangu. Lakini Mwalimu mkuu akaomba nibaki nje. Akaingia na mwanangu ofisi ya walimu na kumtaka amtambue Mwalimu aliyemuadhibu. Mwanangu akamtanbua. Mwalimu Mkuu akaniambia wameshamfahamu ni mwalimu wa "Field" hivyo atazungumza nae.

Wakanipa 20,000/= za matibabu. Nikampeleka mwanangu zahanati. Kesho yake akazidi kutoka damu, na kulalamikia maumivu sehemu za mbavu. Nikampeleka hospitali ya masista. Daktari akaniambia bandama imejeruhika ndio sababu ya kutoka damu mdomoni. Mtoto alidai pamoja na viboko alivyochapwa, Mwalimu pia alimpiga ngumi tumboni. Huenda ndiyo iliyopasua bandama.

Hali yake ilizidi kuwa mbaya tukapewa rufaa kwenda KCMC. Akatakiwa kufanyiwa upasuaji. Gharama 350,000/= lakini sikuwa nayo. Nikapiga simu shuleni wakasema tuombe afanyiwe halafu watalipa baadae. Hata hivyo kabla hajafanyiwa hali yake ikazidi kuzorota, akashindwa kupumua, akawekwa kwenye Oxygen. Akashindwa kula, akawekewa mpira wa chakula. Baada ya siku chache akafariki 😭.

Lakini ripoti ya hospitali inasema mwanangu amekufa kwa kansa ya damu. Kansa gani ya damu inayomuua mtoto kwa wiki mbili? Na kwanini hiyo kansa itokee baada ya kuadhibiwa shuleni? Kwanini Mwalimu aliyemuadhibu mwanangu anafichwa, na sipewi haki ya kumfahamu?

Nalazimishwa nichukue maiti nikazike lakini nimekataa. Nataka uchunguzi huru. Nimeenda dawati la jinsia kulalamika nikapuuzwa. Nimepiga simu kwa Waziri Dkt. Gwajima D akanipa namba ya mtu wa kunisaidia. Nilipopiga kumbe ni yuleyule Mkuu wa dawati la jinsia aliyenipuuza. Nikamrudia Gwajima akasema niwasiliane nae huyohuyo. Nimekosa pa kulilia haki ya mwanangu Jonathan

Kama Dkt. Gwajima D anaona si jambo linalomhusu moja kwa moja basi hii isambazwe na kule X mpaka imfikie mama Samia, kweli ata hili lishindikane kupatiwa haki ?
 
U

Unapingana na uhalisia? Unafikir yeye ndio wa kwanza kupata hiyo michirizi ya kuvilia damu kutokana na cancer ya damu?
Uhasilia gani? Hata hao ma dr wanaweza kuwa walizembea kwenye kuwahi kumtibu na sasa hivi wanasingizia cancer. natakiwa uchunguzi huru ufanywe.
 
Naitwa Janeth Shayo, mkazi wa Uru, Moshi. Naomba unisaidie kupaza sauti mwanangu Jonathan Makanyaga (07) mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Mrupanga, ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inataka kupindishwa.

Tar.28/02/2024 mwanangu alienda shuleni akiwa mzima. Alipofika aliadhibiwa kwa kuchelewa "namba". Alipoingia darasani alianza kutokwa damu puani na mdomoni. Akarudishwa nyumbani. Nilipomkagua nikamkuta na majeraha yaliyovilia damu mgongoni, kwenye mbavu na mguuni.

Kesho yake nikaenda nae shuleni kutaka kuoneshwa mwalimu aliyemfanyia ukatili mwanangu. Lakini Mwalimu mkuu akaomba nibaki nje. Akaingia na mwanangu ofisi ya walimu na kumtaka amtambue Mwalimu aliyemuadhibu. Mwanangu akamtanbua. Mwalimu Mkuu akaniambia wameshamfahamu ni mwalimu wa "Field" hivyo atazungumza nae.

Wakanipa 20,000/= za matibabu. Nikampeleka mwanangu zahanati. Kesho yake akazidi kutoka damu, na kulalamikia maumivu sehemu za mbavu. Nikampeleka hospitali ya masista. Daktari akaniambia bandama imejeruhika ndio sababu ya kutoka damu mdomoni. Mtoto alidai pamoja na viboko alivyochapwa, Mwalimu pia alimpiga ngumi tumboni. Huenda ndiyo iliyopasua bandama.

Hali yake ilizidi kuwa mbaya tukapewa rufaa kwenda KCMC. Akatakiwa kufanyiwa upasuaji. Gharama 350,000/= lakini sikuwa nayo. Nikapiga simu shuleni wakasema tuombe afanyiwe halafu watalipa baadae. Hata hivyo kabla hajafanyiwa hali yake ikazidi kuzorota, akashindwa kupumua, akawekwa kwenye Oxygen. Akashindwa kula, akawekewa mpira wa chakula. Baada ya siku chache akafariki 😭.

Lakini ripoti ya hospitali inasema mwanangu amekufa kwa kansa ya damu. Kansa gani ya damu inayomuua mtoto kwa wiki mbili? Na kwanini hiyo kansa itokee baada ya kuadhibiwa shuleni? Kwanini Mwalimu aliyemuadhibu mwanangu anafichwa, na sipewi haki ya kumfahamu?

Nalazimishwa nichukue maiti nikazike lakini nimekataa. Nataka uchunguzi huru. Nimeenda dawati la jinsia kulalamika nikapuuzwa. Nimepiga simu kwa Waziri Dkt. Gwajima D akanipa namba ya mtu wa kunisaidia. Nilipopiga kumbe ni yuleyule Mkuu wa dawati la jinsia aliyenipuuza. Nikamrudia Gwajima akasema niwasiliane nae huyohuyo. Nimekosa pa kulilia haki ya mwanangu Jonathan
Pole sana kwa msiba mkubwa kama huu mungu akujalie subila kwenye kipindi kigumu kama hiki

Maswali machache ambayo bado yanazunguka kichwani kwangu muda huu
1. Report ya daktari inatoa mawazo mapya ambayo kimsingi mtoto kafariki kwa kansa ya damu ( leukemia) au mtoto aikua na hemophilia Ndio maana damu ikaendelea kutoka mpaka kuperekea kifo na sio mpasuko wa bandama au any vital organs

2. Maelezo ya mtoto wa huo umri mdogo kupigwa ngumi na MWALIMU Tena Kwa kosa la kuchelewa namba haiingi akili

3. Kutoa report kituo chochote cha polisi ambacho kipo karibu bado inaleta mkanganyiko

4. Ni kwa nini dawati ambalo linashughulikia hii kesi limetupilia mbali hii kesi from beginning?

Kuna muda tusiukumu kwa hisia TU kwamba MWALIMU Ndio kasababisha kifo inawezekana mtoto alikua diagnosed with leukemia au hemophilia ila MWALIMU amejikuta katikati na jumba bovu limemuangukia
 
Natarajia kabla ya saa moja jioni Waziri Dkt. Gwajima D atakuwa amejibu hili swala serious sana maana hili ni moja ya kipimo cha utendaji kazi wake ni Waziri ambaye kidogo hapa Jf watu wana imani naye na yuko active lakini kuna watendaje wake kama wanataka kumkwamisha na kumchafua….!

Naona umeonekana jana saa moja kasoro jioni …tunasubiri majibu yako bila shaka una yaandaa
 
Attachments

  • IMG_2077.jpeg
    IMG_2077.jpeg
    141.6 KB · Views: 3
Huyo Daktari wa mwanzo atakuwa ni CO yeye alivyoona bandama ina shida na michirizi ya kuvilia damu basi akajua ni kipigo. Hajui km Kansa ya damu husababisha vyote hivyo.

Huyo ndio chanzo cha sakata lote hili kwa sababu ya ukihiyo wake. Ndio maana nchi zilizoendelea hakuna kitu kinaitwa CO.

Tatizo la nchi hii ni kuruhusu afya zetu zichezewe hovyo kuanzia na hawa waganga matapeli wa tiba mbadala, wauza maduka ya dawa na hawa maCO.
Bila shaka wewe ni mojawapo ya wale MD wasiojitambua, unamponda CO ambaye Yuko kijijini anatibu ndugu zako na wanapona vizuri tu ila wewe ukipelekwa hospital za Tamisemi unakimbia kwahiyo unataka huko nani akafanye kazi?

Uko kituo Cha afya umeletewa mgonjwa anatokwa damu puani, mdomoni, amevilia damu, amevimba wengu na dalili zote hizo zimeanza punde tu baada ya kushambuliwa kwahiyo utasema mgonjwa ana kansa sio?
 
Bila shaka wewe ni mojawapo ya wale MD wasiojitambua, unamponda CO ambaye Yuko kijijini anatibu ndugu zako na wanapona vizuri tu ila wewe ukipelekwa hospital za Tamisemi unakimbia kwahiyo unataka huko nani akafanye kazi?

Uko kituoni Cha afya umeletewa mgonjwa anatokwa damu puani, mdomoni, amevilia damu, amevimba wengu na dalili zote hizo zimeanza punde tu baada ya kushambuliwa kwahiyo utasema mgonjwa ana kansa sio?
Anachosema huyu ni kuwa marehemu ana kansa, hata kama amepigwa ni sawa tu sababu ana kansa. Huyo aliyempiga asisumbuliwe kuhojiwa iwapo alimpiga kweli bila kujali kwa kiwango gani, mgonjwa kafa na kansa nendeni mkamzike.
 
pole sana asee , lkn usiwekeze akili kwa mwl tu , watz hatupend kupima afya zetu , mwl hata awe mkorofi vp haez mpiga ngumi mtoto wa drs la 1 , kwa maelezo yako umeelezea rufaa tatu hapo , ni ngumu kwa rufaa hizi tatu mwl mkuu wa shule ya msingi kujitoa kumlinda huyo mwl wa field , Ziamini report za madaktari , mtoto anauma ila mwisho wa siku kubali tu lkn hii iwe fundisho kwa walimu pia EPUKA KUPIGA MTOTO WA MTOTO ANAEZA KUWA MAREHEMU ANAYETEMBEA HLF MZIGO UKAKUANGUKIA , MIMI NI DAKTARI NA NMEONA WATU WENGI WANAOAMINI WAZIMA KUMBE WANATEMBEA NA MAGONJWA SUGU

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
 
Duuu mkuu pole sana bila shaka Dkt. Gwajima D atakuja hapa kutoa majibu …aisee inauma sana sana yani mwalimu anampiga ngumi mtoto hapa hii haikubalika kabisa kabisa!

Nafikiri kwenye hili Mwl Mkuu anapaswa kuchukuliwa hatua kabisa na huyo mwalimu anapaswa kufikishwa kwenye vyombo vya kisheria hii ni hatari!

Halafu Dkt. Gwajima D unapaswa kutwambia huyo mtumishi wako wa dawati la jinsia anaye lalamikiwa kupuuza watu unapaswa kumuondoa pale hapamfai kabisa!
soma vzr maelezo vzr ya mhanga , utaelewa report ya daktari ndo inamnyima haki huyo mwl mkuu au mhusika wa dawati , TUPENDE KUPIMA AFYA ZETU

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom