DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Rais Samia aliongelea hili jambo juzi ila naona mawazir wake washamsoma na kumzoea wanaona anaongea tu hakuna hatua kwahiyo linaingilia upande mmoja wa sikio linatokea upande wa pili, huyo Dorothy Gwajima ni msanii tu anawahadaa watu kwa kujifanya anatoa mawasiliano yake mtandaoni ili Hali hakuna anachokifanya kuwasaidia wahusika maana kama kweli angekuwa anawasaidia angekuwa anatoa feedback ila hakuna ni kutafuta kiki tu
Kesi hii ni ya kuuwa ila anapiga chenga
Na hapa hawezi kujitokeza
 
Hapa tumepeta maelezo ya mzaz tayr ushachagua upande, nikulize maelezo ya mwalim umeyapata?
Wapi nimechagua upande? Ninachosisitiza ni huyo mwalimu apatikane. Kwanini anafichwa?
Mzaz n mwanadam kam tulivo wengine anaweza kudanganya pia ndomana hata mahakamani pande mbili zote husikilizwa na ushahidi wao huzingatiwa
Wewe kwanini unaamini kuwa anadanganya? Umeshasikiliza upande wa mwalimu?
 
Wewe Hakimu tuambie namna gani fimbo za Mwalimu zimemuua huyo mtoto na kumletea cancer ya damu?
Ni kwanini mwalimu hakuletwa hadharani na mtoto aeleze alichapwa vipi, na kwanini mtoto aseme alipigwa ngumi tumboni? Mtoto wa miaka7 haezi tunga story hata umfundisheje yeye atanyoosha kama ilivokuwa, nikuulize kwanza una mtoto?
 
Mimi nipo kusema ukweli na sio kufurahisha watu. Narudia tena kwa dalili anazoeleza mama wa mtoto zinaendana na ugonjwa husika uliomuua mtoto kulingana na ripoti ya Madaktari bingwa na wabobezi kutoka KCMC. Anything against that ni uongo unless proven otherwise.

Labda nikuulize tu km wewe sio hii Gen Z, haujawahi kuchapwa na Mwalimu? Je, ulikufa? Kwa sisi tuliosoma zamani kidogo tumechapwa sana na tumeshuhudia wenzetu wakichapwa na adhabu za kung'oa visiki n.k na hatukuwahi kushuhudia mwanafunzi kafa

Tatizo la hiki kizazi cha single mothers ni malezi mabovu yanayotengeneza kizazi cha hovyo kwa kuleta hasira za kutelekezewa watoto kila mahali hata shuleni.
Naona umekariri dalili za cancer tu mambo mengine unajifanya kuyapa kisogo, fahamu kwamba hata head injury inaweza kupelekea damu kutoka mdomoni na puani pia, Wengu (spleen ) kupasuka kunawezwa kusababishwa na fimbo pia.
 
Hapa tumepeta maelezo ya mzaz tayr ushachagua upande, nikulize maelezo ya mwalim umeyapata?
Wapi nimechagua upande? Ninachosisitiza ni huyo mwalimu apatikane. Kwanini anafichwa?
Mzaz n mwanadam kam tulivo wengine anaweza kudanganya pia ndomana hata mahakamani pande mbili zote husikilizwa na ushahidi wao huzingatiwa
Wewe kwanini unaamini kuwa anadanganya? Umeshasikiliza upande wa mwalimu?
 
Kansa inaweka na alama za kupigwa mwilini, na mtoto kama kaeleza alipigwa tumboni? Atakuwa amewahiwa hospital dr akapewa cha kupewa akaandika hivo kwenye report, hayo mambo yapo hata postmortem zinapindishwa saana hasa upande wa mashtaka wakiwa hawana kitu
Unazijua petechiae, ecchymosis and purpura?
Ngoja nikusaidie picha
images (15).jpeg
images (16).jpeg
 
sasa na ww Dkt. Gwajima D uko hapa unajidai unafuatilia mambo kumbe hamna lolote kakurudia na kukuambia namba ulizompa ni mtu asiye weza msaidia tatizo lake bado unamkomalia awasiliane nae ni ili haki yake ipotee au ndio watu wa kumshika mkono kwenye swala lake wameisha? je angekua mtoto wa mkubwa mwenzenu danadana hizo zingetokea au iingekua simu moja tu..

mzazi anatamani haki itendeke hata kama haupo hapo unanusa harufu ya uonevu msaidieni kama hamuwezi muwekeni wazi watu tuhamie kwa sangoma tunyooshe mtu..

sijapenda kukuta nawe hujamsaidia dah....
 
Hivi unampigaje mtoto was miaka Saba kiasi hicho? Hawa waalimu ni next level mental cases aisee
 
Back
Top Bottom