DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Bila kuchangia kwa mihemko na bila kujaji kwa nini unapuuzwa ebu tuanzie hapa;
1) Ilikuwaje hizo hospitali zikubali kumtibu mtoto bila PF3 ya police wakati uliwaeleza na kuwaonesha makovu ya vipigo kutoka kwa mwalimu.
2) Kwa nini hujaenda police kutoa taarifa au kwa afisa elimu wake hata wa kata.
3) Mtoto wa darasa la kwanza ni mdogo sn iweje mwalimu afikie hatua ya kumpiga hovyo hovyo hivyo tena kwa sababu ya kuchelewa. Angekuwa mkubwa km sekondari tungesema kulikuwa na majibizano mwalimu akashikwa hasira akampiga hovyo. (NB: Vyovyote mwanafunzi atakavyojibu na kumuudhi Mwalimu, Mwalimu haruhusiwi kumuadhibu hovyo).
4) Unasema mkuu alikataa kukuonesha Mwalimu mhusika. Ulitaka kumuona ili iweje. Km ungemuona ndo angepona. Hapa ndo wazazi wengi wasio na upeo hukurupuka na kutanguliza hasira mbele maarifa kubaki nyuma. Muhimu ulitakiwa ufuate taratib za kisheria ili afahamike na kukamatwa. Na nikuhakikishie hata km angekamatwa iwapo usingekuwepo wakati wa ukamataji usingemuona hata ungelia machozi ya damu police hawawezi kukupa ruhusa ya kuonana na mbaya wako kwa wakati huo labda mkifika mahakamani. Hivyo hivyo Mwalimu mkuu siyo mjinga eti akuoneshe Mwalimu mhusika. Angejuaj lengo llako, je km ulitaka kumdhuru. Kamwe hilo haliwezi kutokea kwenye taasisi kienyeji hivyo.
5) Kwanini hutaki kuamini majibu ya daktari. Je kwanini tusiamini kuwa mtoto alikuwa mgonjwa kweli na wewe tatizo hilo ulikuwa unalifahamu Ila fimbo za Mwalimu zimekuwa sababu tu.
6) Je ni mwanao tu alipigwa hivyo? Km wengine nao waliadhibiwa lakini kwa utaratibu na kuathirika kwa nini awe mwanao tu. Km waliadhibiwa kwa pamoja umeshindwa kuuliza wenzake kilichoprlekea mwanao kupigwa kiasi cha kupasuka bandama.?
7) Unasema ulazamishwa kuzika mwanao. Nani anaekushinikiza kufanya hivyo wakati kwenye bandiko lako hakuna ulikotaja police kuhusika.

Mwisho: Nakupa Pole kwa yaliyokukuta na fuata taratib za kisheria kupata haki yako kuliko kuja humu kulia. Pili, ulitakiwa utaje shule aliyokuwa anasoma.

Kuna jambo nitaeleza hapa kwa ufupi ambalo liliwahi kumtokea Mwalimu flani baada ya kumuadhibu mwanafunzi wa sekondari viboko 2 mkononi tena mbele ya kaka yake waliekuwa darasa moja lakini baada ya muda mfupi alifariki. Lakini alipopewa mzazi taarifa huku mwalimu akitafuta kukimbia, baba wa marehem alisema huyo mwalimu hana hatia aachwe. It means kulikuwa na jambo la kifamilia nyuma ya pazia. Naskia takribani miaka 6 sasa huyo mwalimu yupo hapohapo na maisha yanaendelea.

Nimemaliza; BANDOKITITA

Ebu jifunze kitu hapa.
 
Ukakasi ni mkubwa kwanza kwa psychology haiingi MWALIMU kumchapa mtoto wa chekechea drs la 1&2 tena Kwa kosa la kuchelewa namba mm ntakua mtu wa mwisho kuamini hili

Pili kumpiga ngumi achilia mbali fimbo ambayo kiuharisia haifai kutumika kwa hayo madarasa kwa sababu Ndio anaanza kupenda shule fimbo itamfanya achukie shule Ndio maana Kama ni mfuatiliaji wa makuzi ya mtoto madarasa haya sehemu kubwa ya masomo yao ni kucheza

Hii kesi inamkanganyiko mwingi zaidi ya unavyo fikia Ndio maana from beginning dawati ambalo linashughulikia hii kesi limetupilia mbali hii shauri kuna some sort of ukweli umekosekana kwenye maelezo
Upo Bongo? Nikuambie. Mwaka 2018 nilikwenda shule fulani yenye chekechea kuulizia nafasi ili nimwandikishe mwanangu. Nilichokutana nacho kiliniacha mdomo wazi. Nilikuta mwalimu wa kike anampiga mtoto wa chekechea fimbo kama anaua nyoka. Take it from me. Nikaghairi na mama yake akampeleka shule nyingine. Nikawa nimesafiri kikazi. Nikiwa ugenini mke wangu akanijulisha kuwa mtoto analia sana kila asubuhi basi linapokuja kumchukua na hataki kwenda shule. Kisa? Kipigo. Ni mtoto wa chekechea ukumbuke. Nikamwambia afuatilie shuleni. Kwenda waalimu wakamwambia hii shule fimbo ni lazima. Hapa wazazi wanatusifu na wametupa ruhusu watoto wachapwe. Kama wewe hutaki wako achapwe, basi ondoka naye. Nilichoka kweli kweli. Nikamhamishia shule nzuri na nikatoa masharti kuwa sitaki apigwe. Wakanihakikishia kuwa wao hawapigi. Na kweli alisoma kwa amani. Tanzania yote hizi shule za Kayumba waalim wanaamini kuwa huwezi kumfundisha mtoto bila kiboko..... kuanzia chekechea.
 
Duuu mkuu pole sana bila shaka Dkt. Gwajima D atakuja hapa kutoa majibu …aisee inauma sana sana yani mwalimu anampiga ngumi mtoto hapa hii haikubalika kabisa kabisa!

Nafikiri kwenye hili Mwl Mkuu anapaswa kuchukuliwa hatua kabisa na huyo mwalimu anapaswa kufikishwa kwenye vyombo vya kisheria hii ni hatari!

Halafu Dkt. Gwajima D unapaswa kutwambia huyo mtumishi wako wa dawati la jinsia anaye lalamikiwa kupuuza watu unapaswa kumuondoa pale hapamfai kabisa!
Huyo dokta na huyo mkuu wa dawati wote sasa hivi wanafaa waachie ngazi maana hakuna walichokifanya.

Dkt. Gwajima D unatakaiwa kuwajibika kwa kuachia ngazi maana kama mtumishi wako hafanyi kile kinachotakiwa, hata wewe bosi wake utakuwa ni sehemu yake. Hapo ulipo upo kwa kodi za wananchi na ushukuru kuwa tanzania hakuna utawala wa sheria maana kibarua, na ndani kungekuhusu katika nchi za wenye akili
 
Hapa ni shutuma za kutengenezwa kwa makusudi. Kwanza, sijawahi ongea naye, mawasiliano yangu ni sms , kwenye ukurasa wake hakuna maneno aina hiyo, naye anajua kuwa, watuhumiwa 5 wako ndani. Na baada ya kumpigia kuongea naye imekuwaje, naye anashangaa, nimeomba simu aliyopiga au kupigiwa anipe, tangu asubuhi hajanipa. Humu duniani, tuvumiliane tu...View attachment 2935524View attachment 2935525

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Haya Sasa.
 
Kesi kama hii imkute Maghufuri kwenye Ziara zake...! Siku hiyo hiyo kimeeleweka...!

Lakini Viongozi wetu hawa......!!
 
Ndio haya aliyoyasema juzi Rais Samia yaani Kuna watu hawawajibiki kabisa mpaka wawajibishwe, huyo Wazir Gwajima mwenyewe Dada wa watu anasema amempigia simu mara mbili anamkazania arudi dawati la jinsia ambako wamempuuza sasa sijui wanataka mpaka Makonda apite ndio awasikilize watu wa namna hiyo?
Mm nahisi wakat mwingine huyu wazir Huwa anatafuta kiki tu aonekane ame respond kwa haraka mtandaoni ili Hali hatupati feedback kuhusu nini amemsaidia mlengwa
Vyote hivyo ni uongo. Kwa kuwa mm huwa siongei na simu daima, mm natumia sms tu. Muulize alimpigia nani Ili labda tukaombe kumbukumbu za sauti na ikionekana siyo mm iweje? Maana nimemuomba namba husika tangu asubuhi sijapewa. Ila ukweli ni kwamba, watuhumiwa wako ndani na yy amekiri anajua, na ameshangaa haya maneno yametoka wapi.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Dkt. Gwajima D huwa unakuja humu na mbwembwe kumbe hopeless kabisa. Mtu anakuletea taarifa unamrudisha kulekule alikopuuzwa badala ya kutoa maelekezo yenye msaada. CCM mna shida sana, mnataka mpaka atafutwe Rais?
 
Rais Samia aliongelea hili jambo juzi ila naona mawazir wake washamsoma na kumzoea wanaona anaongea tu hakuna hatua kwahiyo linaingilia upande mmoja wa sikio linatokea upande wa pili, huyo Dorothy Gwajima ni msanii tu anawahadaa watu kwa kujifanya anatoa mawasiliano yake mtandaoni ili Hali hakuna anachokifanya kuwasaidia wahusika maana kama kweli angekuwa anawasaidia angekuwa anatoa feedback ila hakuna ni kutafuta kiki tu
Kwanza tuanze na taarifa hiyo kuwa ni siyo sahihi kwani mm siwasiliani kwa kuongea Bali kwa kuandika sms tu. Simu za kuongea ziko call center. Labda kama yy kapiga hizo akajibiwa hivyo, basi aweke rekodi sahihi.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Inasikitisha Sana yaani hadi Gwajima naye anatoa maagizo badala ya kufatilia yeye kama yeye maana case imefika kwake.
Kifupi sijaongea naye naye anashangaa. Nisaidie kumuuliza ameongea na nani maana mm nasubiri hiyo namba tangu asubuhi. Ukweli uko kwenye tamko la Polisi kuwa watuhumiwa wako ndani.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Vyote hivyo ni uongo. Kwa kuwa mm huwa siongei na simu daima, mm natumia sms tu. Muulize alimpigia nani Ili labda tukaombe kumbukumbu za sauti na ikionekana siyo mm iweje? Maana nimemuomba namba husika tangu asubuhi sijapewa. Ila ukweli ni kwamba, watuhumiwa wako ndani na yy amekiri anajua, na ameshangaa haya maneno yametoka wapi.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Hayo yote hayasaidii cha msingi umepata taarifa fuatilia haki itendeke. Lakini tubaomba mbadilike mawaziri na watendaji wa umma, wengi tunapoteza imani na ninyi. Hata Makonda kawasema wazi kaenda mbali kaigusa mpaka mahakama
 
Ukweli huo hapo kwenye attachment hizo sn 3. Mengine kuhusu kuongea na mm na simu, siyo kweli. Mm natumia sms.
IMG_20240315_140850_094.jpg
IMG_20240315_140850_164.jpg

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Rais Samia aliongelea hili jambo juzi ila naona mawazir wake washamsoma na kumzoea wanaona anaongea tu hakuna hatua kwahiyo linaingilia upande mmoja wa sikio linatokea upande wa pili, huyo Dorothy Gwajima ni msanii tu anawahadaa watu kwa kujifanya anatoa mawasiliano yake mtandaoni ili Hali hakuna anachokifanya kuwasaidia wahusika maana kama kweli angekuwa anawasaidia angekuwa anatoa feedback ila hakuna ni kutafuta kiki tu
Sio Kila kitu lazima azungumze KunA mambo mtu anayafanyia kazi kimya kimya na matokeo una yaona. Tulimlalamikia hapa kuhusu watu kufanyiwa vitendo vya kikatili kwenye fukwe za bahari. Lile swala alilifanyia kazi mguu kwa mguu Mimi mwenyewe nilimuona kwenye Moja ya fukwe pale coco beach ya msasani. Na hivi ninacho zungumzia maeneo hayo Hali ni shwali.

Siwezi kukupinga ila ni vyema uka ainisha ambalo hajalifanyia kazi. Sio lazima mtu aite vyombo vya habari Ili uone amefanyia kazi changamoto...!​
 
Dkt. Gwajima D huwa unakuja humu na mbwembwe kumbe hopeless kabisa. Mtu anakuletea taarifa unamrudisha kulekule alikopuuzwa badala ya kutoa maelekezo yenye msaada. CCM mna shida sana, mnataka mpaka atafutwe Rais?
Sijui kwa mbwembwe mm hata siku moja, nakuja kwa data. Ni kwamba, mm huwa siwasiliani kwa kuongea siku zote nimetoa mwongozo wangu kuwa ni andika ujumbe.

Nimeongea naye kuomba hiyo namba aliyopiga au kupigiwa hajanipa tangu asubuhi. Kwa hiyo hoja ya kuwa tuliongea ni imeundwa maana mm muundo wangu wa mawasiliano ni SMS.

Lazima niyaweke haya wazi mm mwenyewe kwa kumbukumbu sahihi. Kazi tufanyeni kwa ushirikiano kwa kubalance stori. Siyo upande mmoja tu tayari habari hiyo. Hatufiki mbali wote. Ahsante Sana
IMG_20240315_140850_094.jpg
IMG_20240315_140850_164.jpg

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Sio Kila kitu lazima azungumze KunA mambo mtu anayafanyia kazi kimya kimya na matokeo una yaona. Tulimlalamikia hapa kuhusu watu kufanyiwa vitendo vya kikatili kwenye fukwe za bahari. Lile swala alilifanyia kazi mguu kwa mguu Mimi mwenyewe nilimuona kwenye Moja ya fukwe pale coco beach ya msasani. Na hivi ninacho zungumzia maeneo hayo Hali ni shwali.

Siwezi kukupinga ila ni vyema uka ainisha ambalo hajalifanyia kazi. Sio lazima mtu aite vyombo vya habari Ili uone amefanyia kazi changamoto...!​
Ndugu yangu, Dunia haijawahi kuwa na shukrani. Acha nifanye niwezavyo wakati wangu ukiisha watakuja wengine wafanye wawezavyo. Ila mambo haya ya kusingiziana nitayatolea ufafanuzi Mimi mwenyewe. Ili hizi kazi penye kweli pabaki kweli tukiwa wote hai.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Changamoto ni yy mwenyewe mama huyu nimemuomba hiyo namba ya simu ya mtu ambaye waliongea naye Ili nimhoji, naisubiri tangu asubuhi.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Ok Mkuu ngoja tumsubiri lakini hili jambo Mh Waziri unapaswa kulifatilia kwa ukaribu na kujua huyo aliyewasiliana nae ni nani na walio husika lazima wafikishwe kwenye vyombo vya usalama! Mtoto awezi kufa halafu tukanyamaza tuu na ikaisha tuu lazima kuna ukweli na kuna uongo maana najua kwa hali aliyo nayo ni kama kachanganyikiwa bila shaka wewe unaweza kufanya juhudi za kuhakikisha unapata mawasiliano yake na una ujua ukweli na ikiwezekana ukae uongee nae najua wajua fika uchungu wa kupoteza mtoto!
 
Back
Top Bottom