Wakuu Salaam,
Niende moja kwa moja kwenye mada, nina binti yangu wa miaka minne. Hivi majuzi amebainika kuwa na sickle cell kusema kweli nimechanganyikiwa sababu nasikia ni ugonjwa usio na tiba.
Naomba kujua yafuatayo;
1. Ni kweli ugonjwa huu hauna tiba?
2. Kama si kweli, tiba yake ni ipi?
3. Kama hauna tiba nini hatima yake?
Nimenyongea kwa kweli[emoji27]
Sent using
Jamii Forums mobile app
Habari!
Pole kwa yanayokuzunguka. Binafsi nayaona mambo mengi ambayo yanakuletea mtanzuko:
1: Hali isiyo na majibu halisi
2: Hali yenye majibu halisi
A: HALI ISIYO NA MAJIBU HALISI
Umeeleza vyema kuwa mkeo karudi na taarifa husika na wewe binafsi haujashuhudia.
Binafsi ninaona ni vyema kwanza kufanya ufatiliaji wa majibu husika ili uonane na mtaalamu wa afya na kupewa uhakika wa maelezo.
Hali uliyonayo na kwenda mbele zaidi ya kuhukumu inaweza kuleta pengo ndani ya familia na maisha kwa ujumla kwani:
1: Inajenga mtizamo wako ulivyo kwa mkeo pale kuna tatizo au kuhisiwa tatizo.
2: Inajenga mtizamo wako kwa mwanao pale kuna tatizo au kuhisiwa tatizo.
Vyema ujiridhishe, kwani kama ulivyooa mkeo bila kujua ana tatizo hilo, vivo hivyo unaweza usijitambue wewe au ndugu zako kuwa na urithi wa tatizo husika.
Pia, kwa kutokufahamu namna majibu yalivyopatikana inaleta pengo la taarifa, kwani hatujui huyu mtoto:
1: Ni mgonjwa kamili wa sickle cell/sickle cell disorder
2: Ana urithi tu wa sickle cell/traits
Ni vyema kujua aina ya kipimo na aina ya sickle cell.
Vipimo vyetu pia vina hali ya kukata rufaa, kwenda kipimo cha juu ili kutanabaisha haya.
Mfano: Kama umefanya sickling test basi ni vyema kwrnda kwenye electrophoresis.
B: HALI YENYE MAJIBU HALISI
Kama utapata maji halisi.
Tatizo hili halina tiba ya moja kwa moja kwa dawa bali kwa mtu kuhamishiwa ute ulioko kwenye mifupa ambao huusika kwenye kuzalisha damu. Na hii huitaji ndugu wa karibu ili kuwiana kwa karibu sana.
Wagonjwa wa sickle cell wamegawanyika kwenye makundi mawili.
1: Wagonjwa halisia/sickle cell disorder
2: Wagonjwa wenye urithi/trait
I: Wagonjwa halisia
Hawa huweza kutambuliwa kwa muonekano kwa wataalamu wa afya hasa wanapokuwa na umri mkubwa. Si rahisi kuwafahamu wakiwa wachanga, labda tu wanapooanza kuonyesha dalili zinazoendana na tatizo.
Hawa ni wale ambao ambao wanakuwa wamerithi matatizo ya sickle cell toka kwa wazazi wote wawili.
Kwa sasa, watoto hawa wanaishi vyema kutokana na uwepo wa kliniki na dawa za kwasaidia hivyo kupunguza shida zinazowapata na kukua vyema.
Hii inahusisha:
1: Kutambua aina ya ugonjwa
2: Kutoa ushauri kwa wazazi au walezi juu ya jinsi ya kuwaelewa, kuwalea vs kuwasaidia watu husika kwa tiba halisi na kwa yupi hasa kulingana na sayansi na teknolojia iliyopo.
3: Kupewa viinirishe saidizi kwa wahusika.
4: Kutoa dawa za kuwakinga na maambukizi.
5: Kutoa dawa za kuwapunguzia attack.
Wagonjwa hawa hawatakiwi kupata stress yoyote ikadumu ndani yao hasa:
1: Maambukizi ya ugonjwa
2: Kutokunywa maji ya kutosha
3: Kuwa sehemu yenye oksijeni kidogo
4: Nk.
II: Wagonjwa wenye urithi/traits
Hawa huishi maisha ya kawaida na huwezi kuwatambua kwa macho hata kwa wataalamu.
Wahusika huweza kupata msukosuko kidogo mara wapatapo stress ndani ya miili yao kama ilivyotajwa hapo juu lakini si kwa kiwango cha wale wagonjwa halisi. Pia hawahitaji kuwa kwenye kliniki za mara kwa mara.
NB: Hivyo, yote kwa yote ni haki ya mtoto husika kuendelea na maisha kama kawaida na hasa ukichukua hatua kulingana na hali halisi utakayokutana nayo kwa misingi tajwa hapo juu.