Mwanangu ana Sickle Cell, tiba yake nini?

Asante mkuu, karibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bone marrow transplant, Benjamin Mkapa Hospital wanafanya kwa watoto wenye sickle cell.
 
Sickle Cell hauna Tiba maalumu ya kupona, na hii nikutokana na Maumbile mabaya ya cell nyekundu za Damu, kupelekea kugota kwenye mishipa ya Damu na nyinginezo uwa mwili uamua kuzivunja vunja hili kuondoa zilizo haribika... Sasa kitendo cha mwili wenyewe kuendelea kuzivunja vunja seli nyekundu ambazo ni mbovu, hivyo upelekea mtu kuishiwa Damu, kwa sababu asilimia kubwa ya chembe nyekundu za Damu zinakuwa ni mbovu basi mtu huyu upungukiwa Damu.

Mara nyingi kwa watu wa Sickle cell unatakiwa uwe unampima malaria mara kwa mara ukiona anaugua na kupata homa, kwa sababu shida yake ya malaria ukiongezea sickle cell inaweza kufanya ugonjwa kuwa mkubwa zaidi kwa sababu pia Malaria uenda nayo kushambulia sell nyekundu za Damu.

Mara nyingi hawa watoto, utibiwa maumivu ya mara kwa mara kwa kupewa dawa za kupunguza maumivu, kupewa vidonge vya folic acid kwa ajili ya kuongezea damu, upewa antibiotic kama Pen V kwa ajili kuzuia pneumonia na magonjwa mengine ya bacteria, pia kama kaishiwa Damu zaidi basi uwa wanaenda kuwekewa Damu, na kama kapata shida ya upumuaji basi oxygen uwa anaekewa ikiambatana na matibabu mengine madogo madogo. Nyumbani ajitahidi kunywa maji hili kupunguza msongamano wa seli nyekundu zilizogota kwenye mzunguko wa damu basi.

Mwisho, ni vyema kufuata ushauri wa Daktari zaidi kuliko humu mitandaoni kwa maana Daktari ndio atakuwa anaona hali ya mgonjwa, na matabibu ya wagonjwa wa Sickle cell uwa hayafanani, atatibiwa kulingana na Crisis (Hatua ya ugonjwa) aliyonayo. Hivyo ni vyema kumuona mtaalamu hili hajui mtoto yupo kwenye crisis gani na apewe matabibu yapi na dose hipi.
 
Ndio maana wanashauri kabla ya ndoa ni vyema kupima afya kwanza kuona kama kuna uwezekano wa kupata mtoto mwenye sickle cell au ugonjwa kama ule aliompata mtoto wa masood kipanya...DNA unaweza Pima lakini unaweza kuta still bado ni mwanao 100 percent ..make sure usiongeze mtoto wa pili bila kujua mwingiliano wako na mkeo kama ndio ulisababisha.
 
Kama biology naikumbuka vizuri ni kwamba siyo baba na mama mna ugonjwa ila mna hivyo vinasaba hivyo miongoni mwa watoto wenu kuna atakayepata vinasaba na kuna atakayepata ugonjwa kabisa.

Huyu mwenye vinasaba akikutana na mwenye vinasaba mwenzake basi na wenyewe watapata watoto wagonjwa au wenye vinasaba.

Kuhusu tiba sina cha kusema.
 


Wanakuja wataalam, nilikuwa na rafiki yangu college na ugonjwa huu, zingatia sana maelekezo ya madaktari. Hakuwa mwangalifu alikuwa anateseka na kututesa sana, mbaya walokole hewa (Kuna walokole safi) wakawa wanafikiri ni mapepo.
 
Inasikitisha sana kwa kweli.
 
Maelezo yamejitosheleza bosi asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmh au ana baba mwingine isije kiwa si wako.


Nimewaza kwa sauti tu usije anza kuhukumu ila.
 
Messi alikuwa na tatizo la ukuaji...(udumavu)
 
Nenda Benjamin Mkapa hospital-Dodoma nasikia wameanza kutoa huduma hiyo kwa watoto wadogo.
Usikate tamaa wala kuchanganyikiwa.
 
Mungu ambaye ni muweza wa yote akutendee na kumtendea mwanao kwa kadiri ya mapenzi yako.Uwe na imani Mungu yupo.Amini kwamba hakuna jaribu lisilo na njia ya kupona
 
Mashaka Gani unapata jamaa angu
 
Ni ugonjwa wa kurithi/kuzaliwa nao, hakuna tiba; wapo jamaa zangu walizaliwa na hizo changamoto na kwa sasa wako kwenye miji yao na wameoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…