Mwanangu ana Sickle Cell, tiba yake nini?

Bro Pole sana.
Sina chochote cha kusema kuhusu huu ugonjwa ila kama mzazi naelewa unachopitia mana ni njia ambayo nimepita na ninaipita mpaka sasa

Mungu akupe nguvu. Imani yangu utapata suluhu tu siku moja
 
Pole brother, siku hizi damu za wazazi hupimwa ili kujua kama ni carriers kabla ya kuzaa ili wapate njia za kumlinda mtoto asipate shida hiyo.

Nakusihi, nenda hospital utapata muongozo sahihi zaidi.
 
Ni kweli, nimeshudia pia.
Itapona. Mungu ni mwema
 
Pole.

Naona huku juu umeshapata ushauri wa kuweza kusaidia.

Hilo la DNA isiwe kipaumbele sana, mtoto ameshazaliwa kwako ni wako hasa kipindi hiki cha ugonjwa usianze kuweka maulizo akilini mwako.

Zamani walikuwa wakisema baada ya miaka saba huo ugonjwa unapungua nguvu.

Pia tafuta waombaji, hata akiwa anatumia dawa na maombi yawepo, Mungu anapenda watoto, atamponya.
 
Kuna jamaa nimesoma naye o level na uni, alikuwa na shida hii. Hadi sasa yupo hai na ana mke na mtoto mmoja. Alikua akitumia mronge miaka yake yote. Na nadhani ndio uliomsaidia, maana familia yao ilikua ni duni kumudu hayo masuala ya kubadili damu.
 
Usikute Mtoto wa mchepuko, documents zimechakachuliwa
 
Hapana usimtirie mashaka mkeo Kwa lolote

Nina Binti pia anaumwa, historia nilivyouliza waliniambia hawana,lakini baada ya miaka miwili mbele niligundua Kuna ndugu wa babu ya baba inasadikika walikuwa wanakufa sana

Kuuliza kiundani walikuwa na changamoto zinazofanana na sickle cell..

Maana yangu vinaweza pita vizazi hata 4 au zaidi visioneshe dalili zozote ya kuumwa ila wakawa carrier TU

Kuhusu majibu hata mm mke alipewa kikaratasi Cha kawaida TU ambacho hakikua na details za kutosha, lakini Haina maana Kuna fraud yoyote
 
Pole sana mkuu. Fuata maelekezo ya wataalam na funguka kama hapa. Mbona mtafanikiwa tiba na kulea mtoto. All the best
 
Pole sana mkuu wapo wengi wanao zaliwa na huu ugonjwa ila Kwa case mbili nilizo ziona nilijifunza haya. Ina takiwa uwazi wa family nzima kuelewa hususani ni mgonjwa mwenyewe anatakiwa kupewa elimu juu ya vyakula vyenye kipaombele Kwake na Hali halisi ya ugonjwa. Maana ukicheza vibaya mtu kuvuka 20s ni msala sikutishi ila na kumbuka chuoni tulimzika dada mmoja alikua kwenye 21 hivi. Lakini ukiaangalia Kwa undani unakuta family ndio ilikuwa haijielewi mtu anaumwa sickle cell hafu anasoma boarding from one Hadi chuo sasa hiyo special care angeitowa wapi. Hapo ni mboga majani na matunda Kwa wingi na mkinge sana na malaria hapa hata hizo homa atazisikilizia kwenye bomba
 
Akifanikisha kuvuka 20s ndio huwa unaishiwa nguvu kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…