Mwanangu anapenda kuwa Askari polisi namsaidiaje kufuta fikra hizo?

Mpeleke kwa Mwamposa akaombewe
 
Kwa nn usimwambie uovu wao ili ajue ukwel ? Akjua ukwel atawachukia sana!! Kama mm nakumbuka zaman nakumbuka nliwah kuona mapolis wakimpiga mjomba angu Bure ,mjomba alinichukua nikiwa dogo sana kwenda center ya karb na home ,sasa tukakutana na gari la field force lilikua kinaitwa "shika kamba" wakampiga mafimbo Yao Bure tuu,kuanzia sku iyo sjawai wakubali Hawa jamaa,bas siku moja polis wakawa wanakimbiza majambazi yaliokua yameiba gari ,jambaz moja sugu likatokea kweny dirisha la gari na kumiminia gari la polis risas ,aisee nyie nyie nlifurah sanaaa yaan nliona majambazi kama ndo kiboko ya wates wa watu ,, na Kwa akili za kitot nkawa napenda majambazi kulko polis mpka baadae sana nlipokuja kua na akili za ukubwan
 
Kweli hilo ni janga ndugu
Dogo katinga kituoni,akikutana na mwema pale kituoni atajua vitu vingi sana napia kusaidia wengine,mpeleke skauti za mashuleni itampa dira nzuri zaidi ya kuanza jua yaliombele yake
 
Usimzuie kipawa chake ndio anaweza kuja kuleta mapinduzi makubwa ndani ya jeshi..!
 
Anataka Kuwa Pongo Oops Nzuri Sana
 
Astaghifilullah!Mtoto amepatwa na pepo baya sana.Mola awe na yeye tusimkose.
 
Ahahahahahah aisee
 
Mfundishe apende JESHI
 
Kwasasa unajiona upo sahihi, lakini amini nakwambia unatengeneza potential criminal bila kujijua ambayo itakuja kukugharimu pakubwa hapo baadaye.
Hiyo mentality unayoitengeneza ya mtoto kuchukia Polisi na ikatokea kwa bahati mbaya huyo dogo akakutana na makundi yanayo recruit watoto kuwa terrorist amini nakwambia kitakachotokea hapo kina uwezo hata wa kugharimu maisha yako.
Wazazi muwe makini sana na ideology mnazo pandikiza kwa watoto wenu
 
Polisi hawapaswi kuonea raia.
Muache ajiunge labda atakuja kuwa IGP na kufanya reforms
 
Mpeleke akafanyiwe maombi pepo la upolisi limtoke akuna pepo baya kama la upolisi
 
Mfundishe maadili aje awe Polisi mwenye hofu ya Mungu anayechukia rushwa na mpenda haki na usawa na uhai wa binadamu.
 
Kazi ya Polisi ni kazi nzuri.
Mimi kama wewe. Nilikuwa nalaani kabisa mtu katika familia yetu kuwa Polisi.
Na sidhani kama yupo Polisi katika familia yetu.
Lakini now I think different.
Inaleta balance katika familia watu kuwa na proffession tofauti.
 
Polisi hawapaswi kuonea raia.
Muache ajiunge labda atakuja kuwa IGP na kufanya reforms
IGP hapo alipo anataman kufanya reform lakn anashindwa kutokana na namna jeshi la polisi lilivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…