Mwanangu anashindwa kutumia common sense?? Hii ni shida gani?

nimekuelewa sana mkuu naww nimekuuliza
Sehemu tunayokaa hamna watoto wa rika lake kwaiyo watoto wa rika lake anaonana nao shule. sasa unavosema namchanganya na werevu nawatoa wap

mtoto anaenda asubuhi anarudi jioni!
ungefafanua tu hapo tungeelewana
Weekend au kipindi cha likizo
Usimuache ajifungie chumbani mwenyewe
 
tafuta kitu anaweza kufanya kwa ufanisi muendeleze huko. school is not for everebaadi. wengine wanakwenda kujua kusoma na kuandika. mfano p.funk majani. yule alikua ni kilaza wa masomo ya kawaida shuleni..IST wakagundua uwezo wake ktk muziki na mapenzi yake ktk fani ya utayarishaji. from there a star p.funk was born
 
mkuu naona uko well Educated kwene mambo za temperament
nieleweshe monology??

huyu kwa ninavomsoma ni introvert lakin sasa ndo nashangaa introvert huwa na akili nyingi tofauti ni kwake.


Mkuu , monology ni ile hali ya MTU kuongea peke yake hali hiyo sana Sana huwa wanakuwa nayo introvert.

Ikiwa mwanao ni introvert , muwekee mazingira ambayo yatamsapoti kutokana na hali yake.

Mfano swala la Akili kuwa smart huwa ni matokeo ya mtu kuwa na teachability attitude kupenda kufundishika na kupenda kujifunza.

Umri wake wa 17 bado ni umri Mdogo ikiwa utaanza kumjenga Kiakili na kihisia atakuwa smart Sana .

Kuwa smart ni swala la kuhakikisha kijana wako anakuwa na ile hali ya kujifunza mambo chanya kila siku.


Kuhusu kuwa mkimya na kuwa na akili au smart majibu yapo hivi.

Sisi introvert ni kweli watu husema tuko smart Ila ukweli ni kwamba sisi tunauwezo mkubwa wa kujifunza mambo na kuyaelewa kwa haraka kuzidi extrovert.

Hivyo unachobidi kufanya nikumuwekea supportive environment kijana wako Kutokana na hiyo silika yake. (introvert).
 
Pole sana ila usione kuwa ni mzigo. Binadamu tuna uwezo tofauti kwa sababu mbali mbali. Alikulia kwenye mazingira gani? Alikuwa anapigwa au kufokewa sana? Sisi waafrika kuna vitu huwa tunadhani ni kumjenga mtoto kumbe tunamharibu. Jaribu kumuonyesha upendo na kumsahihisha bila kumfokea.
 
Nilivyoona tu hii reply yako basi nimepata jibu tatizo ni wew
mkuu kwene familia zetu ni ngumu sana watoto kumzoea baba hasa kwakua anawafuatilia mambo yao muhimu!!

Kijana wangu nikiwa sipo anakaa sebulen na shangazi zake nakupga stori ila nikiwepo hang’ai hii ni kwasababu siwezi kaa hata nusu saa nisiulize mambo ya shule!

wengine hawana habari nae aende asiende wao sawa tu
 
mkuu naona uko well Educated kwene mambo za temperament
nieleweshe monology??

huyu kwa ninavomsoma ni introvert lakin sasa ndo nashangaa introvert huwa na akili nyingi tofauti ni kwake.
Huyo mtoto sio introvert ila ni kuwa umetengeneza mazingira ya kuogopwa kama baba. Huna muda nae zaidi ya kuulizia madaftari tu full time. Hii inaua confidence kwa mtoto.

Nilikulia mazingira hayo nilikuwa sina maamuzi juu ya chochote na siwezi toa opinion yeyote. Baba mlezi alikuwa mkali kama simba akija tunakimbilia kujificha vyumbani. Muda wote ni hofu tu kwamba ataanza kufoka mara kwanini sijisomei. Sikuwahi enjoy life kama mtoto.

Nilipoondoka kwenye mazingira yale na kurudi kwa baba mzazi ndio nikawa free sasa maana mzazi wangu yeye hakuwa mkoloni ila ni facilitator. Una raise matters anakusikiliza yuko supportive na unaweza kumpinga in short kuna freedom of speech. Hapo ndipo akili ilifunguka zaidi nikawa najihisi ni mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…