Mwanangu hachangamki

Mwanangu hachangamki

Atabadilika tu maana mimiwenyewe nilikuaga mzembe mzembe ila sasa iv wee nihatari
 
Huyo ni mtumishi wa Mungu, mpeleke madhabauni mapema. Mungu atasema naye sana na ataokoa kizazi chenu. Ni kina Musa hao.

Hesabu 12:3
[3]Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.
Acha kuleta hekaya za vitabuni hapa.
 
Mshukuru mwalimu anamshughulisha huyo mtoto, huyo asipopata shughuli za kuchangamsha akili yake atakuwa jingajinga.

Usimlee kimayai mpe shughuli ndogondogo hapo nyumbani na ufatilie utendaji wake
 
Wakuu dogo saivi yuko la pili...hachangamki kabisa...ni mtu wa kukaa pekee yake ...anaweza akacheza kidogo tu nawenzake halafu aka achana nao mda huohuo
Nishamuuliza sana ana tatizo gani mbona anakuwa mpole sana?ila anasema hana tatizo tu,,,kingine anakuwa na mawazo sana hadi mwalimu wake ashawahi kuniita kuniuliza...lakini nikamwambia hana tatizo..

Dogo kuna siku alikuwa na mawazo sana ...ikabidi nimuulize shida ndio akaniambia ametumwa shuleni mbolea...nikahisi tu huyu walimu wanamchapa sana...asa mbolea anatoa wp mtoto wa darasa la pili.
Mchukue nenda nae sehem nzuri atakayokua na utulivu wa akili ongea nae kirafiki kabisa lazima atakwambia ni nini kinamsibu.
 
Hapana kuna katoto miaka 3 ni hacheki anabaguwa wa kumbeba sijui uko mbeleni
 
Back
Top Bottom