VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Kimbelembele changu kiliwahi kuniponza. Niliwahi kwenda ofisini kwa Paul Makonda, alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo. Mazungumzo yenyewe yalitakiwa na yeye mwenyewe katika kujipanga na kujidai kwake kichama na kiserikali. Katika timu iliyokwenda ofisini kwake siku husika, mimi ndiye niliyekuwa mtu mzima kuliko wengine. Ilikuwa rahisi kuniona na kunitambua.
Pamoja na utumishi wangu uliotukuka kwenye chama na serikali, siku hiyo nilionja joto ya jiwe. Kila mfano mbaya nilitolewa mimi. Wazee tulionekana ndo chanzo cha kila tatizo, uozo, mzozo na gumzo. Tulionwa na Makonda pia hatufai na hatuna maana yoyote. Nilijuta hata kushiriki na kumpitisha kwenye 'vetting' yake kichama na kiserikali. Nilijisikia vibaya sana kwa kubagazwa, kutwezwa na kubezwa. Lakini, nikabaki kimya. Nikavumilia.
Baada ya kikao kile, kila mmoja wetu alitafutwa na Makonda na kuendelea kumwagiwa mambo yake. Mimi nilidhalilishwa kikauli bila nauli; nilioneshwa jeuri bila uzuri; niliambiwa mambo ya kutishwa na kutahadharishwa. Kwakuwa najiamini na najua Makonda hawezi kunifanyia lolote na popote, nilibaki kimya na kuvumilia. Nilikaa naye mbali. Hata alipowatuma watu wake kuja kuniomba ushauri kuhusu ubunge wake, niliwajibu kuwa wazee hawana uwezo wa kumshauri. Akaninunia zaidi na kunipania. Yakatokea taliyotokea.
Sasa mwanangu Makonda anakonda. Hajiamini. Anaogopa kila mlio na kila apitaye au aongeaye. Ana hofu kwa uchafu wake. Ameshasahau kebehi, jeuri, kiburi, majivuno, dhulma, hila na inda aliyotuonesha akiwa Mkuu wa Mkoa na jinsi tulivyovumilia na kutulia. Ameshau kuwa tulikuwa tukichomwa na kuumwa na kauli na matendo yake. Alidhani mambo yatabaki vile na ataendelea kubaki yule. Mambo yamebadilika. Wazee bado tupo kama vile, tunadunda.
Kwangu mimi nguli wa siasa, Makonda ametupa karata yake ya mwisho kupitia tuhuma zake za vitisho. Amenyoosha mkono ili Mama Samia na Serikali yake wamuone. Waone kuwa ipo haja ya yeye kurejeshwa Serikalini ili kumfanya kuwa salama. Yaani, Makonda ameomba kupewa cheo ili awe salama. Bado ana siasa za kilaghai na kitapeli. Ana siasa za kitoto. Ana siasa za magumashi. Bora akae atulie. Karma is real!
Mama Samia, nasi tuanze makundi na kampeni za 2025?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Misungwi, Mwanza)