Mwanangu Makonda, tulia kama tulivyotulia... Vumilia kama tulivyovumilia

Makonda Paulo Daudi Bashite Albert, Je anastahili haya anayopitia? ama anaonewa na watesi wake?

1649769606619.png
 
Anataja makundi ya wauza madawa ya kulevya wanataka kumshughulikia....ukitazama katika ile orodha aliyowahi itaja hakuna hata mmoja zaidi ya Shikuba amembaye alifikishwa mahakamani na kupatikana na hatia, alimsababishia madhira Manji akabumba kesi mwisho wa siku akaambulia aibu....alitaka kumchafua Mzee Lowassa kwa kumsingizia kuwa ametelekeza mtoto...mwisho wa siku akaambulia aibu....Kuna wakati wa kupanda na wakati wa mavuno....atulie tu huu ni wakati wake wa mavuno....waswahili tunasema "usipande miiba kwenye njia ambayo unaweza pita usiku ukiwa miguu peku"
 
Kimbelembele changu kiliwahi kuniponza. Niliwahi kwenda ofisini kwa Paul Makonda, alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo. Mazungumzo yenyewe yalitakiwa na yeye mwenyewe katika kujipanga na kujidai kwake kichama na kiserikali. Katika timu iliyokwenda ofisini kwake siku husika, mimi ndiye niliyekuwa mtu mzima kuliko wengine. Ilikuwa rahisi kuniona na kunitambua.

Pamoja na utumishi wangu uliotukuka kwenye chama na serikali, siku hiyo nilionja joto ya jiwe. Kila mfano mbaya nilitolewa mimi. Wazee tulionekana ndo chanzo cha kila tatizo, uozo, mzozo na gumzo. Tulionwa na Makonda pia hatufai na hatuna maana yoyote. Nilijuta hata kushiriki na kumpitisha kwenye 'vetting' yake kichama na kiserikali. Nilijisikia vibaya sana kwa kubagazwa, kutwezwa na kubezwa. Lakini, nikabaki kimya. Nikavumilia.

Baada ya kikao kile, kila mmoja wetu alitafutwa na Makonda na kuendelea kumwagiwa mambo yake. Mimi nilidhalilishwa kikauli bila nauli; nilioneshwa jeuri bila uzuri; niliambiwa mambo ya kutishwa na kutahadharishwa. Kwakuwa najiamini na najua Makonda hawezi kunifanyia lolote na popote, nilibaki kimya na kuvumilia. Nilikaa naye mbali. Hata alipowatuma watu wake kuja kuniomba ushauri kuhusu ubunge wake, niliwajibu kuwa wazee hawana uwezo wa kumshauri. Akaninunia zaidi na kunipania. Yakatokea taliyotokea.

Sasa mwanangu Makonda anakonda. Hajiamini. Anaogopa kila mlio na kila apitaye au aongeaye. Ana hofu kwa uchafu wake. Ameshasahau kebehi, jeuri, kiburi, majivuno, dhulma, hila na inda aliyotuonesha akiwa Mkuu wa Mkoa na jinsi tulivyovumilia na kutulia. Ameshau kuwa tulikuwa tukichomwa na kuumwa na kauli na matendo yake. Alidhani mambo yatabaki vile na ataendelea kubaki yule. Mambo yamebadilika. Wazee bado tupo kama vile, tunadunda.

Kwangu mimi nguli wa siasa, Makonda ametupa karata yake ya mwisho kupitia tuhuma zake za vitisho. Amenyoosha mkono ili Mama Samia na Serikali yake wamuone. Waone kuwa ipo haja ya yeye kurejeshwa Serikalini ili kumfanya kuwa salama. Yaani, Makonda ameomba kupewa cheo ili awe salama. Bado ana siasa za kilaghai na kitapeli. Ana siasa za kitoto. Ana siasa za magumashi. Bora akae atulie. Karma is real!

Mama Samia, nasi tuanze makundi na kampeni za 2025?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Misungwi, Mwanza)
Katumia silaha yake ya mwisho kabisa.. Hana nyingine tena iliyobaki.. Sasa ni mwendo wa kukimbia mpaka kivuli chake
 
Anataja makundi ya wauza madawa ya kulevya wanataka kumshughulikia....ukitazama katika ile orodha aliyowahi itaja hakuna hata mmoja zaidi ya Shikuba amembaye alifikishwa mahakamani na kupatikana na hatia, alimsababishia madhira Manji akabumba kesi mwisho wa siku akaambulia aibu....alitaka kumchafua Mzee Lowassa kwa kumsingizia kuwa ametelekeza mtoto...mwisho wa siku akaambulia aibu....Kuna wakati wa kupanda na wakati wa mavuno....atulie tu huu ni wakati wake wa mavuno....waswahili tunasema "usipande miiba kwenye njia ambayo unaweza pita usiku ukiwa miguu peku"

Shikuba alikamatwa awamu ya nne kwenye ule msala wake wa Lindi na yule binti wa Liumba wa BOT....Wanyamwezi walikuwa wanamtafuta kitambo wakamuomba na kumpeleka USA na kijana wake Tikotiko, Tikotiko ndio pekee alikamatwa awamu ta tano....wote wakala mvua USA japo tikotiko ameshaachiwa baada ya kutumikia....
 
Akina Le mutuz alikuwa kila siku anampost Makonda nakumsifia kwa kumuita El comendant ila leo hii kamkimbia mwenzake na kahamia kuwasifia mabilionea
 
Kwanza atuambie kwamba yeye ni Daudi Albert Bashie ama ni Paul Christian Makonda??
 
Kimbelembele changu kiliwahi kuniponza. Niliwahi kwenda ofisini kwa Paul Makonda, alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo. Mazungumzo yenyewe yalitakiwa na yeye mwenyewe katika kujipanga na kujidai kwake kichama na kiserikali. Katika timu iliyokwenda ofisini kwake siku husika, mimi ndiye niliyekuwa mtu mzima kuliko wengine. Ilikuwa rahisi kuniona na kunitambua.

Pamoja na utumishi wangu uliotukuka kwenye chama na serikali, siku hiyo nilionja joto ya jiwe. Kila mfano mbaya nilitolewa mimi. Wazee tulionekana ndo chanzo cha kila tatizo, uozo, mzozo na gumzo. Tulionwa na Makonda pia hatufai na hatuna maana yoyote. Nilijuta hata kushiriki na kumpitisha kwenye 'vetting' yake kichama na kiserikali. Nilijisikia vibaya sana kwa kubagazwa, kutwezwa na kubezwa. Lakini, nikabaki kimya. Nikavumilia.

Baada ya kikao kile, kila mmoja wetu alitafutwa na Makonda na kuendelea kumwagiwa mambo yake. Mimi nilidhalilishwa kikauli bila nauli; nilioneshwa jeuri bila uzuri; niliambiwa mambo ya kutishwa na kutahadharishwa. Kwakuwa najiamini na najua Makonda hawezi kunifanyia lolote na popote, nilibaki kimya na kuvumilia. Nilikaa naye mbali. Hata alipowatuma watu wake kuja kuniomba ushauri kuhusu ubunge wake, niliwajibu kuwa wazee hawana uwezo wa kumshauri. Akaninunia zaidi na kunipania. Yakatokea taliyotokea.

Sasa mwanangu Makonda anakonda. Hajiamini. Anaogopa kila mlio na kila apitaye au aongeaye. Ana hofu kwa uchafu wake. Ameshasahau kebehi, jeuri, kiburi, majivuno, dhulma, hila na inda aliyotuonesha akiwa Mkuu wa Mkoa na jinsi tulivyovumilia na kutulia. Ameshau kuwa tulikuwa tukichomwa na kuumwa na kauli na matendo yake. Alidhani mambo yatabaki vile na ataendelea kubaki yule. Mambo yamebadilika. Wazee bado tupo kama vile, tunadunda.

Kwangu mimi nguli wa siasa, Makonda ametupa karata yake ya mwisho kupitia tuhuma zake za vitisho. Amenyoosha mkono ili Mama Samia na Serikali yake wamuone. Waone kuwa ipo haja ya yeye kurejeshwa Serikalini ili kumfanya kuwa salama. Yaani, Makonda ameomba kupewa cheo ili awe salama. Bado ana siasa za kilaghai na kitapeli. Ana siasa za kitoto. Ana siasa za magumashi. Bora akae atulie. Karma is real!

Mama Samia, nasi tuanze makundi na kampeni za 2025?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Misungwi, Mwanza)
Laghai na tapeli😀😀😀😀😀
 
Back
Top Bottom