Mwanangu Makonda, tulia kama tulivyotulia... Vumilia kama tulivyovumilia

Hata Sabaya ilikuwa hivihivi, alienda Clouds akaliamsha dude likatambaa naye 30 yrs na bado kuna mingine.
Kijana anaenda kuzeekea na kufia jela kisa Magufuli alikuwa anakupa moyo kuwa we fanya tuu mie nipo!
Hakika Mkuu
 
Buuuuuuuuuuuuuuoooooo !!!! ni mlipuko au [emoji50][emoji50][emoji50]
 
Kimbelembele changu kiliwahi kuniponza. Niliwahi kwenda ofisini kwa Paul Makonda, alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo. Mazungumzo yenyewe yalitakiwa na yeye mwenyewe katika kujipanga na kujidai kwake kichama na kiserikali. Katika timu iliyokwenda ofisini kwake siku husika, mimi ndiye niliyekuwa mtu mzima kuliko wengine. Ilikuwa rahisi kuniona na kunitambua.

Pamoja na utumishi wangu uliotukuka kwenye chama na serikali, siku hiyo nilionja joto ya jiwe. Kila mfano mbaya nilitolewa mimi. Wazee tulionekana ndo chanzo cha kila tatizo, uozo, mzozo na gumzo. Tulionwa na Makonda pia hatufai na hatuna maana yoyote. Nilijuta hata kushiriki na kumpitisha kwenye 'vetting' yake kichama na kiserikali. Nilijisikia vibaya sana kwa kubagazwa, kutwezwa na kubezwa. Lakini, nikabaki kimya. Nikavumilia.

Baada ya kikao kile, kila mmoja wetu alitafutwa na Makonda na kuendelea kumwagiwa mambo yake. Mimi nilidhalilishwa kikauli bila nauli; nilioneshwa jeuri bila uzuri; niliambiwa mambo ya kutishwa na kutahadharishwa. Kwakuwa najiamini na najua Makonda hawezi kunifanyia lolote na popote, nilibaki kimya na kuvumilia. Nilikaa naye mbali. Hata alipowatuma watu wake kuja kuniomba ushauri kuhusu ubunge wake, niliwajibu kuwa wazee hawana uwezo wa kumshauri. Akaninunia zaidi na kunipania. Yakatokea taliyotokea.

Sasa mwanangu Makonda anakonda. Hajiamini. Anaogopa kila mlio na kila apitaye au aongeaye. Ana hofu kwa uchafu wake. Ameshasahau kebehi, jeuri, kiburi, majivuno, dhulma, hila na inda aliyotuonesha akiwa Mkuu wa Mkoa na jinsi tulivyovumilia na kutulia. Ameshau kuwa tulikuwa tukichomwa na kuumwa na kauli na matendo yake. Alidhani mambo yatabaki vile na ataendelea kubaki yule. Mambo yamebadilika. Wazee bado tupo kama vile, tunadunda.

Kwangu mimi nguli wa siasa, Makonda ametupa karata yake ya mwisho kupitia tuhuma zake za vitisho. Amenyoosha mkono ili Mama Samia na Serikali yake wamuone. Waone kuwa ipo haja ya yeye kurejeshwa Serikalini ili kumfanya kuwa salama. Yaani, Makonda ameomba kupewa cheo ili awe salama. Bado ana siasa za kilaghai na kitapeli. Ana siasa za kitoto. Ana siasa za magumashi. Bora akae atulie. Karma is real!

Mama Samia, nasi tuanze makundi na kampeni za 2025?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Misungwi, Mwanza)
Aisee
 
Kwa jinsi Makonda alivyojaa kiburi kipindi cha Magufuli, huwezi kuamini yeye ndio anajifanya kulia sasa. Kuna uwezekano Makonda akapata kinga ya muda kwa serikali hii ya ccm, ila jinai haifi ni lazima atakuja kukutana na mkono wa sheria tu huko mbele.

Lakini kwa sasa anatakiwa avunjwe miguu yote miwili ili aone ni jinsi gani wale aliowaua na kuwaacha na vilema vya maisha wanajisikia. He should pay the price of his barbaric behaviour.
Hata jinai ya mbowe haifi japo utawala huu umemwonea huruma
 
Aliyekuwa mwanachama wenu mwaminifu Leo mnamsimanga Kwa viwango,hivi mwoneeni huruma ,msije mwuua Kwa msongo wa mawazo 🤭
"Hakuna asiyejua, wanasiasa ni Wanafiki" Steven Wassira, 13 May, 2023
 
Ningekuwa mie ndio Makonda a.k.a. Bashite ningesaga chupa nachanganya na sumu ya panya, DDT, dawa za kutolea mimba pamoja maji ya betri nakunywa nife niende kuzimu nikaungane na wengine humo.
Ndo maana Makonda sio wewe na wewe sio Makonda.
 
Kwa jinsi Makonda alivyojaa kiburi kipindi cha Magufuli, huwezi kuamini yeye ndio anajifanya kulia sasa. Kuna uwezekano Makonda akapata kinga ya muda kwa serikali hii ya ccm, ila jinai haifi ni lazima atakuja kukutana na mkono wa sheria tu huko mbele.

Lakini kwa sasa anatakiwa avunjwe miguu yote miwili ili aone ni jinsi gani wale aliowaua na kuwaacha na vilema vya maisha wanajisikia. He should pay the price of his barbaric behaviour.
Kabisa Mkuu..
Nakazia hapo pa kumvunja mguu Bashite..au kama mchakato wa kuondoka na mguu ule ni mrefu,watu waanze hata na sikio la upande mmoja basi.
 
Kimbelembele changu kiliwahi kuniponza. Niliwahi kwenda ofisini kwa Paul Makonda, alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo. Mazungumzo yenyewe yalitakiwa na yeye mwenyewe katika kujipanga na kujidai kwake kichama na kiserikali. Katika timu iliyokwenda ofisini kwake siku husika, mimi ndiye niliyekuwa mtu mzima kuliko wengine. Ilikuwa rahisi kuniona na kunitambua.

Pamoja na utumishi wangu uliotukuka kwenye chama na serikali, siku hiyo nilionja joto ya jiwe. Kila mfano mbaya nilitolewa mimi. Wazee tulionekana ndo chanzo cha kila tatizo, uozo, mzozo na gumzo. Tulionwa na Makonda pia hatufai na hatuna maana yoyote. Nilijuta hata kushiriki na kumpitisha kwenye 'vetting' yake kichama na kiserikali. Nilijisikia vibaya sana kwa kubagazwa, kutwezwa na kubezwa. Lakini, nikabaki kimya. Nikavumilia.

Baada ya kikao kile, kila mmoja wetu alitafutwa na Makonda na kuendelea kumwagiwa mambo yake. Mimi nilidhalilishwa kikauli bila nauli; nilioneshwa jeuri bila uzuri; niliambiwa mambo ya kutishwa na kutahadharishwa. Kwakuwa najiamini na najua Makonda hawezi kunifanyia lolote na popote, nilibaki kimya na kuvumilia. Nilikaa naye mbali. Hata alipowatuma watu wake kuja kuniomba ushauri kuhusu ubunge wake, niliwajibu kuwa wazee hawana uwezo wa kumshauri. Akaninunia zaidi na kunipania. Yakatokea taliyotokea.

Sasa mwanangu Makonda anakonda. Hajiamini. Anaogopa kila mlio na kila apitaye au aongeaye. Ana hofu kwa uchafu wake. Ameshasahau kebehi, jeuri, kiburi, majivuno, dhulma, hila na inda aliyotuonesha akiwa Mkuu wa Mkoa na jinsi tulivyovumilia na kutulia. Ameshau kuwa tulikuwa tukichomwa na kuumwa na kauli na matendo yake. Alidhani mambo yatabaki vile na ataendelea kubaki yule. Mambo yamebadilika. Wazee bado tupo kama vile, tunadunda.

Kwangu mimi nguli wa siasa, Makonda ametupa karata yake ya mwisho kupitia tuhuma zake za vitisho. Amenyoosha mkono ili Mama Samia na Serikali yake wamuone. Waone kuwa ipo haja ya yeye kurejeshwa Serikalini ili kumfanya kuwa salama. Yaani, Makonda ameomba kupewa cheo ili awe salama. Bado ana siasa za kilaghai na kitapeli. Ana siasa za kitoto. Ana siasa za magumashi. Bora akae atulie. Karma is real!

Mama Samia, nasi tuanze makundi na kampeni za 2025?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Misungwi, Mwanza)
Na Rais Samia akitaka kujua hasira ya watanzania kwa huyu mwehu Bashite,basi mpe hata cheo cha Mtendaji wa Kata.
 
Manara atulie tuu, afanye mambo ya mpira.
ila kabla ya huo mpira Manara alikuwa kijana wa chama, kada mtiifu aliyeponea kwenye tundu la sindano kwenda lupango.

Hakuna jipya sana Mkuu, ni muda tu ndio unaobadilika.
 
Kwani CCM kuna asiye mwizi? Manara ni kama wengine tuu na huko kwenye mpira ni cover up ya uchokoraa wake.
malisa_gj-___CS-KDJgMnmF___-.jpg
 
Back
Top Bottom