VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Jana nilikusikia na kukusikitikia sana. Jinsi unavyojikaanga kwa mafuta yako mwenyewe. Jinsi unavyoonesha kuchoka na kukinai nafasi uliyonayo kwasasa chamani. Pale ulipozungumzia kuhusu mdahalo na viongozi wa CHADEMA.
Ngoja nikusaidie kwakuwa nilikuwa kiongozi mwandamizi chamani kabla yako. Naujua msimamo wa CCM juu ya midahalo. Ni kwamba, CCM si mfuasi na wala mpenda midahalo. Hata wagombea wetu wa Urais tangu kuanza kwa vyama vingi hukwepa midahalo, isipokuwa Hayati Benjamin Mkapa.
Mdahalo si lelemama. Mdahalo si mchezo. Ni rahisi kuchanganya msimamo wa chama na hisia binafsi mdahaloni na kuharibu bila ya kutibu. Hata kutubu huwa tabu. Mdahalo na CHADEMA, chama kikuu cha upinzani ni kuwatangaza na kuwapa umaarufu.
CHADEMA watakuwa huru kusema kwa kukosoa kila lifanywalo na Serikali inayoundwa na CCM. Jazba inaweza kutokea; makosa ya kitakwimu yanaweza kutokea; usahaulifu unaweza kutokea; kujichanganya kunaweza kutokea na hivyo CCM huepuka midahalo baada ya kuyatazama mambo hayo na mengine kwa kina.
Mwanangu Makonda, acha kutafuta kiki zisizo na mpango. Midahalo inayohusisha CCM kama taasisi ilishapigwa marufuku. Mfuate Komredi Anamringi Macha, Kaimu Katibu Mkuu akuoneshe kumbukumbu nyeti za kichama kuhusu hilo.
Halafu, Mwenezi napaswa kusemezana na Mwenezi. Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au Katibu Mkuu wa chama chochote cha siasa nchini si 'level' yako. Hautasifiwa na yeyote ukimtaja na kumtaka Mbowe au Lissu kwenye mdahalo. Ni kiki tu. Kama umechoka tuambie tuchukue hatua za kichama.
Mabadiliko ya sheria za uchaguzi yatanguliwe na mabadiliko ya katiba!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Burigi, Chato)