Mwanangu Makonda, umeichoka na kuikinai nafasi yako chamani?

Chama kikongwe cha siasa kinaogopa midahalo,sasa icho ni chama au genge la Wahuni.
Vyama vikongwe kama Labor na Conservative vya Uingereza na Republican na Democrat vya Marekani haviogopi midahalo, kwanini CCM?
Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya alishasema kuwa CHADEMA ni Wajenzi wa hoja wazuri kuliko CCM (tuishi humu)

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Huwa nakufananisha na mzee mkama!
 
Mdahalo ni hoja! Na hoja ni mpaka ziwepo!!

CHADEMA wamelambishwa asali na Chama Cha anayeutaka mdahalo!!

Viongozi wa CHADEMA wameneemeka na Ruzuku, magorofa yameshamiri Kila Kona mpaka kule Umachameni!!

CHADEMA wameomba wawepo wabunge wawili Kila jimbo, Watanzania wamewashangaa na kuwapuuza; nguvu ya hoja inatoka wapi?

Pale mikocheni imebainika Chama kimepangishwa kwenye jengo la Mbowe; likiibuka hilo huoni namna macho ya wanamdahalo yatakavyopoteza mwelekeo?

Hayo ni machache katika mengi tunayoweza kuyaweka mezani na mdahalo ukawa mwiba kwa CHADEMA.

CCM siyo wajinga, jichanganyeni mkakutane na Form Four ambaye hana subra!!

Namshauri Lissu aendelee kuukimbia mcdahalo kama alivyoyakimbia maandamano ya januari 24!
 
Amazing
 
Kwanza ni Makonda au Bashite ?
 
Mtu mwenye tuhuma chafu kama Makonda anaomba mdahalo na mtu kama Lissu?!
 
Ni kweli. Juzi hapa Dar nilimkuta kijana mjanja kwa viwango vya mtaani. Nikamwuliza kama anasoma shule? Akanijibu kisha maliza shule! Nikamwuliza kamaliza shule gani? Akanijibu darasa la saba. Nikamwambia unasema umemaliza shule mbona ndiyo unaanza? Akanijibu kuwa yeye kisha maliza shule na kama siamini nimwulize swali lo lote nione kama atashindwa kujibu!! Ikabidi nimwache, sikummuliza swali!!
 
Samahan mzee wangu. Kwa hio wasiwas wako ni kuwa makonda atachanganya mafile. Nadhan debate ni nzuri mbona marekan trump kila siku debate na anakuwa muda mwinginwle anachemka
 
Asante kwa kulinda heshima na sifa ya chama chetu.maana asiyesikia la mkuu uvunjika mguu.
 
Wakati Kikwete wanamchomoa jukwaani katikati ya mdahalo baada ya kuanza kumung'unya maneno huyu mtoto alikuwa shule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…