Mwanangu Makonda, umeichoka na kuikinai nafasi yako chamani?

Ina kipi kipya? Makonda anaweza fanya mdahalo na lisu? Yule mwenyekiti wa UVCCM anaweza fanya Mdaharo na Yule wa BAVICHA? We jamaaa wewe.
Tofuaiti ni kwamba, CCM ya zamani ilikuwa haitaki midahalo ya Sasa imataka.

Kwani unataka tusemeje Sasa?
 
Halafu, Mwenezi napaswa kusemezana na Mwenezi. Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au Katibu Mkuu wa chama chochote cha siasa nchini si 'level' yako. Hautasifiwa na yeyote ukimtaja na kumtaka Mbowe au Lissu kwenye mdahalo. Ni kiki tu. Kama umechoka tuambie tuchukue hatua za kichama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makonda ni zaidi ya CHADEMA. Ndo maana CDM kimetoa tamko/Taarifa kuhusu Makonda!

Tulieni
 
We nae kichwa panzi kweli kweli, kwa akili yako unazani atakaa nao katika mdahalo? Hizo kiki tu usiwe taken sana na hisia.
 
LAWAMA HIZI ZIENDE KWA ASKOFU GWAJIMA,YEYE SI ALISEMA ANAMFUTA MOJA KWA MOJA KWENYE RAMANI ZA ULINGO WA SIASA??

NINI SASA KINAENDELEA,AU NI EPISODE YA PILI
 
Mimi naweza kufanya mdahalo na kamati kuu nzima ya CHADEMA iliyojiandaa kwa mwezi mzima na nikaikalisha na kuipa darasa na Elimu ya kutosha juu ya masuala mbalimbali ya kisiasa ,kijamii ,kiuchumi n.k.
Pale ponguwani na nguruwe wa ccm anapohis kuweza kufanya mdahalo na chadema.
 
Acha kijana afanye mdahalo, zama zinabadilika, acha kumwingiza kijana baridi
Hivi kweli kwa akili yako ya kuzaliwa tu ukiacha mbali ya shule unaamini Makonda ana content yoyote tangible ya kufanya mdahalo na Lissu! Wonders shall never end.
 
Yani zero brain akadebate na Lissu bora wewe kada mkongwe umekiri CCM na midahalo ni mbalimbali.

Maana 2010 mliijarabu midahalo kwenye media yenu ya TBCCM mkaishia kupata fedhea na kama ilivyo kawaida yenu mkatafuta mbuzi wa kafara kwa kupoteza majimbo mkaruka na Tido Mhando.
 
Nakubaliana na wewe mdahalo ufanyike,maana huko hakutakuwa na JW wala PT mnakokimbilia.
 
MAKONDA NI MJUAJI WA KILA KITU WACHA AENDE KWENYE HUO MDAHALO AIVUE NGUO CCM

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Nakuunga mkono kwa asilimia mia. Ni bahati mbaya sana CCM ina makada vijana wasioweza kuona changamoto zinazoweza kukikabili chama kwa maamuzi ya kukurupuka na kutafuta kiki. Mbali na sababu ulizoziainisha, Makonda hana kichwa cha kuweza kufanya mdahalo na Lissu au Mbowe, si level yake kwa akili na uwezo wa kujadili serious issues ukiweka pembeni vyeo vyao kichama. Sana sana atachemka na kuanza kutukana.

Kapata katibu mkuu mwenye msimamo na anaekijuwa chama na siasa za nchi hii. Asitegemee kumchezea Nchimbi kwa figisu zake na ubabe aliouzoea. Nchimbi siyo mwoga na wala hana tabia ya kuongoza kwa kujikomba. Nauona mwisho mbaya wa Makonda hasipobadilika.
 
Wakubwa wametafakari na kuona ukweli ametolewa na kupelekwa kuleee! atulie anaongea anapitiliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…