Mwanangu wa darasa la pili hili swali kakosaje? Au mwalimu ndiye hajielewi?

Mwanangu wa darasa la pili hili swali kakosaje? Au mwalimu ndiye hajielewi?

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Shule za msingi zinafungwa Leo, Niko hapa napitia mitihani na ripoti za wanangu!

Kuna swali hili; Mwamuzi wa mchezo wa mpira wa miguu anaitwa nani? Mwanangu kajibu MWAMUZI kakosa, eti mwalimu kawaambia jibu sahihi ni REFARII.

Je, jibu sahihi ni lipi hapo? Kosa ni la mtoto au mwalimu ndo hajielewi?

ed.jpg

2797179_Screenshot_20210604-083525.jpg
 
Unajua mfundishaji wa watoto shuleni ni mfundishaji ndio lakini jina specific analoitwa ni mwalimu. Sasa ukijibu mfundishaji haujakosea Sana ila sio sahihi kwa 100%.

Ni sawa na ukamuita mtu mlimaji badala ya mkulima, au muendeshaji badala ya dereva.
 
Mkuu mwanao mjanja mjanja sana. Katelezea kwenye swali mule mule, mwamuzi wa mpira anaitwa, nae karudia mwamuzi!

Hivi mkuu nikikuuliza fundi wa ujenzi wa nyumba anaitwa nani utasema fundi au muashi

Tukiuliza askari wa usalama barabarani anaitwa nani utasema askari au trafiki

Tukiuliza muendesha ndege anaitwa nani utasema mwendesha ndege au rubani
 
Nikiwa darasa la kwanza niliulizwa kwenye mtihani kuwa sare tunayovaa shuleni inaitwaje nikajibu ni sweta, shati na kaptura. Nilishindwa kabisa kujua kama yunifomu ni neno la kutumika katika Kiswahili, kati ya mitihani yangu pendwa ninayoitazama na kufurahia na ule upo.
 
Ukimwambia mtoto mwalimu kakukosesha utamujaribu kisaikolojia, hatamuamini tena mwalimu tena anaweza kumchukia kabisa, hapo maliza kesi kiutu uzima, mwambie baby hapa mwalimu alijisahau kidogo akakuwekea umekosa, lakini ulipata.
 
Unajua mfundishaji wa watoto shuleni ni mfundishaji ndio lakini jina specific analoitwa ni mwalimu. Sasa ukijibu mfundishaji haujakosea Sana ila sio sahihi kwa 100%.

Ni sawa na ukamuita mtu mlimaji badala ya mkulima, au muendeshaji badala ya dereva.
Akili kubwa

Sent from my TECNO B1 using JamiiForums mobile app
 
Shule za msingi zinafungwa Leo, Niko hapa napitia mitihani na ripoti za wanangu!
Kuna swali hili; Mwamuzi wa mchezo wa mpira wa miguu anaitwa nani?....mwanangu kajibu MWAMUZI kakosa...Eti mwalimu kawaambia jibu sahihi ni REFARII

Je; jibu sahihi ni lipi hapo? Kosa ni la mtoto Au mwalimu ndo hajielewi?
View attachment 1807698
View attachment 1807699
La pili! Basi kijana wako yupo vizuri, lakini jibu hilo ni kweli kakosea.

Haiwezekani 'structure' ya swali ikatumika kuwa ndiyo jibu la swali hilo hilo....'Mwamuzi' wa michezo halafu jibu liwe 'mwamuzi' hiyo hiyo.
 
Back
Top Bottom