All in all, angalia shuleni, watoto anaocheza nao, na vipindi anavyoangalia kwenye TV. Kuna ujinga ujinga mwingi sana. Mfano mdogo, hebu sikiliza radio zetu kuanzia saa mbili hivi asubuhi mpaka mchana wanaongea vitu gani?
Huwa najiuliza, hivi hizi radio mpaka zinaruhusu mavipindi ya umbea umbea na ujinga, kweli wamekosa program ambazo zinaweza kuwa interest watu kwa muda huo? mfano wakileta wataalamu wa biashara mbali mbali na kuwafundisha watu mida hiyo ya saa mbili mpaka saa nane mchana, si ingekuwa na tija sana. Hata mambo ya banking, maswala ya kutunza na kumanage hela. Kuna mengi sana. Wao wamekomalia maumbea umbea na udaku sijui kuchamba..mbaya zaidi kuna vipindi eti mashoga kabisa wanaendesha.