Mwanangu wa kiume miaka 4 lakini haongei ni kupiga makelele tu

Yohane 9 : 2 Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu?
3 Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake.

Msaidie kupata mazoezi maalum, hiyo.pesa utaitupa tu bure kwa matapeli, Hiyo ni mboneka yake
 
kama ajaanza shule tafuta izi shule za watoto wadogo za mtaani...hizi local sio hizi za ada kubwa....mpeleke akazuge uko....akutane na ile changanyikeni ya watoto wa mtaani...inaweza saidia pia
 
Zile Mercury kwenye chanjo ni hatarishi sana. Zinavuruga gastrointestinal system na mfumo mzima wa fahamu.

Hata immune system lazima ivurugike na kufubaa.

Watakwambia umuone PEDIATRICIAN ili mtoto akadungwe machanjo mengine tena.

Cc DR Mambo Jambo
 
Sdhan kama ni usonji, umeambiwa anapenda kupiga piga kidevu rejea watu wenye mental retardation utaona tabia zao
Ndio maana zinaitwa "Autistic Spectrum Disorders".
Ameorodhesha tabia nyingi na hiyo kupiga kidevu ikiwepo.
 

Attachments

  • images (3).jpeg
    39.5 KB · Views: 14
Mercury Ni sumu Hakuna Chanjo iliyo na mercury Bichwa!
Unaweza kunitajia Moja?
 
With All Due Respect Mkuu, samahani kwa Maswali haya nitakayokuuliza!
  • Unafahamu Kuhusu Speech pattern (Speech Development milestone) ya Mtoto? Kama unaijua niambie kwanini Umesema mtoto huyo ni Mute au Mute-Deaf (Bubu)?
  • Unafahamu kuhusu Polio?
  • Dalili za mental Retardation ulizoziona ni zipi?
  • Teratogenic 😅😅 (Samahani kwa kucheka) unajua Maana yake? Unayajua magonjwa yanayotokana na Hiyo Disorder?
  • Una ufahamu wowote kuhusu Usonji (ASD-Autism spectrum disorder)?
Samahani lengo la kuuliza kulia mtoto ulikuwa unataka kujua nini? Kama ni APGAR score ya mtoto,Je mtoto wa Miaka minne itasaidia nini?

Lengo la maswali hayo nataka Tuweke mazingira sawa ili tutoke na Wazo moja la kumsaidia Huyu baba kwa mwanae..

Natanguliza Shukrani za dhati kwako
 
Zile Mercury kwenye chanjo ni hatarishi sana. Zinavuruga gastrointestinal system na mfumo mzima wa fahamu.

Hata immune system lazima ivurugike na kufubaa.

Watakwambia umuone PEDIATRICIAN ili mtoto akadungwe machanjo mengine tena.
Ni kweli siku hizi watoto wengi wanasumbuliwa na usonji (Autism) inasemekana ni kutokana na chanjo wanazopigwa ambazo wanatumia thimerosal (Mercury), lakini hakuna tamko rasmi kutokana na hilo. Ni vigumu sana kumlea mtoto mwenye tatizo la Usonji. Hivyo ikiwezekana wazazi ambao watoto zao wameathirika na matatizo haya waishinikize serikali ili ifanye uchunguzi wa kina ili watu waweze kuwa na imani ya kupewa chanjo watoto zao. Kwani kuna nchi wamepiga marufuku chanjo zote za watoto zilizokuwa na Thimerosal, Kuna artice ambayo tuliipitia kuhusu Mercury, Vaccines, and Autism.
Na kuna makala nyingine kutoka kwenye website ya DownToEarth itakuwa vizuri kama itasomwa na kujua nini kinachoendelea.
 
Asante sana kwa kushindilia msumari.

Aione DR Mambo Jambo
 
Mpeleke kanisani akaombewe
 
Mwanao ana Usonji....! Utapoteza pesa kwa Waganga wa Kienyeji....!

Nina jirani yangu kahamia Mtaani hivi karibuni, ana Mtoto wa Kiume wa miaka 4 pia...! Mwanzoni nikasema Baba ake anamdekeza sana Mtoto...!

  • Mtoto analia bila sababu.
  • Ukimkataza kufanya Jambo hasikilizi.
  • Hawezi kuongea, japo anaongea Maneno machache lakini sio kwa Usahihi.
  • Hana marafiki.
  • Ameanza Kusoma Vidudu, walimu wanasema japo Mtoto haongei ila Ana akili Shupeni, na pale Mwalimu anapofundisha, anakua wa Kwanza kumuelewa Mwalimu kuliko Watoto wengine Timamu.

Kuna siku naongea na Baba wa Mtoto ananambia Mwanae na Usonji, naujua Ugonjwa wa Usonji, na huwa una Daraja tofauti, kuna Watoto wanaonhea japo taratibu, na wengine wanakua hawawezi kuongea...!

Nilimshauri ampeleke Mtoto Hospital, akasema alishanya hivyo, kwa sasa hakuna Vidonge ama Madawa ambayo Mtoto atapewa Hospital ili aanze kuongea, ila kuna Wataalamu Wachache wana Clinic za Watoto wenye Usonji kuwasaidia kuongea na kuwaweka sawa...! Na gharama ni kubwa wana charge mpaka 400,000 kila mwezi.

Huyu Mzazi hawezi kumudu, anachofanya ni kusoma Mtandaoni mbinu mbalimbali za kumsaidia mtoto then anamfanyia Mwanae.

Mfano moja ya mbinu, anakaa na Mtoto kwa saa kama moja, hafu ana cheza Nyimbo za Bongo fleva kwenye simu yake, huku akijifanya kama Nyimbo imemkolea, akiweka na Vibe, na mwanae nae akawa anamfatisha Baba ake kwa kutikisa kichwa, ana play nyimbo zile zile kwa saa nzima, ni baada ya siku 3 tu, mtoto kuna nyimbo akawa amezipenda, hawezi kuongea lakini unaona anavyohangaika kuimba kama Bubu.... Leo ni mwezi wa pili namsikia akiimba nyimbo lakini kaanza kutamka maneno machache kwenye Nyimbo anazopenda...!

Tiba ya Usonji ni Vitendo zaidi, tumia Google, tafuta group za Whatsapp za Wazazi wenye Watoto wenye Usonji.....!

Baada ya mwaka tu, mwanao hatabaki alivyo leo.
 
waone wataalam,lakini pia inatakiwa aishi na watoto wenzie kwa muda mrefu,wale pamoja,wacheze,walale pamoj hiyo itamsaidia sana.
 
Asante sana
 
Mnawaaharibu watoto kwa MACHANJO halafu mnaleta MAIGIZO ya USONJI.
 
Mpeleke iringa wilaya mufindi,Kijiji kinaitwa kiyowela,Kuna mzee anaitwa madati.mi mtaalamu hasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…